Mitume na manabii wa kileo ni viumbe waliojaa, ghiliba, uroho ubinafsi na uchoyo uliopitiliza

Kumbe watenda kazi hawalipwi
 
Asante mwamposa umetujengea hospital kubwa kyela(mbeya) hospital kubwa kuliko ya rufaa ya mkoa...

Huduma nzuri, umetuletea madaktar bingwa wazungu..mwisho mdogo wangu asiependa biashara umemwajiri kwenye hospital Yako..ubarikiwe sana.

Nimeona huo mkesha wa leo,,kwa makadirio sadaka za leo utatujengea hospital nyingine Tano pale mbeya..usijali wazaramo kulalamika ndio desturi Yao na roho za wivu, sisi tunaona uwekezaji pale mbeya!!
 
Mambo yamechanganyikana, waganga wa kienyeji kujifanya ni watauwa wa Mungu na waumini kuwafanya wachungaji kama waganga wa kienyeji, wamelikoroga walinywe
Hili ni dongo la direct sasa
 
Hao wafuasi by nature ni wafuasi
Wasipofuasi kwenye kanisa watafuasi kwenye siasa, mpira, muziki nk. Hao wapo kila kundi ili kuwapa watu utajiri.
Imagine miaka tangu uhuru kuna vyama vina wafuasi wakati havijawahi kuwaletea unafuu wa maisha.
Ki uhalisia kila mtu anatakiwa awe mfuasi wa yeye mwenyewe.
 
Halafu wamama hao hao hizo pesa wanazichuna kutoka kwa wanaume na kisha wanawapelekea Manabii uchwara.
Wanaume siku tukiamka na kuacha ujinga wa kuwapa pesa ovyo wanawake nakuhakikishia huenda 80% ya manabii uchwara wanayeyuka.
Wengine wana pesa zao, nyingi tu, na wengine wanatumwa kabisa na kina baba nenda ulete maji na mafuta, ni ngumu manabii kuyeyuka Mkuu.
 
Wajinga ndo waliwao! Na kuwakomboa kwenye hilo jinamizi inahitaji elimu kubwa, na sanasana nguvu za kimamlaka za kiselikari laasivyo tumekwisha.
Mimi acha tu niitupie lawama serikali maana matapeli wengine inawashughulikia lakini hawa waliojificha kwenye kichaka cha dini wanawaacha watapeli kwa raha zao mchana kweupe. Sielewi hata kidogo. This is not justice. Tapeli ni tapeli tu wote washughulikiwe.
 
Mimi sielewi kwa nini serikali yetu haikomeshi huu utapeli. Au mtu akitapeli kwa jina la dini ni poa tu?? Sielewi!!
 
Wivu,wivu mama wivu.
 
Ndio najiuliza serikali yetu hailioni hili kama ni janga la taifa??
 
Kwahiyo wewe shida yako kuu ni kuwa hawakatwi kodi?peleka ombi serikalini waanze kuwakata kodi ili roho yako ifurahi.
 
Nakazia hapa. Umenena ukweli mtupu.

Kiukweli matendo yao yanatia shaka. Hivi huwa wanawafanya nini wafuasi wao hadi hawashutukii huu mchezo wao. Ata ukikutana na mfuasi wa hao mitume/manabii ukamshauri anakuona kama pepo.
Tatizo ni afya ya akili. Hili ni janga la kitaifa. Mtu mwenye akili iliyo timamu hawezi kufuata huu upumbavu wa mitume na manabii.
 
Wanajifanya wanawaonea huruma wakati mtaani kwao hata kutoa msaada kwa wenye njaa na dhiki hawajawahi kufanya,ila likija suala la manabii na mitume mishipa inawatoka,mi nawaona ni wapumbafu na wanafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…