Mita mpya za maji ni kama king’amuzi, maji yakiisha inaji-lock

Hii system niliikuta Mbeya, Mwanjelwa na Soweto.
 
Wasoma Mita waliopo kazini kwa Sasa wataekekea wapi?
kusoma mita ni kazi ya kikoloni ktk zama hizi za kidigitali.
sasa wafundishwe namna ya kuzisoma kwenye computer sio manual tena.
tena sasa watakuwa wamepunguziwa kazi ya kuzurura, watatulia ofisini.
tuko ktk zama za sayansi na tecknologia.
 
Hili ndilo litakuwa mwarobaini wa tatizo la kubambikiana Bills! Unatumia maji ya 3000 unapewa bill ya 12000.
Extrovert mzee wa kicheko, nakupa angalizo yasije kutokea yale ya tanesco mfumo uka buma siku iyo hamtakoga😅😅😅😅
 
Nahisi, itakuwa na betri, solar na kakompyuta kadogo ndani kwa ndani. Ni nzuri kwakweli! Ndiyo maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Hata Tanesco ilikuwa unaletewa postpaid, baadae luku za nje, na sasa hivi unaingiza umeme kwa rimoti tu ukiwa ndani!
 
Mbona hizo Iringa mjini zimefungwa kitambo,ni mwaka wa pili sasa.
 
Kivip,wale wa kushea mita moja weng je,wahama nayo vp
 
Safi sana! Yahooooo! Nipo Arusha, kilio changu siku zote ni ubambikiwaji wa bill! Familia yangu ni ta watu wanne (mimi, mke wangu, Mjukuu na binti wa kazi), bili inakuja Tsh. 89,500 kwa mwezi! Utadhani nina kiwanda. Cha kusikitisha huduma yao kwa mteja ni ya hovyo sijapata ona nchi hii. Ukienda lalamika wana printi bili za nyuma a kisha kukutumia SMS za vitisho kwenye simu. Hawataki kujua chanzo cha tatizo ni nini! Sasa nimeamua siwalipi waje wachukue mita yao!
 
Siku network ikigoma ndio wenye vyoo vya ndani mtazungumza
 
Da asavali zile bili za kutubambikia ndio zitakuwa mwisho wake na wenzangu mimi wale vishoka wa kuchezea na kurekebisha mita ili apate chochote hatima yao ndio imefikia ukingoni,sijui walioajiriwa kazi ya kusoma mita watafanya kazi gani sasa kwa maana walikuwa wanakaa tuvijiweni wakituandikia bili za uongo na hata walikuwa hawasomi mita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…