Picha kama hiyo mimi naisoma hivi:
Naona waTanzania watulivu kabisa wanaotafuta haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wao wanaopenda wawaongoze miaka mitano.
Watu hawa watakwenda kupiga kura kutimiza adhma yao hiyo, kwa utulivu bili ya rabsha zozote.
Halafu baada ya hapo, kura hizo kundi la watu wanaamua hazina thamani yoyote, na wala hazihesabiki katika kumpata kiongozi atakayetangazwa.
Ninaishia hapo katika mtiririko huo wa mawazo yangu.
Hapana. Kabla hujanirukia kwa jazba, sijaandika kwamba waTanzania wengine wapo kwenye mistari mingine, nao wametulia kama hawa. Wao pia wanastahiri heshima yao na kama ndio watakuwa wengi kwa kura zao za haki, basi wana haki ya kupata mtu wanayemtaka, nasi sote ambao hatukumpa kura zetu tutaheshimu maamuzi hayo bila ya shari kama ni matokeo ya haki.