Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hebu rudia tena alichokisema!Tatiyo lipo kwa yale makanisa yanayojiita ni ni makubwa, nadhani mnayajua, viongozi wake ni wasomi wakubwa wa kila taaluma. Huu umati unaokimbilia kwa mwamposa unatoka huko. Hayo makanisa makubwa hayana mafundisho ya kutosha kuwaweka sawa waumini wao. Wanafundishwa mafundisho manyonge yaleyale kila mara. Umati mwingine unatoka kwa wale wengine wa 'uswahilini' ambao nao hawana mafundisho murua huko wanakoabudu shida zimewajaa na tumaini hawana. Wanakimbia porojo huko wanakosali na kukimbilia abrakadabra za kina mwamposa and so alike wanakoona watatatuliwa shida zao
Hizo nguvu na huo ushawishi vinaweza asili ya kutisha sana nyuma ya paziaMtu yeyote anayeweza kusanya watu namna hii ni mtu wa kuanza mwangalia kwa jicho jingine. Sidhani kama kuna mtu amewahi kusanya watu namna hii hapa nchini. Si
Idadi ya watu waliokosa ufahamu imeongezeka sana....Mtu yeyote anayeweza kusanya watu namna hii ni mtu wa kuanza mwangalia kwa jicho jingine. Sidhani kama kuna mtu amewahi kusanya watu namna hii hapa nchini. Sikumbuki
Either ways tukubali the man ana ushawishi mkubwa na Serikali imeliona na itajadili hilo. Si dogo.Hizo nguvu na huo ushawishi vinaweza asili ya kutisha sana nyuma ya pazia
Possibly ila je nani mwingine anaweza kukusanya watu waliokosa ufahamu kiasi hiki?Idadi ya watu waliokosa ufahamu imeongezeka sana....
kwa sasa hakuna....ndio maana sirkali yajisogezamoPossibly ila je nani mwingine anaweza kukusanya watu waliokosa ufahamu kiasi hiki?
Hapa umeyasingizia tu hayo makanisa. Shida kubwa iliyopo ni Umasikini, maradhi na ujinga. Hivi vitatu vinawatesa wananchi walio wengi nchini mwetu zaidi ya miaka 60 sasa tangu tulipopata Uhuru! Na ndiyo maana wanatafuta namna ya kuondokana na hayo matatizo kupitia njia mbalimbali, zikiwemo hizi za wajasiriamali wapya wa miujiza.Tatizo lipo kwa yale makanisa yanayojiita ni ni makubwa, nadhani mnayajua, viongozi wake ni wasomi wakubwa wa kila taaluma. Huu umati unaokimbilia kwa mwamposa unatoka huko. Hayo makanisa makubwa hayana mafundisho ya kutosha kuwaweka sawa waumini wao. Wanafundishwa mafundisho manyonge yaleyale kila mara. Umati mwingine unatoka kwa wale wengine wa 'uswahilini' ambao nao hawana mafundisho murua huko wanakoabudu shida zimewajaa na tumaini hawana. Wanakimbia porojo huko wanakosali na kukimbilia abrakadabra za kina mwamposa and so alike wanakoona watatatuliwa shida zao
Cha ajabu hapo jirani yake kuna sehemu wanakaa mateja,wakabaji wanalala hapoNa haziko monitored
Jana nilikuwa Kawe kwenye Mkesha 😀😀Kwenye huu uzi mbona sioni wale watu waliowahi kuhudhuria mkutano wa Mwamposa au ameshawaloga wasione nyuzi kama hizi hapa JF. Akina johnthebaptist, Yesu Anakuja, Yesu anarudi, Yesualiniitanjoo, Yesunipendo, pamoja na molanehemia wanaona giza wakifika kwenye huu uzi.
Ukweli mtupuHapa umeyasingizia tu hayo makanisa. Shida kubwa iliyopo ni Umasikini, maradhi na ujinga. Hivi vitatu vinawatesa wananchi walio wengi nchini mwetu zaidi ya miaka 60 sasa tangu tulipopata Uhuru! Na ndiyo maana wanatafuta namna ya kuondokana na hayo matatizo kupitia njia mbalimbali, zikiwemo hizi za wajasiriamali wapya wa miujiza.
Na siku zote hawa wajasiriamali wa miujiza wamekuwa wakiwaahidi watu wajinga kuwapa utajiri, kuwaponya magonjwa sugu na yasiyo na tiba, pamoja na shida zao lukuki zinazowakabili kwa kutumia miujiza!! Jambo lisilowezekana hata kidogo.
Na serikali kwa sababu inatambua fika imeshindwa kutimiza jukumu lake la msingi kwa vitendo (la kuwatoa wananchi kwenye ujinga kwa kuwapatia elimu bora na yenye manufaa kwao, kwa kushindwa kuboresha huduma za afya na kushindwa kuwakwamua kiuchumi na hivyo kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini wa kipato), imeamua kwa makusudi kabisa kushirikiana nao.
Agano jipya limeanzia wapi na litaishia wapi?Bro; sio mitume na Manabii wa kweli, ni matapeli wa kweli na waongo! Kwenye agano jipya hatuna nabii Kama office
Wacha mafala watapeliwe!
Hawa hawana tofauti na waganga wa kienyeji, mtaji wao mkubwa ni umaskini na ujinga wa wafuasi wao, huwashibisha matumaini hewa na kuwalewesha kisha kuwaibiaKama kuna watu whuni, wanyama katili na wenye rohombaya sana basi hawa ndugu wanaongoza.
Wao wanachojua ni mashindano yq kukusanya pesa tuu na kuzitumia kwenye mambo binafsi ya kifahari na kufuru ya pesa.
Wanashindana kuvaa mavazi ya bei ghali
Wanashindana kumiliki magari ya kifahari na ya gharama kubwa.
Wanashindana kuwa na mijumba ya kifahari na kila aina ya kitu cha gharama kubwa na cha thamani unachojua wewe. Mtaji wao mkubwa ni waumini na naamini fukara hohehahe wanaowaamini sana!
Kwenye makanisa yao hakuna huduma inatolewa bure.. Hata ile nakala ya fomu ya shilingi 50 au mia ya kuandika shida yako inauzwa si chini ya elfu 50... Na kila fomu ina viwango vya gharama kwa kila huduma utakayo.
Wanaotoa dau kubwa ndio hupewa kipaumbele cha kuonana na mtumishi.. Na mapato yao hayo hayatozwi kodi yoyote ya serikali. Huwezi hata siku moja ukute
Wametoa sehemu ya mapato yao kuhudumia yatima na wajane wasiojiweza.
Huwezi hata siku moja kuwakuta wakijenga vituo vya afya kuwahudumia wasio na uwezo.
Huwezi hata siku moja kuwakuta wakijenga shule na vituo vya huduma za kielimu kama msaada kwa wasiojiweza
Huwezi hata siku moja wakiwa na programu mbalimbali za Kusaidia makundi mbalimbali kwenye Jamii kama wafanyavyo kina Malisa G.J na Lions clubs kwenye nyanja za elimu, makazi, lishe, tiba na matukio ya kibinadamu ya dharura.
Ni wepesi mno wa kufarakanisha na kugombanisha familia, wanandoa, ndugu na jamaa.. Hasa kwa wale wasiopenda mambo yao na kuharibu kuwaelimisha waliokwisha tekwa!
Kukupa tuhuma za uchawi, uongo uzinzi nk kwa wenza wa wengine wao ni fasta sana.. Wameharibu ndoa nyingi na kufarakanisha ndugu wengi sana!
Hawa si watumishi wa kweli maana hawahubiri upendo, amani na mshikamano kwa vitendo
Hawa ni watu wa makafara ya kutisha,ibada za siri, washirikina wakubwa!
Ni wachafu na ni walafi wanaofanya mambo machafu na mabaya kizani..
Kuwanyesha waumini wao vitu vichafu kwao ni kawaida kabisa.
Maji yaliyochanganywa na maji yaliyooshea maiti;
Maji yaliyochanganywa na manii au uchafu uliotoka ukeni;
Maji yaliyooshea miguu au mikono ya nabii au mtume nknk
Ni wezi wakubwa!
Udongo uliochimbwa na scavator na kuusafirisha kwa roli kisha kuwauzia Watu kijiko shilingi elfu moja.. Huu ni zaidi ya wizi na utapeli wa kiwango kikubwa sana
Kuna mafuta ya upako, sabuni za upako, leso za upako.. Nknk vyote hivyo ni biashara kubwa isiyochajiwa kodi yoyote na serikali
Naendelea…
Agano jipya limeanzia wapi na litaishia wapi?
Paul alikuwa kwenye agano la kale?
Huduma ya kitume ipo mpaka sasa ila mostly wa hawa wanaoitwa mitume ni aidha folse or fake.
Fake ni wanaotumia ujanja ujanja while false ni hawa wenye cult spirits, wanaponya, wanaona na kufanya miujiza mingi lakini si kwa roho ya Mungu.
Wenye huduma ya kitume wapo wengi tu mpaka leo ila hawajijui hivyo huishia kujipa title nyepesi like mchungaji, mwinjilisti.
Suala la fake and false Ministers liko makanisani kwa ofisi zote ila tu jamii huwakomalia mitume na manabii.
5% tu tu ya watumishi wa leo walioitwa na Mungu wengi wameitwa na njaa