Mitego ya Rais ya kununua Magoli iwakamate wajinga wa hili Taifa tu. Mimi siwezi kamatwa kamwe

Mama anapiga Kampeni za 2025, ile ni mitego kaweka Ulimbo ili akamate wajinga?
 
Hadi hapo mkuu bado tu haujaona hoja yangu? Napinga hilo suala la kugawa pesa iwe kwa simba na yanga au kwa kuwapa tu raia ni sawa na mtu kukupa samaki badala akupe nyavu ukavue mwenyewe.

Kama angekuwa mwenye kugawa hizo pesa ni raia wa kawaida tu anatoa pesa zake binafsi basi wala nisingeongea ila tunamzungumzia kiongozi mkuu wa nchi hapa, anachofanya ni kujinufaisha yeye kisiasa hana nia ya dhati kusaidia soka letu.

Halafu unavyosema akija Rais mwengine atajua afanye nini kuhusu michezo utadhani anachofanya Samia kununua magoli ya simba na yanga inasaidia michezo Bongo.
 
Huko kwa wahitaji mbalimbali peleka pendekezo kwa Waziri Ridhiwani Kikwete ndio mhusika mkuu, kwenye michezo kuna Mwana FA hawa ni mawaziri wawili wenye bajeti mbili tofauti.
Hata kwenye michezo kuna uhitaji pia kama yangefanyiwa kazi hayo mahitaji ingekuwa limefanyika jambo la msingi sana kuliko kununua magoli ya simba na yanga, hizi ni siasa kwenye michezo tu hazina msaada wowote kwenye soka la bongo.
 
Hata kwenye michezo kuna uhitaji pia kama yangefanyiwa kazi hayo mahitaji ingekuwa limefanyika jambo la msingi sana kuliko kununua magoli ya simba na yanga, hizi ni siasa kwenye michezo tu hazina msaada wowote kwenye soka la bongo.
CCM ni Chama cha siasa kina umri wa miaka 47 usishangae kwa wao kufikiria kufanya siasa kila unapotokea mwanya wa kufanya hivyo ndio lengo la kwanza la uwepo wao.

Motisha unafaa sana kuwafikia hao kina Yanga na Simba wameifikisha CCM hapa ilipofikia.

Na michezo imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 10 ya JPM na SSH, timu ya wanawake chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza imeshiriki michuano ya kombe la dunia, ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1961, mengi yanafanyika lakini hatukumbuki kuyaona kwani akili zetu ni za kukosoa tu, hazifikirii mema yanayofanyika huko kwenye michezo.
 
Kugawiwa pesa wavuvi wa samaki zipo sera nenda katika wizara ya mifugo na uvuvi uwe na mipango yenye kueleweka ya uvuvi uone kama wizara haitakuwezesha juu ya upatikanaji wa nyavu na mafunzo sahihi ya uvuvi.

Tatizo lako unaitwisha michezo lawama za sera za wizara nyingine ukisahau kuwa michezo na utamaduni ni wizara yenye mahitaji yake yanayojitegemea sawa na hizo wizara nyingine.

Una uhakika gani kuwa hana ni ya kusaidia michezo yetu wakati aliwapa Yanga ndege ya kwenda na kurudii kule Algeria mwaka juzi wakati walipokwenda kucheza na USM Algiers mechi ya fainali ya kombe la shirikisho?., Tatizo lako unalalamika wakati huna hata data za kisasa za kinachoendelea nchini mwako!.

Michezo ni tasnia pana sana zaidi ya haya magoli yanayonunuliwa kwa shilingi milioni tano kila moja.
 
Mkuu hapa tunajadili suala la Rais kugawa pesa simba na yanga kwa kununua magoli, sasa hayo ya kwamba tunakosoa tu hatufikirii mema sijui yanatoka wapi?
 
Mkuu hapa tunajadili suala la Rais kugawa pesa simba na yanga kwa kununua magoli, sasa hayo ya kwamba tunakosoa tu hatufikirii mema sijui yanatoka wapi?
JPM alikuwa anagawa pesa huko njiani misafara yake ikisimama na akaanza kuongea na raia na watu waliona poa tu Samia kaamua kuwapa motisha Yanga na Simba wanapocheza mechi za kimataifa.

Milioni tano kwa goli moja ni pesa kidogo sana kulinganisha na mabilioni yanayokusanywa kila siku na TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…