Mitume walikuwa wanaomba kuombewa na wafuasi kipindi wanafanya huduma. Kwanini mwingine anaombewa hata baada ya kufa?

Mnamtakia Aman mfu marehemu?

Hizo kumtakia Aman zinamsaidia nn?

Kama alikufa katika dhambi ,asubiri Moto wa jehanum
Kwenye Uislamu wema hauishi hata mtu akifa , kama alisomesha watu utanufaika mpaka wale watu waishe wote, huku ni rahaa tupuu, Mtume Mohamadi kafundisha watu tutamtakia imani mpaka waislamu wote waishe
 
Maswali yangu umeyaona? narudia hili moja labda unaweza elewa , kwanini Mungu aliendelea kumbariki Yakobo pamoja na kutumia njia za uongo? inakuwaje ubatili ulete jambo jema? aya jibu
 
Dhehebu pekee linalo kiri kuwa Allah hana mshirika , hakuzaa wala hakuzaliwa, Mohamadi ni mtume wa Mungu na Issa bin Maryamu ni nabii tu wala sio Mungu, hili ndio dhehebu la kufata, swali jingine?
Litaje Hilo dhehebu katika Shia ,Sunni na hayo mengine 70+
 
Kwenye Uislamu wema hauishi hata mtu akifa , kama alisomesha watu utanufaika mpaka wale watu waishe wote, huku ni rahaa tupuu, Mtume Mohamadi kafundisha watu tutamtakia imani mpaka waislamu wote waishe
Huo wema unamsaidia nn ikiwa hakutubu?

Anapata nn marehemu ?
 
Hakika mkuu, huu ni ukweli unaodumu milele. Imeandikwa mtu anakufa mara moja na baada ya hapo ni hukumu.
Kuna wale wanakufa halafu wanafufuliwa na akina gwajima na bushiri, wale siku wanakufa mara ngapi?
Au wao hili andiko haliwahusu?
 
Litaje Hilo dhehebu katika Shia ,Sunni na hayo mengine 70+
Wote hao wanakubali kuwa Allah hana mshirika hakuzaa wala hakuzaliwa, Mohamadi ni nabii wa Mungu, Isa bin maryamu ni nabii sio Mungu, hivyo yote hayo yako sawa , swali jingine?
 
Unamsaidia sana maana tunaendelea kufundisha na kumuombea dua, hivyo thawabu tunazo pata na yeye anapata
ACHA kudanganywa ukifa hujatubu na kuungama ,imeisha hiyo

Yaan ufanye upuuz duniani utegemee ukifa uombewe Aman na rehema ? Yaan uende mbinguni kwa lift?

Haya mafundisho Ni ya mashetan ,muasisi Ni Roman Catholic , wao wanaita purgatory

NDIO maana ukichunguza kwa jicho la 3

Utagundua Uislamu ULIANZISHWA na Roman Catholic
 
Wote hao wanakubali kuwa Allah hana mshirika hakuzaa wala hakuzaliwa, Mohamadi ni nabii wa Mungu, Isa bin maryamu ni nabii sio Mungu, hivyo yote hayo yako sawa , swali jingine?
Kama wanakubaliana kipi kinachowafanya watofautiane ?

Na hiyo uliyotaja sio mising ya uislamu

Hizo Ni sababu zako binafs
 
Maswali yangu umeyaona? narudia hili moja labda unaweza elewa , kwanini Mungu aliendelea kumbariki Yakobo pamoja na kutumia njia za uongo? inakuwaje ubatili ulete jambo jema? aya jibu
Haki ya mzaliwa wa kwanza aliipata kihalali hivyo ndio maana akapata na baraka zake.
 
Yasio kuhusu achana nayo broo we elewa ivyo ivyo na sisi acha tumuombee huyo wetu kwani we unaumia
 
Kama wanakubaliana kipi kinachowafanya watofautiane ?

Na hiyo uliyotaja sio mising ya uislamu

Hizo Ni sababu zako binafs
1. Wote wanakubali kuwa Allah ni Mungu
2.wote wanakubali mohamadi ni nabii
3.wote wanakubali kuwa Isa bin Maryamu ni nabii sio Mungu
Hayo mengine yote sio tatizo kutofautiana, sasa watu wanatofautiana kwenye mwezi muandamo hivi ni vitu vidogo ambavyo haviwezi mtoa mtu katika Uislam
 
Kuna wale wanakufa halafu wanafufuliwa na akina gwajima na bushiri, wale siku wanakufa mara ngapi?
Au wao hili andiko haliwahusu?
Sina uhakika na hao unaowataja kwasababu sijafuatilia kwa karibu kujua details zao.

Ila mtumishi yoyote wa kweli wa Mungu anaweza kumuombea aliyekufa ili afufuke ikiwa ndio mapenzi ya Mungu hasa ikiwa huyo mtu hajakamilisha kusudi lake na shetani amehusika kukatisha maisha yake.
 
Swadakta kabsa
 
Maombezi sio jambo la kukurupuka, ni matokeo ya kazi nzuri uliofanya duniani, kama mtoto dini ulikuwa unaacha kumuelekeza sasa atakuombea vip dua? ukiona watu wanaomba dua ujue ni matokeo ya kazi nzuri za hao watu walipokuwa duniani, kama mimi namuombea sheikh wangu kwa kunipa elimu hii murua kabisa, ukiona vyaelea vimeundwa
 
Haki ya mzaliwa wa kwanza aliipata kihalali hivyo ndio maana akapata na baraka zake.
Uhalali uko wapi kijana wakati mtoa baraka kadanganywa ? au hujui mzee Isiaka alilalamika kudanganywa, yaani wewe haki iwe yako halafu utumie uongo kuipata uko serious kweli!!!
 
Uhalali uko wapi kijana wakati mtoa baraka kadanganywa ? au hujui mzee Isiaka alilalamika kudanganywa, yaani wewe haki iwe yako halafu utumie uongo kuipata uko serious kweli!!!
Kijana baraka inatoka kwa Mungu, Isaka alikuwa channel tu ya kupitishia ndio maana hakuwa na namna ya kumbariki Esau baada ya Yakobo kuchukua nafasi. Isaka hakulalamika popote, alishangaa tu na nadhani hakuwa na taarifa kwamba Esau alishauza haki yake.
 
Baraka inatoka kwa Mungu kupitia baba mzazi, sasa baba mzazi tayari alishadanganywa na akatoa baraka kwa kudanganywa, maana yake process nzima imejaa ubatili na baraka zimejaa ubatili, vip Mungu atie mkono wake kwenye ubatili wa namna hii?
 
Uduni wa wachangiaji ni ishara kuwa mleta mada umefeli kwenye lengo lako.......watu wamekausha tu wanaendelea na mambo mengine. Kajipange tena!
Rudi hapa kwenye komenti yako. Watu wamechoka kuombea wafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…