Mitandao ya kijamii siku hizi imekuwa chanzo kikubwa cha stress na msongo wa mawazo kwa vijana

That's the spirit my man.

Zile colognes kwa sasa zimezidi mara mbili.

Na tangu siku ile sijawahi tena kupost picha.

Maana ilikuwa mpaka Nyani Ngabu mtu wa ma cologne hajaamini kama picha ya kwangu, alifikiri nimeiokota kwenye internet.

Na mimi nilijua watakuwapo watu wa kuhoji, kwa hiyo nilivyopiga picha niliweka kikaratasi nimeandika "Kiranga".

Nikamwambia Nyani Ngabi hebu zoom katikati ya picha chini utaona salamu zako hapo.

Mwenyewe alizima fegi, alimeza moshi na kuutolea masikioni.

Jivin'.

Ha ha ha, ulivunja sana siku ile. Nadhani ndiyo mwanzo wa watu kupunguza kupost post vitu baada ya wewe kupiga gape kubwa vile.

Kuna kipindi nilikuwa so obsessed na kuangalia Sneaker Rooms za Ma-Star, kina Dj Khaled, Chris Brown, Rick Ross na wengine, kuna mchezaji wa Houston P.J Tucker alinifunikia balaa, sasa nilivyoona kwako ile ya perfume nikaona kabisa inawezekana, siyo mpaka uwe star kuwa na vitu vya namna ile.

Nimeshaanza taratibu kujaza viatu, ingawa mchina amejaa sana, ila nikibahatisha orijino naweka sehemu line yake.

Ulitisha sana mkuu.
 
Mambo ya kawaida tu. Kipe roho kitu inataka, lakini angalia usiue bendi.

Kizuri zaidi ni roho ya kitajiri, hizi mali mafarao walizikwa nazo halafu zikawa sababu za wahuni kufukua makaburi yao.

Tutaziacha tu.

Hivyo tujikite kuishi vizuri na kutengenezea wengine njia kwa nia safi.
 
Kizuri ni roho ya kitajiri.

...tujikite kuishi vizuri na kutengenezea wengine njia kwa nia safi.

Hizi sentensi mbili zimenibariki, thank you man.
 
That's the spirit my man.

Zile colognes kwa sasa zimezidi mara mbili.

Nilikuta watu wanaongelea perfumes na colognes, na mimi kama kawaida yangu si mgumu wa kuchangia kwenye hoja ninayoipenda.

Na tangu siku ile sijawahi tena kupost zile picha.

Maana ilikuwa mpaka Nyani Ngabu mtu wa ma cologne hajaamini kama picha ya kwangu, alifikiri nimeiokota kwenye internet.

Na mimi nilijua watakuwapo watu wa kuhoji, kwa hiyo nilivyopiga picha niliweka kikaratasi nimeandika "Kiranga".

Nikamwambia Nyani Ngabi hebu zoom katikati ya picha chini utaona salamu zako hapo.

Mwenyewe alizima fegi, alimeza moshi na kuutolea masikioni.

Jivin'.
Hahahahhaaa...
 
Wakuu habari zenu,leo kidogo tuzungumzie kuhusu hili la mitandao ya kijamii.

Siku hizi maisha yamegeuka sana,ni ngumu sana kudeal na stress na msongo wa mawazo hasa pale unapokuwa unapitia kipindi kigumu katika maisha.

~Umeachana na mpenzi wako uliyempenda sana,kesho unamuona facebook,instagram or WhatsApp anakula maisha na mpenzi mpya tena aliyekuzidi viwango.

~Unaperuzi facebook mara unakutana na picha za jamaa uliowaacha shule tena wale vilaza kabisa wanakula good time,wakati huo wewe upo tu nyumbani kwa shemeji na vyeti vyako vya chuo havina kazi.

~Hujabahatika kupata mtoto, unapita mitandaoni watu wanapost picha za birthday za watoto wao, huku upande wako mawifi wanakusakama kila kukicha kwamba unakula tu na kujaza choo.

~Au unapitia chats kwenye group unakutana na mapicha wenzako wote uliosoma nao wanaolewa huku wewe upo nyumbani umezalishwa huna mbele wala nyuma.

~Ni ngumu sana kukutana na hizo mambo ukapotezea,lazima zitakuathiri kwa kiasi flani, na mara nyingi husababisha watu kupata hali ya upweke, mfadhaiko,wivu uliopindukia au kumfanya mtu awe depressed na mara chache watu huishia kujiuwa kabisa.

______________________________________
Youngblood
Upo sahihi sana mkuu, japo maigizo pia ni mengi sana
 
Balaaa, hata bongo wapo tenashara
Screenshot_20190926-113529_BBC%20News.jpeg
Screenshot_20190926-113544_BBC%20News.jpeg
Screenshot_20190926-113550_BBC%20News.jpeg
Screenshot_20190926-062625_BBC%20News.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_20190926-062625_BBC%20News~2.jpeg
    Screenshot_20190926-062625_BBC%20News~2.jpeg
    67.2 KB · Views: 15
That's the spirit my man.

Zile colognes kwa sasa zimezidi mara mbili.

Nilikuta watu wanaongelea perfumes na colognes, na mimi kama kawaida yangu si mgumu wa kuchangia kwenye hoja ninayoipenda.

Na tangu siku ile sijawahi tena kupost zile picha.

Maana ilikuwa mpaka Nyani Ngabu mtu wa ma cologne hajaamini kama picha ya kwangu, alifikiri nimeiokota kwenye internet.

Na mimi nilijua watakuwapo watu wa kuhoji, kwa hiyo nilivyopiga picha niliweka kikaratasi nimeandika "Kiranga".

Nikamwambia Nyani Ngabi hebu zoom katikati ya picha chini utaona salamu zako hapo.

Mwenyewe alizima fegi, alimeza moshi na kuutolea masikioni.

Jivin'.
Itume na humu tuoshe macho kidogo ama tupe link mkuu
 
Wakuu habari zenu,leo kidogo tuzungumzie kuhusu hili la mitandao ya kijamii.

Siku hizi maisha yamegeuka sana,ni ngumu sana kudeal na stress na msongo wa mawazo hasa pale unapokuwa unapitia kipindi kigumu katika maisha.

~Umeachana na mpenzi wako uliyempenda sana,kesho unamuona facebook,instagram or WhatsApp anakula maisha na mpenzi mpya tena aliyekuzidi viwango.

~Unaperuzi facebook mara unakutana na picha za jamaa uliowaacha shule tena wale vilaza kabisa wanakula good time,wakati huo wewe upo tu nyumbani kwa shemeji na vyeti vyako vya chuo havina kazi.

~Hujabahatika kupata mtoto, unapita mitandaoni watu wanapost picha za birthday za watoto wao, huku upande wako mawifi wanakusakama kila kukicha kwamba unakula tu na kujaza choo.

~Au unapitia chats kwenye group unakutana na mapicha wenzako wote uliosoma nao wanaolewa huku wewe upo nyumbani umezalishwa huna mbele wala nyuma.

~Ni ngumu sana kukutana na hizo mambo ukapotezea,lazima zitakuathiri kwa kiasi flani, na mara nyingi husababisha watu kupata hali ya upweke, mfadhaiko,wivu uliopindukia au kumfanya mtu awe depressed na mara chache watu huishia kujiuwa kabisa.

______________________________________
Youngblood
Kila mtu anakipaumbele chake
 
Kweli kabisa, kuna kipindi niliacha kuingia mitandaoni baada ya kuona kuna vitu vinaniumiza sana,
Mitandao pamoja na uzuri wake lakini imekuja kupunguza muktadha wa kupata rafiki, siku hizi unabofya tuu tayari ushapata rafiki
 
Wakuu habari zenu,leo kidogo tuzungumzie kuhusu hili la mitandao ya kijamii.

Siku hizi maisha yamegeuka sana,ni ngumu sana kudeal na stress na msongo wa mawazo hasa pale unapokuwa unapitia kipindi kigumu katika maisha.

~Umeachana na mpenzi wako uliyempenda sana,kesho unamuona facebook,instagram or WhatsApp anakula maisha na mpenzi mpya tena aliyekuzidi viwango.

~Unaperuzi facebook mara unakutana na picha za jamaa uliowaacha shule tena wale vilaza kabisa wanakula good time,wakati huo wewe upo tu nyumbani kwa shemeji na vyeti vyako vya chuo havina kazi.

~Hujabahatika kupata mtoto, unapita mitandaoni watu wanapost picha za birthday za watoto wao, huku upande wako mawifi wanakusakama kila kukicha kwamba unakula tu na kujaza choo.

~Au unapitia chats kwenye group unakutana na mapicha wenzako wote uliosoma nao wanaolewa huku wewe upo nyumbani umezalishwa huna mbele wala nyuma.

~Ni ngumu sana kukutana na hizo mambo ukapotezea,lazima zitakuathiri kwa kiasi flani, na mara nyingi husababisha watu kupata hali ya upweke, mfadhaiko,wivu uliopindukia au kumfanya mtu awe depressed na mara chache watu huishia kujiuwa kabisa.

______________________________________
Youngblood
Kuna ukweli kwa mbaaali.
 
Kweli kabisa
Hahahhaaa mitandao inawafanya wadada wengi wamekuwa inferior
Akiangalia wadada wenzake wanapost wapo soft
Chuchu saa sita
Kiuno nyigu

Halafu yeye akijitizama ni kama mimi basi anapoteza ujasiri,
Anaanza kumuabudu mtu na editing apps !

Kumbe you're beautiful the way you are!
 
Yes ni kweli psychology inasema hivyo.
Nilichokigundua utakuta wale ambao mara nyingi wanapost picha za kuonyesha furaha na kuwa na Mali Kwenye social media ndio hali halisi ni kinyume chake.
Ukiona mtu anaweka sana picha ya Me/Ke na kuonyesha jinsi gani anampenda mkewe kiuhalisia wapo Kwenye ugomvi mzito.
 
Umenena vyema sana mkuu
Kanuni 10 za kushinda sononeko katika mitandao ya jamii.

1. Usijilinganishe na watu wengine. Jilinganishe na wewe mwenyewe wa kabla. Kuna mtu mwanamme alimzidi mshahara mwanamke kazini, akashangaa huyu mwanamke mbona anavaa nguo za fahari, ana gari la fahari, wakati namzidi mshahara? Kumbe mwenzake anahudumiwa na mumewe.

2. Furahia mafanikio ya wenzako. Kuwa na kijiba cha roho kwa sababu mwingine kafanikiwa si tabia mbaya tu, ni tabia inayokupa sononeko lisilo na sababu.

3. Badala ya kusononeka watu wengine wanapofanikiwa, jaribu kutafuta sababu za mafanikio yao. Kuna watu wengine wanaonekana wamefanikiwa lakini wamefanya mambo ya aibu kama umalaya na kuuza madawa ya kulevya. Kwangu kupata hela kwa njia hizo si mafanikio.

4. Tambua si kila anayeonekana kafanikiwa amefanikiwa kweli, na si kila anayeonekana hajafanikiwa hajafanikiwa. Waingereza wanasema "everything that glitters, is not gold". Kuna watu wanajua kujiweka kama wamefanikiwa katika mitandao ya jamii, wakati hawana lolote. Halafu kuna kina Said Bakhressa kuwaona mitandao ya jamii wanajitapa ni kazi sana.

5. Tumia muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli za maendeleo, kusoma, kufanya kazi, kufanya biashara na kadhalika, zaidi ya kuangalia mitandao ya jamii.

6. Pambana na hali yako. Kama unataka mambo makubwa, fanya utafiti wa kitu kipi kitakutoa na kukupa kipato na nafasi ufanye makubwa.

7. Ukishindwa kabisa kubadili hali yako, kubali ukweli na kubali maisha yako. Ukiwa na tamaa kamwe huwezi kutosheka hata uwe mfalme wa dunia utataka utawale na Mars. Ukiwa mtu wa kuridhika unaweza kuwa na amani kwa shamba lako dogo tu. Inawezekana mwenye kidogo akaishi kwa amani kuliko mwenye kingi.

8. Elewa kwamba kujionesha sana mitandao ya jamii kuna ku expose kwa mengi. Kuna wezi wanaangalia nani ana mali gani tumuibie, kuna madanga yanataka kufuatilia watu, kuna ma hackers wanataka ku hack na ku blackmail. Wanaojionesha sana mitandaoni wana ji expose kwa wote hao.

9. Tambua mitandao ya jamii ni chanzo cha wivu na magomvi mengi katika jamii. Wanaojinadi sana wanapata magomvi sana.

10. Tambua watu wengi huheshimika sana mpaka wanapoonekana upumbavu wao kwenye mitandao ya jamii. Unavyozidi kutumia muda kwenye hii mitandao na kuipa nguvu, ndivyo unavyozidi kuanika upumbavu wako.
 
Mkuu umenigusa sana nikionaga watu na watoto nahisi kama wao ni special sana aisee..[emoji22]
Unachokisema ni kweli wakati mwingine unamu unfollow mtu maana anachangia hoja kubwa ya kukunyanyasa kifikra bila yeye kujua
Kuna watu yani since day 1 wao mambo yao hayajawahi kupinda ..bora Jf hatuonani aisee
Nakazia hapa
 
Back
Top Bottom