Mita mpya za maji ni kama king’amuzi, maji yakiisha inaji-lock

Hili ndilo litakuwa mwarobaini wa tatizo la kubambikiana Bills! Unatumia maji ya 3000 unapewa bill ya 12000.
Wale jamaa waliokuwa wanapaswa kupita mitaaani kusoma mita manually walikuwa wanapika sana data. Unakuta hwajafika hata eneo la tukio wapo kwa mama ntilie wana jaza jaza tu taarifa za bill za uongo,
 
Sio sawa kabisa.
Wananchi wataumia.

Matumizi ya maji sio sawa na umeme
 
Tumezibuni na kutengeneza wenyewe au tumezitoa kwa MABEBERU?
 
Msishangilie sana tatizo litakuja kwenye upatikanaji hizo meter!! Sio mara ya kwanza luku za maji kuletwa ; namkumbuka enzi ya Lowassa akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na bwana mmoja akiitwa engineer Kaaya aliyekuwa mkuu wa DAWASCO alizileta hizi meter halafu zikapotea!!! Hopefully, safari hii zitakuwepo za kutosha na hakutakuwa na mizengwe ya milungula!!!
 
Hii unapanga nyumba iliyo na kina dada, hawavumilii kukosa maji, kuliko wanaume ambao anaweza kutoboa mwezi hana tone la maji ndani.
Khaa mkuu hata kama exaggeration hii imezidi sasa
 
Mbona uko hasi
Uhasi wangu una sababu na ukweli. Maendeleo yana gharama, na siku zote mtumiaji ndio mlipaji. Ujio wa mitaa si wa kufurahia, una gharama. Moja wapo ni watu kukosa maji hapo program inapotibuliwa makusudi ilu programmer apate hela.
 
Kubambikiwa bill kwenye mita huwa ni jambo la muda. Msoma mita hana uwezo wa kusogeza mita mbele, zinazo ongezwa ni tarakimu, ambao hupingwa kwa physical reading, na ukiwafikisha mahakamani, with proven evidence, una fidia kubwa.
 
Kwahy wale wafanyakaz wanazunguka kusoma meters watakosa kazi
Yani wajiandae. Teknolojia huwa inakuja na positive and negative effects. Wajifunze ufundi wa hizo meters ili waendelee kuwa relevant.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…