Misingi, itikadi za dini na mabomu ya kujitoa mhanga

Umeandika vizuri sana, ila nadhani ushawahi kusikia baadhi ya Waislamu wakilalamika kuwa wanadhurumiwa maslahi yao na kundi fulani lenye nguvu ya dhurma.
Nyanja ya Elimu imewahi kulalamikiwa sana na baadhi ya Waislamu, kuwa wanafelishwa kwa makusudi ili kuwadhoofisha kijamii.
Maeneo mengine ni kama, ajira, Afya, Sheria ( hapa wakadai mahakama ya Kadhi ighalimiwe na serikali ili ilinde maslahi yao) nk.
Baadhi ya makundi ya Kigaidi yamejibainisha wazi kuwa ni Jeshi la kutetea maslahi ya waislamu, hapa sio makundi yote ni baadhi kama Boko haram, na Al-Shabab.
Boko haram kwa mfano, maana yake ni, Utamaduni wa Kimagharibi ni Haramu, Utamaduni wa Kimagharibi unajumuisha Dini ya Kikristo ambayo nayo ni Haramu kwao wao.
Uhalali ni Utamadini wa Mashariki ya kati unaojumuisha Dini ya Kiislamu.
Hivyo asiye Muislamu kwa mtazamo wao ni mtu Haramu.
Ndio maana nikasema kuna baadhi ya makundi ya Kigaidi yameibuka ili kutetea Uislamu kwa hali na mali ili usimezwe na utamaduni wa Kimagharibi.
 
Aya haina ukomo itaendelea kutumika hadi siku ya mwisho,ndio maana hata mtu muovu anapokuijia mfano jambazi amekuja usiku kutaka kukudhuru na kuchukua mali zako unaruhusiwa kupambana nae kadri unavyoweza.
Kumbuka kuwa dini imekuja kwa mapokeo kwa maana kuna utofauti wa uelewa baina ya watu wa dini moja,hata kwa wakristo kuna wasabato ambao wanatofautiana ktk baadhi ya mambo na wakatoliki,hivyohivyo kwa waislam tofauti hizo zipo,uelewa hauwezi kuwa wa aina moja baina ya watu.
Mtu au kikundi cha watu atakapofanya jambo baya kwa kisingizio cha dini usiinyooshee kidole dini,hapo anakuwa anatumia dini kama mgongo wa kuficha uovu wake.
 
yaani ambacho nataka wewe ukielewe ni kwamba", wakubwa wenye huu ulimwengu" wanayatumia hayo mapungufu" ya hao wafia dini wanaolalamika kuwa wanaonewa na dini Fulani" ili waweze kusimika maslahi yao" wanajitangaza kuwa ni wakombozi wa hao wanaollamikA", wanaolalamik wanawaamini" na kuwa support " kumbe nyuma ya pazia wana malengo yao ya kuchimba madini" mafuta' ". so ill hayoyafnyike" nilazima" waidhohofishe" serikali iliyopo madarakani" n idondoshe wino" nakuingia nao mikataba" hivyo vikundi huwa vinatumiwa na mataifa makubwa yote " USA .RUSSIA" UFA, UINGEREZA"," etc .. but huwa vinajifanya kuitumikiA dini" kwakuwa " vinajua" kwamba sehemu kubwa ya jamii inakaliwa na watu ambao wanaimani za kidini" so wanAwachonganisha", umeshawahi kujiuliza " wanapata wapi pesa za " kujiendesha", " Kama kununua mafuta chakula na gharama za kununua silaha""
 
Pamoja na propaganda zote,kejeli,matusi dhidi ya uislam, bado uislam ndio dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani hasa America na Europe.
Kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2018 jina *Muhammad* limeongoza ktk majina wanayopewa watoto wanaozaliwa ndani ya UK (uingereza).Limeyashinda majina kama Harry,Jackson na william.
 


Haina haja ya kujiuliza, kwani si kama Uislam unaenea duniani bali wakimbizi toka hizo nchi za waarab wanakwenda Ulaya na hiyo dini yao, wakifika huko baada ya muda wanajiua kwa kujitwika mabomu kisa wanakuwa wanamiss kunyanyasika huko kwao. Hawajalazimishwa kwenda kuishi ukimbizini Ulaya ila wanashikwa na hasira za kutaka kujiua tu. Jana Denmark mwanamke mwarab aliyevaa hijab ameshitakiwa kwa kuvaa hijab, wazungu hawaoni umuhimu wa kuvaa kininja na wanasema kama unataka kuvaa kininja rudi kwenu ulikokukimbia. Nchi zingine zinataka kuleta sheria kama hii pia, hawataki upuuzi huu uenee Ulaya. Uholanzi nayo ukivaa hijab unakamatwa. Safi sana hii,
 
Povu la nini mtoto wa kike?jibu hoja nchi zote zenye waislam machafuko yana mkono wa makafiri.


Unataka jibu gani zaidi ya hilo nililokupa? Nikuulize nini tatizo la Sudan Kusini, nani yuko nyuma yake? Syria na Iran nani anawasimamia? Usijipige vidole kwa hasira nipe jibu sahihi.
 



Unaona sasa akili za kukopa zilivyo? Wale watoto wanaozaliwa Ulaya na kupewa jina la Mohammad si watoto wa kizungu bali ni watoto wa kikimbizi wa kiarab/waislam waliokimbilia Ulaya kuepuka vita vya kuuana wenyewe kwa wenyewe. Ni sawa tu na wewe ukimbilie Brazil ukazaa mtoto na mkeo mkamuita (Hasmoir), this doesn't mean kuwa dini yako imekuwa, huyo mtoto ni wako na ndivyo ilivyo Ulaya. Jiulize kwanini waarab wanapingwa Ulaya na hawatakiwi….sasa iweje Uislam uzidi kukuwa ikiwa waarab hawatakiwi na si Ulaya tu hata Marekani. Hivi nyie hizi data za kijinga mnazitoa wapi? Acheni kudanganyana jamani. Obama kabla ya kuachia madaraka, alipokea wakimbizi wa kiislam wengi sana toka hizo nchi tata za kiarab na Trump kaingia madarakani anawarudisha hawataki kuwaona Marekani, sasa huo Uislam umekuwa wapi?
 
Ukisikia Allah akbar sokoni we kimbia akuna kutafakari si dini si siasa we kimbiaaaaa[emoji23][emoji23]
Mtemi, Mbabe na Msema Hovyo DONALD F TRUMP alithibitisha kwa vitendo. Akiwa mkutanoni alisikia Mungu Mkubwa Mungu Mkubwa [Allah akbar Allah Akbar], akaanza kitete cha kutaka kukimbia.

Nakuunga Mkono. Kimbia ukiisikia usalimishe maisha yako
 

Enzi zile la Al kaida pale Afghanistan, opium ilikatazwa na wakafanikiwa kwa 90% , Ila Sasa imeshamiri kwa sana tu.
Al kaida hawakujitanua ile 9/11 ni inside job ili wapate kuanzisha Vita ila.....
 
Kule Iraq na Syria ISIS tangu walipotangaza Caliphate wanaua watoto wazee wake mwa waume na ukiangalia video zao wanafanya yote hayo ili kujenga dola ya Kiislamu sasa kwa muktadha huo jibu ninalopata ni kwamba dini ni confusion tuu maana kila mtu anafanya lake na kujustify anayofanya kwa kutumia kitabu hichohicho!
 
Hapana, "confusion " ni mtu kujitakia. Pengine labda unaweza ukajiuliza ni kwa nini nimekanusha hilo, Ni kwa sababu ya dibaji hii ndogo ifuatayo.

Uislam unarejelea, ni kama sheria. Kwa linalozungumzwa au kutendwa katika uislam ni lazima uoneshe rejelea yako kwa hayo. Qur'an, imeshuka ndani ya miaka 23, na kwa nini imekuwa hivyo? Ni kutokana na matukio, naam Qur'an imeshuka kutokana na matukio. Sura / aya ya aina yoyote katika Qur'an ni lazima uoneshe imeshukia wapi, kwa sababu zipi na mtume ameitafsiri vipi. ISIS kama wanadai ushahidi wao unatokana na aya/ sura katika Qur'an, Uislam na waislam watahoji; watuambie ni sura/ aya ipi, imeshukia wapi, na lazima uelezee sababu ya kushuka ni ipi na Mtume ameitafsiri vipi? Kuna aya za vita, kuna ahadithi zinazozungumzia vita lakini uislam na waislam watahoji tupeni rejelea na mantiki ya hizo aya/ahadith kama Mtume alivyokusudia. Na katika uislam hakuna rai maadam Mungu na Mtume wake wamesema hivi basi hakuna kupinga. Ukiwa kinyume na hilo umetoka moja kwa moja kwenye uislam.

Katika uislam vita imehalalishwa ila imehalalishwa kimisingi yake na kanuni zake. Mathalani muislam ameruhusiwa kupigania dini yake na kuipigania nchi yake ila uislam umeweka hali ya namna gani inayokupasa mpaka ufikie hiyo hatua. Moja ya misingi yake Imekataza usiue wanawake, watoto, wazee, usiharibu vyanzo ambavyo ni vyenye manufaa kwa binadamu na hakuna kumlazimisha mtu/watu katika dini. Kama kulazimisha angelazimisha Mungu mwenyewe watu wote wangekua dini moja.

Uislam, wasiokuwa waislam umewaweka katika makundi mawili. Wapo ambao wasiyokuwa waislam wenye ukarimu, upole na wenye kupenda amani na wenye kupenda haki. Hata wakiwa kinyume na hayo, maadam hawafanyi uadui juu yenu uislam unakutaka uishi nao kwa wema. Na kwa wale ambao wamejitolea nafsi zao na mali zao kupambana na uislam, basi uislam unakutaka mpambane nao mithili ya wao kama wanavyopambana nanyi na wala msichupe mipaka kwa yale wanayowafanyia.

Makundi ya kigaidi Dunia nzima hakuna hata moja linalofuata uislam na si wamba hawajui; wanajua na Mungu atawalipa kwa istihzai wanayoifanya. Usama mwenyewe alipokuwa gaidi mama yake alilia sana na kumwambia mwanae mambo anayoyafanya si sahihi.
 
Mambo hayo hadi kwenye biblia yapo hayajaanza leo,ndiyo maana mie huwa naona kuna tofauti ya dini na imani tu.
 
Kwahiyo wewe kwa kutumia akili yako unakubali kabisa haya makundi ya kigaidi ajenda yao ya kufanya ugaidi ni kutaka watu wawe waislamu?

Yani kwa mfano hao boko haram hufanya yale machafuko ili lengo wasio waislamu wawe waislamu?
 
Inaonesha imani zao za dini wazungu hazina athari kwenye maisha yao na tamaduni zao na ndiyo maana wanaendana nazo bila tabu yeyote,hivyo inaonekana uislamu ndio tishio la tamaduni zao wazungu walizozizoea.
 
Kwahiyo wewe kwa kutumia akili yako unakubali kabisa haya makundi ya kigaidi ajenda yao ya kufanya ugaidi ni kutaka watu wawe waislamu?

Yani kwa mfano hao boko haram hufanya yale machafuko ili lengo wasio waislamu wawe waislamu?
Unakumbuka wale watoto wa kike zaidi ya mia nne wa shule ya Sekondary ya Chibok huko Nigeria waliotekwa na Boko Haramu jambo la kwanza kabisa walifanyiwa nini ?
Wote walilazimishwa kusilimu na kuwa waislamu.
Na wakafundishwa kwanza Uislamu kwa bidii zote.
Jiulize kwanini Boko Haramu waliwafanyia hivyo.
Je wakifanikiwa kuitawala Nigeria na kama hawataingiliwa na Mataifa ya nje watu wa Nigeria wasio waislamu watapataje uhuru wa kuabudu chini ya utawala wao.
Sisi tusio waislamu tunajua kabisa malengo ya baadhi ya hayo makundi ya kigaidi ni kusaidia kueneza Uislamu kwa nguvu kama walivyo fanyiwa watoto wa Chibok au walivyo uliwa Wanafunzi wa Kikiristo wa Chuo cha Garissa Kenya na magaidi wa Alshababu baada ya kuwaondoa wanafunzi wa Kiislamu wote.
Sisi Wakristo usifikiri tumelala ni kwamba tunawaangalia kwa tahadhari zote na kama vikundi hivi vikiendelea kutudhurumu kwa kiasi cha kuvichoka tutaingia vitani mazima mazima na hapo ndipo dunia itakapo tikisika kwa kishindo kikuu.
Nadhani wewe unayajua haya matukio na matendo haya wanayofanya magaidi hutaki kuyaona kama ni dhulma dhidi ya Wakristo.
ISS wana wateka na kuwaua Wakristo kila kukicha kwa kuwachinja, ila kwakuwa ni Wakristo wewe unajifanya huoni hivyo vitendo vyao.
Nakuhakikishia Dawa yao bado inachamka.
Tumia vizuri Akili yako.
 
Mkuu basi utakuwa haujatumia akili sawa sawa bali unatumia hisia,madhara yanayo sababishwa na hayo makundi huyapata watu wote haijarishi ni muislamu au sio muislamu Ila wewe mkuu umeamua kuchagua kuzungumzia hayo matukio machache kwa sababu ya hisia ulizonazo.

Maana hakuna muislamu ambaye hujiona yupo salama mbele ya hayo makundi kisa tu yeye muislamu.
 
Yako matukio mengi sana mabaya ambayo hayo makundi yanawafanyia Wakristo.
Kule Afrika ya kati waliwaua Wakristo kwa makusudi kabisa mpaka baadhi ya Wakristo wakaunda kikundi chao cha Antibaraka ili kujilinda na dhulma dhidi yao, kikundi hicho kilifanya mauaji ya kutisha kwa lengo la kulipa kisasi. Matokeo yake nchi ikakosa Amani kwa kipindi kirefu.
Hayo makundi adui yao namba moja ni Wakristo, namba mbili ni watu wa imani nyingine, namba tatu ni Waislamu wasiowaunga mkono.
Ndio maana kila mahali yanapoanzishwa na kudumu ni pale penye makazi ya waislamu, maana baadhi yao wanashiriki kuyaanzisha na kuyafadhiri, na asilimia kubwa ya watu wa makundi hayo ni waislamu.
Ni lazima tuelezane ukweli kwa nia ya Kujenga jamii yenye Amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…