Siwezi kushindana na wewe bro, ni wewe na nguvu zako tu mkuu💪😅Nikiweka CV yangu hapa PM itafurika maombi😂💪🏿
Kipindi hicho hakuna mitandao ya kijamii.. Marafiki wanatafutana kwenye magazetiyaaani😀😀😀imebidi nianze kukumbuka visa vyangu daah
Hahahah!Siku hizi ukiwazingua wana namna yao🙌🏿🙌🏿🙌🏿🏃🏿View attachment 3648649
😀😀😀😀alafu fala mwenyewe umekaa pembeni daahKipindi hicho hakuna mitandao ya kijamii.. Marafiki wanatafutana kwenye magazeti
Siku moja nikasoma kwenye gazeti la KOMESHA mdada anatafuta mchumba.. Kaweka na namba za simu
Mimi nikamwendea hewani.. Ila sauti yake kidogo ikanipa mashaka ilikuwa nene halafu ya kibabe fulani hivi
Basi tukapanga tuonane CHAGA BITE Makumbusho bythen.. Yeye alikuwa anatokea mitaa ya Sinza makaburini
Basi Mimi nikafanya ujanja wa kufika mapema na kukaa meza ambayo inatazama barabarani kisha simu nikaweka vibration
Aisee kikaja kipisi cha mdada sura ya babuyake halafu bouncer fulani... Kavaa T-shirt nyekundu na pensi la kijani!
Kufika nje akapiga simu.. Sasa anapopigia simu na niliko ni kama mita 3 tuu.. Mimi sikuipokea baada ya kumuona alivyo😂
Nikamtumia msg kwamba nakaribia kisha nikazima simu..basi akaingia ndani na kukaa meza jirani na Mimi akaagiza viroba viwili vya konyagi bila soda kisha akaendelea kunipigia simu
Kuona sipatikani alimaindi vibaya mno.. Akampigia ndugu yake akamwambia huyu fala kanizimia simu ole wake siku moja nimjue..😂😂😂
Asilimia kubwa ni utapeli.
Asilimia chache Kuna ukweli
Unajua kufake nayo ni kazi kubwa.
Inakubidi ukumbuke Kila kitu ulichosema.
Wakati uliopita.
Na mtandao hauoneshi uhalisia
Wa mtu hususan kwenye Kimo,Rangi na Size. 😝
ephen_ una siri sana familia kumbe kuna mtu mnapendana mno ila unaringa😆😆Braza mshana nje ya madaa kaka yangu NISAMEHE kama takukosea, Kuna Hawa wa dada aizat, ephen na cocastic natamani nipate Mmoja kati Yao asee nawapenda sana lakini Iko hivi, aizat kanichunia, cocastic nilipewa mashaka kidogo, ephen huyu ni wangu kabisa na ananipenda NAMI NAMPENDA tunapendana in short, sana tena sana shida yake ana shobokea wanaume wengine mbele yangu natumia sana Kwa kweli ni kama anani dharririsha, ndugu yangu nisaidie jamani
Chagua mmoja uliyempenda kabisa kwa dhati ya moyo mengine niachieBraza mshana nje ya madaa kaka yangu NISAMEHE kama takukosea, Kuna Hawa wa dada aizat, ephen na cocastic natamani nipate Mmoja kati Yao asee nawapenda sana lakini Iko hivi, aizat kanichunia, cocastic nilipewa mashaka kidogo, ephen huyu ni wangu kabisa na ananipenda NAMI NAMPENDA tunapendana in short, sana tena sana shida yake ana shobokea wanaume wengine mbele yangu natumia sana Kwa kweli ni kama anani dharririsha, ndugu yangu nisaidie jamani
Zamani, watu wazima walikuwa wanakutana sokoni, kanisani, misikitini, au kupitia marafiki.
Lakini leo, kupata mwenza kumehamia kwenye mitandao kama Tinder, Badoo, DM za Instagram, na makundi ya WhatsApp.
Ukiwa mtu mzima mwenye majukumu yako, unatafuta mtu makini wa kutulia naye. Hata hivyo, ulimwengu huu wa mtandaoni una mitego mingi sana.
Hapa kuna changamoto chache ambazo wengi wanakutana nazo:
Profaili feki (Catfishing): Unazungumza na mtu picha yake inaonyesha ni mtanashati au mrembo, lakini mkikutana live ni mtu mwingine kabisa.
Matapeli wa mapenzi (Romance Scammers): Watu wanaojifanya wako siriaz, kumbe lengo lao ni kuomba mizinga ya hela baada ya wiki mbili tu.
Watafuta burudani ya muda mfupi:
Kupata mtu anayetaka uhusiano wa kudumu (ndoa/uchumba) ni ngumu; wengi wanatafuta michepuko au starehe za usiku mmoja.
Uongo wa umri na hadhi: Watu kudanganya kuhusu kazi zao, umri, au hata kama wameoa/kuolewa.
Hebu tushirikiane uzoefu wenu:
1.Je, umewahi kujaribu kutafuta mwenza mtandaoni ukiwa mtu mzima?
2.Ilikuwaje?
3.Ni mtego gani mkubwa zaidi uliowahi kukutana nao au kuusikia kwa rafiki yako?
Unafikiri ni mbinu gani bora ya kumtambua mtu muongo au tapeli kabla hamjakutana ana kwa ana?View attachment 3648487
Si ni ukweli lakini Coca😅😅😅😂😂😂😂
Una Mambo Wewe !! Hewa Gani Hapo Mbele Kuna Engine Utapata Joto 😂kiti cha mbele dirishani nipate hewa kabisa