Ukiwa huna uhakika na unachoandika ni BORA KUTOANZISHA UZI....
kwenye Uislam ukisikia anatajwa Mola Mlezi utasikia kwa mfano Allah Subhanah Wataala, akitajwa Mtume utasikia Rehema na Amani ziwe juu yake, wakitajwa mitume wote waliobakia aliwemo mtume wa Allah Issah utakisikia Alayh Salam, wakitajwa maswahaba utasikia Radhiallah Anhu, Waja wema waliotangulia Rahmahullah au waliopo HAI utasikia hafidhallah
Kwa hiyo siyo kweli UNACHOKISEMA KUWA KWENYE UISLAM MTUME ANAOMBEWA MSAMAHA.....
MOLA MLEZI ameweka utaratibu wa kumtukuza YEYE kila anapotajwa au unapotaja jina la Mola Mlezi, kuwatakia salama na amani Waja wema waliotangulia kwa maana waliishi na kumridhisha YEYE na YEYE amewaridhia na wanaombewa mpaka na malaika...
KINYUME CHAKE kwa kila aliyeishi kwa UJABARI NA KUMUASI MOLA MLEZI KAMA FIRAUNI na wote wanaomfuatia basi utasikia yakitamkwa MKASIRIKO YA MOLA MLEZI NA KUWEKWA MBALI NA REHEMA ZAKE baada ya majina yao!!!!
Kwa aliye hai ataombewa UONGOFU ila akifa mwanadamu kati uasi basi hadi Malaika watamwombea Makasiriko ya Mola Mlezi....
HUJAWAHI ONA MTU ANAFARIKI NA WATU WANAFURAHI KUWA WATAPUMZIKA KUTOKANA NA MAUDHI AU DHULMA ZAKE???? Au MWINGINE ANAFARIKI KILA YUALIA KUTOKANA NA WEMA WAKE KWA WATU???
Basi jua vivyo hivyo kwa wanadamu na Mailaka kumwombea aliyefariki au hata aliye HAI...