Misimamo ya Waafrika na Vita vya Ukraine

Ukweli mtupu
 

Ubinafsi uliopitiliza ni kama huu hapa:

 
Hv unaujua ubaguz wahuko russia ww, nikwamba wew mweusi hakuna akupendae tujijali wenyewe

Sent from my DRA-LX2 using JamiiForums mobile app
Russia Kuna ubaguzi sana, ila Atleast serikali yao imesomesha Waafrika wengi Bure, hapa kwetu tu Angalia vichwa Vingapi vimesoma Urusi.

Magharibi wana Elimu Nzuri ila mpaka uwe unajiweza ama upate sponsor ndio unagusa vyuo vyao.
 
Russia Kuna ubaguzi sana, ila Atleast serikali yao imesomesha Waafrika wengi Bure, hapa kwetu tu Angalia vichwa Vingapi vimesoma Urusi.

Magharibi wana Elimu Nzuri ila mpaka uwe unajiweza ama upate sponsor ndio unagusa vyuo vyao.
Mwafrika asipojiongezea thamani yeye mwenyewe atajikuta kokote anakoenda hapendwi.

Ukiwacheki hao wanafunzi walioko Ukraine wa kiafrika wanaokimbia vita karibia wote wameenda huko kwa ufadhili wa nchi ya Ukraine. Pengine wangeenda huko kwa kujilipia na kuiingizia vyuo vya Ukraine fedha kama waarabu na wahindi wanavyofanya pengine wangefanyiwa ukarimu na askari wa border.

Ombaomba yeyote humu duniani hawezi kuwekwa kundi moja na kupewa thamani sawa na mtu anayejitosheleza!
 

Ukweli mchungu: "Omba omba anapotaka first class treatment kwa sababu naye ni binadamu."
 
Report zinaonesha wanajisomesha labda kama una source tofauti. Ukraine bado haijawa developed kama Nchi nyingi za Ulaya Na Ada si kubwa sana.

Na msitetee ubaguzi kwenye hii vita upo wazi wazi, na si kweli waarabu na wahindi wanaachiwa unless asijulikane wao pia wanabaguliwa.
 

Hakuna anayetetea ubaguzi. Lakini siyo tuanze na kupinga vita iliyopelekea watu kubaguliwa kwenye kuikimbia.

Yasemekana katika waliokimbia kura ya kulaani UN na sisi tumo!
 
By nature mzungu ni kiumbe mbaguzi, nadhani ni ile mifumo yao ya toka zama za kale ya ubwana na utwana.

Lakini nirudie tena (na hapa sitetei ubaguzi) waafrika tusipojiongezea uwezo wa kujitegemea tutaendelea kubaguliwa tu. Pamoja na vita ya kiuchumi iliyopo kati ya West and East yet watu wa China au wa Urusi wakitaka kuhamia Marekani au Ulaya wazungu wanawakaribisha kwa mikono miwili. Kwa nini, kwa sababu mchina na mrusi hawaendi Marekani na Ulaya kama ombaomba, wanaenda na ujuzi na maarifa na wakati mwingine na pesa za kutosha. Wakatu mwafrika akienda huko anaitwa mhamiaji haramu cause hana cha maana cha kuoffer zaidi ya kuwa tegemezi.

Tusipojifunza kutengeneza mambo yetu kuwa bora na sisi wenyewe kujiongezea ubora (na hui ndio msingi wa kujitegemea) tutabaki kuwa watu wa lawama hadi Kristo anarudi.
 

Mkuu wahamiaji haramu ni kama Mexico wanavyokatisha border kuingia America

Sasa hao Ethiopians wamekimbia kichapo cha kila siku na serikali yao dhalimu
Sasa wanakimbia ili kunusuru maisha yao
Wanaitwa Political Asylum sasa kwa nini wapigwe na kuonewa na kama wamehangaika kukimbia na ni waafrika wenzetu mbona kuna taratibu za kuwahudumia kitaifa na sheria za dunia zipo?

Kwa hiyo jinsi hao unaowaita wahamiaji haramu ilikuwa ni haki maiti zao kuwekwa kwenye viroba na kutupwa barabarani?

Kama tulivyoambiwa na waziri wakati huo?

Hakuna sheria yoyote inayosema mkimbizi aonewe na kudhalilishwa tena viongozi wa Africa ni majuha sana la sivyo nchi nyingi zingeshitaki kwa uonezi wa wananchi wao

Angalia kelele tunazopiga kwa ajili ya ndugu zetu sio waTamzania tu bali waafrika waliokwama Ukraine

Hitimisho muwe na huruma na binadamu wenzenu period
 
Mimi ni mmoja wapo ,Ukraine achapwe,ili liwe fundisho kwa wengine wenye uroho wa vipesa na offer kutoka US !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…