Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Toka Uhuru hata baba wa taifa hakuwahi kufikiria kutufungia mitandao hata siku moja , mnajitapa majukwaani etu mnawaenzi waasisi wetu kwa lipi, agenda ya siri kutuua watanzania wote imejulikana endeleeni, safari hii ni ya wote nchi ni ya wote sio ya mtu mmoja, ni sawa na mhasibu aibe mali za ofisi halafu apambane na kila mtu asimuhoji kuhusu wizi wa mali za ofisi.

TUkutane kesho kwenye sanduku la kura.

MUNGU IBARIKI NA UIPONYE TANZANIA
 
Nimeona na mataga huko wanalialia huko dawa ishaanza kuingia walidhani hali itakua kwa upendeleleo ! Nachojiuliza mtu kama amejenga flyover sjui mabwawa na kusema anakubalika why afanye traffic jam ya internet?
Mpaka WhatsApp imegoma
 
Kati ya vitu vinavyokera ni hivi. Yaani siamini Kama kupashana habari kipindi cha uchaguzi ni hatari kwa usalama wa taifa kiasi hiki. Nafikiri kuna mifumo ya kiutawala tuliipokea tukiwa na mihemiko ila hatukuwa tayari kuiishi. Zama hizi kuzimiana mitandao na internet si tu ni kuwanyima wananchi haki ya kupashana habari bali ni kukosa maono na kuwajulisha kuwa kuna jambo lisilo la kawaida ambalo si vizuri kwao kulijua.
 
Back
Top Bottom