Kanuni 10 za kushinda sononeko katika mitandao ya jamii.
1. Usijilinganishe na watu wengine. Jilinganishe na wewe mwenyewe wa kabla. Kuna mtu mwanamme alimzidi mshahara mwanamke kazini, akashangaa huyu mwanamke mbona anavaa nguo za fahari, ana gari la fahari, wakati namzidi mshahara? Kumbe mwenzake anahudumiwa na mumewe.
2. Furahia mafanikio ya wenzako. Kuwa na kijiba cha roho kwa sababu mwingine kafanikiwa si tabia mbaya tu, ni tabia inayokupa sononeko lisilo na sababu.
3. Badala ya kusononeka watu wengine wanapofanikiwa, jaribu kutafuta sababu za mafanikio yao. Kuna watu wengine wanaonekana wamefanikiwa lakini wamefanya mambo ya aibu kama umalaya na kuuza madawa ya kulevya. Kwangu kupata hela kwa njia hizo si mafanikio.
4. Tambua si kila anayeonekana kafanikiwa amefanikiwa kweli, na si kila anayeonekana hajafanikiwa hajafanikiwa. Waingereza wanasema "everything that glitters, is not gold". Kuna watu wanajua kujiweka kama wamefanikiwa katika mitandao ya jamii, wakati hawana lolote. Halafu kuna kina Said Bakhressa kuwaona mitandao ya jamii wanajitapa ni kazi sana.
5. Tumia muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli za maendeleo, kusoma, kufanya kazi, kufanya biashara na kadhalika, zaidi ya kuangalia mitandao ya jamii.
6. Pambana na hali yako. Kama unataka mambo makubwa, fanya utafiti wa kitu kipi kitakutoa na kukupa kipato na nafasi ufanye makubwa.
7. Ukishindwa kabisa kubadili hali yako, kubali ukweli na kubali maisha yako. Ukiwa na tamaa kamwe huwezi kutosheka hata uwe mfalme wa dunia utataka utawale na Mars. Ukiwa mtu wa kuridhika unaweza kuwa na amani kwa shamba lako dogo tu. Inawezekana mwenye kidogo akaishi kwa amani kuliko mwenye kingi.
8. Elewa kwamba kujionesha sana mitandao ya jamii kuna ku expose kwa mengi. Kuna wezi wanaangalia nani ana mali gani tumuibie, kuna madanga yanataka kufuatilia watu, kuna ma hackers wanataka ku hack na ku blackmail. Wanaojionesha sana mitandaoni wana ji expose kwa wote hao.
9. Tambua mitandao ya jamii ni chanzo cha wivu na magomvi mengi katika jamii. Wanaojinadi sana wanapata magomvi sana.
10. Tambua watu wengi huheshimika sana mpaka wanapoonekana upumbavu wao kwenye mitandao ya jamii. Unavyozidi kutumia muda kwenye hii mitandao na kuipa nguvu, ndivyo unavyozidi kuanika upumbavu wako.