Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Uchaguzi 2020 Mitandao ya kijamii Tanzania yawa restricted. YouTube, WhatsApp, Twitter, JamiiForums na Telegram zimeguswa - Oktoba 27, 2020

Najaribu kuingia YouTube lakini inagoma, kama nusu saa iliyopita nilikuwa naipata.

Kuna yeyote anapata tatizo kama langu?

Natumia mtandao wa Tigo
Mbona mimi YouTube inafanya kazi... Weka bundle wewe
 
mi natumia VPN mkuu so sijaathirika
Kunandugu yangu huwa anafanya biashara za viatu mitandaoni,karudi kafura leo kaka mbona fb,whatsp,insta siwezi kuzifungua nikamwambia raisi wako kazifunga, ananiuliza sasa wateja wangu wanataka niwatumie waone mzigo itakuwaje ,nikamwambia kawaulize ccm unawashabikiaga Kila siku, kasema kesho simpi sasa Maguful kura kanikosesha zaidi ya laki 4 kisa uraisi wake.
 
Tusifanye makosa kesho, hatuwezi kuishi kama watumwa katika nchi huru, hii imevuka mipaka
 
Star TV nao wamekata matangazo yao na BBC Dira ya dunia baada ya Zuhura Yunus kutaka kuelezea madai ya habari inayozagaa kuhusu kuuawa kwa watu tisa Zanzibar. Mara paaap wamemla mtama hewani hayupo tunaangalia matangazo hapa

Wamemrudisha baada ya habari hiyo kuisha, wanaongelea kuhusu kuzima kwa mitandao
 
Back
Top Bottom