Wakuu habari zenu,leo kidogo tuzungumzie kuhusu hili la mitandao ya kijamii.
Siku hizi maisha yamegeuka sana,ni ngumu sana kudeal na stress na msongo wa mawazo hasa pale unapokuwa unapitia kipindi kigumu katika maisha.
~Umeachana na mpenzi wako uliyempenda sana,kesho unamuona facebook,instagram or WhatsApp anakula maisha na mpenzi mpya tena aliyekuzidi viwango.
~Unaperuzi facebook mara unakutana na picha za jamaa uliowaacha shule tena wale vilaza kabisa wanakula good time,wakati huo wewe upo tu nyumbani kwa shemeji na vyeti vyako vya chuo havina kazi.
~Hujabahatika kupata mtoto, unapita mitandaoni watu wanapost picha za birthday za watoto wao, huku upande wako mawifi wanakusakama kila kukicha kwamba unakula tu na kujaza choo.
~Au unapitia chats kwenye group unakutana na mapicha wenzako wote uliosoma nao wanaolewa huku wewe upo nyumbani umezalishwa huna mbele wala nyuma.
~Ni ngumu sana kukutana na hizo mambo ukapotezea,lazima zitakuathiri kwa kiasi flani, na mara nyingi husababisha watu kupata hali ya upweke, mfadhaiko,wivu uliopindukia au kumfanya mtu awe depressed na mara chache watu huishia kujiuwa kabisa.
______________________________________
Youngblood
Kanuni 10 za kushinda sononeko katika mitandao ya jamii.
1. Usijilinganishe na watu wengine. Jilinganishe na wewe mwenyewe wa kabla. Kuna mtu mwanamme alimzidi mshahara mwanamke kazini, akashangaa huyu mwanamke mbona anavaa nguo za fahari, ana gari la fahari, wakati namzidi mshahara? Kumbe mwenzake anahudumiwa na mumewe.
2. Furahia mafanikio ya wenzako. Kuwa na kijiba cha roho kwa sababu mwingine kafanikiwa si tabia mbaya tu, ni tabia inayokupa sononeko lisilo na sababu.
3. Badala ya kusononeka watu wengine wanapofanikiwa, jaribu kutafuta sababu za mafanikio yao. Kuna watu wengine wanaonekana wamefanikiwa lakini wamefanya mambo ya aibu kama umalaya na kuuza madawa ya kulevya. Kwangu kupata hela kwa njia hizo si mafanikio.
4. Tambua si kila anayeonekana kafanikiwa amefanikiwa kweli, na si kila anayeonekana hajafanikiwa hajafanikiwa. Waingereza wanasema "everything that glitters, is not gold". Kuna watu wanajua kujiweka kama wamefanikiwa katika mitandao ya jamii, wakati hawana lolote. Halafu kuna kina Said Bakhressa kuwaona mitandao ya jamii wanajitapa ni kazi sana.
5. Tumia muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli za maendeleo, kusoma, kufanya kazi, kufanya biashara na kadhalika, zaidi ya kuangalia mitandao ya jamii.
6. Pambana na hali yako. Kama unataka mambo makubwa, fanya utafiti wa kitu kipi kitakutoa na kukupa kipato na nafasi ufanye makubwa.
7. Ukishindwa kabisa kubadili hali yako, kubali ukweli na kubali maisha yako. Ukiwa na tamaa kamwe huwezi kutosheka hata uwe mfalme wa dunia utataka utawale na Mars. Ukiwa mtu wa kuridhika unaweza kuwa na amani kwa shamba lako dogo tu. Inawezekana mwenye kidogo akaishi kwa amani kuliko mwenye kingi.
8. Elewa kwamba kujionesha sana mitandao ya jamii kuna ku expose kwa mengi. Kuna wezi wanaangalia nani ana mali gani tumuibie, kuna madanga yanataka kufuatilia watu, kuna ma hackers wanataka ku hack na ku blackmail. Wanaojionesha sana mitandaoni wana ji expose kwa wote hao.
9. Tambua mitandao ya jamii ni chanzo cha wivu na magomvi mengi katika jamii. Wanaojinadi sana wanapata magomvi sana.
10. Tambua watu wengi huheshimika sana mpaka wanapoonekana upumbavu wao kwenye mitandao ya jamii. Unavyozidi kutumia muda kwenye hii mitandao na kuipa nguvu, ndivyo unavyozidi kuanika upumbavu wako.