Kwa kweli ni ujinga wa hali ya juu kufurahia utapanyaji wa fedha kwenye starehe zisizo na tija wakati mambo muhimu kabisa, yanayohitaji sana pesa yashindwa kupata fedha.
Nina mfano unaoishi ambao sitausahau maishani, tuliwapeleka watu waliokuwa kwenye hali mbaya sana baada ya kupata ajali ya agari, na mmoja alifariki, lakini majeruhi wale baada ya kuwafikisha hospitali ya wilaya walikaa kwa masaa 7 bila ya huduma ya daktari kwa sababu hospitali nzima ina madaktari watatu tu walioajiriwa, na mmoja ni daktari mfawidhi, anashughulika zaidi na masuala ya utawala, mmoja yupo likizo, na aliyebakia azunguke wodini kuwahudumia wagonjwa wote. Tulipolalamika kwa huduma dhaifu, patron wa hospitali alitujibu kwa hasira kuwa, 'msitusumbue, hata mngekuwa ninyi msingeweza. Rais wenu anagawa hovyo pesa kwenye magoli lakini sisi hapa tumeandika barua za kuomba kuajiri madaktari na wauguzi mpaka tumechoka. Jibu kila mara ni kuwa Serikali haina pesa. LAKINI hela ya kununulia magoli na kusafiri na wasanii nje ya nchi ipo nyingi sana'. Tulipatwa na simanzi kubwa. Ikabidi tuliokuwepo pale hospitali tuchangishane pesa haraka ili majeruhi wale wakimbizwe hospitali ya rufaa. Maana tuliambiwa ambulance ipo ila hela ya mafuta hakuna, hela ya dereva na nurse hakuna.
Hapo ndipo ilipofikia nchi hii!! Mambo ya kijinga yanafanywa ni muhimu, na mambo ya muhimu yamepuuzwa kabisa. Inakera sana. Watawala wanatafuta sifa za kijinga kabisa!!