Misimamo ya Waafrika na Vita vya Ukraine

Misimamo ya Waafrika na Vita vya Ukraine

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Vita vyote huwa mwonevu na mwonewa.

Hata hivyo pana wimbi la mashabiki pia.

Kwanini waafrika tunatokea kukenua mno bila kusimamia misingi ya haki wala kuzingatia madhara?

Hata hivyo nisiache kutambua mchango wa Kenya na Afrika Kusini kwenye kumkemea hadharani, mbabe huyu wa vita bwana Vladimir Putin.

IMG_20220302_115525_094.jpg
 
Ha ha ha!! Nimecheka sana ila ndivyo tulivyo Miafrika, uwoga uwoga na kukenua, wachache ndio wenye uthubutu wa kulisema kama lilivyo.
 
Vita vyote huwa mwonevu na mwonewa.

Hata hivyo pana wimbi la mashabiki pia...
Wakati wewe ukiendelea kutumia nguvu kuubwa kuwatetea waUkraine, maelfu ya waAfrika wenzako waliopo Ukraine walia na kulalamikia ubaguzi unaofanywa na mamlaka za Ukraine kwa kuwazuia waAfrika weusi mpakani wasivuke kwenda nchi za jirani kupata hifadhi. Ila waUkraine, wahindi, waarabu na mataifa mengine waruhusiwa kupita mpakani

=====

SmartSelect_20220302-083328_Chrome.jpg

SmartSelect_20220302-122914_Chrome.jpg
 
Waafrika sisi tuna roho mbaya sana kuliko mataifa mengi na continents zingine
Nasema hivi kwa sababu katika vita wenzetu wanasaidiana kwa hali na mali pindi mmoja anapopata matatizo

Angalia Ukrainians wanavyopokelewa na Poland na mataifa mengine na huo ndio undugu na umoja

UK wanaanza kuwaandalia wakimbizi kuja kuishi na mpaka wanawaza kuhusu watoto watakao kuja kusoma wataenda shule zipi

Sisi Waethiopia au Wasomali wakikamatwa yaani mapolisi watawapiga picha na kuwafanya kama wahalifu na habari inawekwa kwenye tv huku mkuu wao akipiga nao picha kama kashika madawa ya kulevya

Hawaishii hapo mpaka hela zao watanyang’anywa na kinyimwa haki zao za msingi kabisa

Hatuna ubinadamu na sasa wengi wanafurahia watu wafe

Serikali haina msimamo na wananchi wanakuwa wabaya pia ila kama serikali Ina msimamo wa haki za binadamu na kuwasaidia ndugu zetu waafrika tungepata akili tofauti na za kwetu ambazo zimeganda
 
Wakati wewe ukiendelea kutumia nguvu kuubwa kuwatetea waUkraine, waAfrika wenzako waliopo Ukraine walia na kulalamikia ubaguzi unaofanywa na mamlaka za Ukraine kwa kuwazuia waAfrika weusi mpakani wasivuke kwenda nchi za jirani kupata hifadhi...

Pa kuanzia kulaani kwenye kadhia hii ni wapi?

Kwenye ubaguzi huu leo kwenye kujiokoa kumkimbia fedhuli au kwenye kumkomalia fedhuli kuacha kufurusha watu?

Pole sana Afrika kwa kupishana na misingi mizima ya haki.

Full kutapa tapa tu? Looh!
 
Wakishabikia NATO wa buza mnakaa kimya hamsemi, ila wakishabikia Warusi wa Tandale mnasema"acheni ushabiki watu wanakufa huko",watu kufa wanakufa tu Dunia nzima, Africa ya kati,Msumbiji,Rohingya,Popua Guinei na kwengineko kote uko kuna mauwaji ya kutisha.
 
Pakuanzia ni hapa alipoanzia Colonel Macgregor wa jeshi la Marekani.

Colonel Douglas Macgregor, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani anasema Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba, Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).

===

COL. DOUGLAS MACGREGOR: Let me just reiterate something. I, like you and millions of Americans, would prefer that the troops headed to Eastern Europe right now were headed to the Mexican border. But I’m also very concerned that we find a way to avoid a conflict with Russia. The first thing we have to do is acknowledge that Putin’s basic point, not just his point, the Russian government’s point, which they’ve made for 25 years, is valid. They don’t want U.S. forces and missiles and NATO troops immediately across the border in eastern Ukraine. Absolutely. We didn’t want them in Cuba, he doesn’t want them in eastern Ukraine.

We should acknowledge that. Stop pretending it’s a nonissue. It is a major issue for them. Let’s acknowledge it and then let’s get down to business and tell them fine, our concern at this point is we don’t want you to proceed west towards the polish border over the Dnieper River in Ukraine.
 
Wakishabikia NATO wa buza mnakaa kimya hamsemi, ila wakishabikia Warusi wa Tandale mnasema"acheni ushabiki watu wanakufa huko",watu kufa wanakufa tu Dunia nzima, Africa ya kati,Msumbiji,Rohingya,Popua Guinei na kwengineko kote uko kuna mauwaji ya kutisha.

Unayasoma wapi ya NATO hapo?

Hata Kingai, Mahita, Goodluck, Jumanne, Sirro na timu yao tunawananga vile vile kwa mafyongo yao. Sembuse NATO?

Huwezi kuona kosa mahali ila kulinganisha na kosa jingine?

Huoni dunia kuwa hatarini hapo ila umebakia kukenua tu?

Utu wako uko wapi wewe?
 
Pakuanzia ni hapa alipoanzia Colonel Macgregor wa jeshi la Marekani.

Colonel Douglas Macgregor, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani anasema Marekani ina nafasi ya kuepusha vita na Putin (Russia). Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya Wamarekani ni kukiri na kukubaliana na nukta ya msingi ya Putin (Russia), ambayo serekali ya Russia imeiweka wazi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba, Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).

===

COL. DOUGLAS MACGREGOR: Let me just reiterate something. I, like you and millions of Americans, would prefer that the troops headed to Eastern Europe right now were headed to the Mexican border. But I’m also very concerned that we find a way to avoid a conflict with Russia. The first thing we have to do is acknowledge that Putin’s basic point, not just his point, the Russian government’s point, which they’ve made for 25 years, is valid. They don’t want U.S. forces and missiles and NATO troops immediately across the border in eastern Ukraine. Absolutely. We didn’t want them in Cuba, he doesn’t want them in eastern Ukraine. We should acknowledge that. Stop pretending it’s a nonissue. It is a major issue for them. Let’s acknowledge it and then let’s get down to business and tell them fine, our concern at this point is we don’t want you to proceed west towards the polish border over the Dnieper River in Ukraine.

Kwa akili za kawaida si tungejikita kwenye hoja tukaachana na wanawake na watoto wasiokuwa na hatia?

Au ki Pinda Pinda na wauwawe tu?
 
Back
Top Bottom