Mixx by Yas jina la kihuni sana badala ya Tigo Pesa

Ndio athari za kuingia kwenye kikao ukiwa umelewa. Huyu boss aliyependekeza hii mixx by yas alikua tungi na kama unavyojua wafanyakazi wake kuhofia kibarua chao wakashindwa kukosoa zaidi ya kupiga makofi.
 
Hizi kampuni wakitaka kufanya jambo lao wanafanya lolote wamejiunga na kampuni kutoka South Korea ili mradi wakwepe kodi tu hakuna kingine...
Hao ni Wakwepa kodi wakubwa Tanzania kisheria kwa kuangalia mapungufu ya Income Tax yetu harafu utasikia Waziri anaongeza kodi sehemu kwa kuwakandamiza Watanzania huku wakiwaachia hawa majambazi wakiichezea Tanzania.
 
Sasa sisi watu wazima mnatukosea heshima maana hiyo sio lugha yetu.
Mkuu hawa walianza kitambo, hilo jina tIGO lenyewe wengi hatukujua kama ni back door, wakaja na cha asubuhi wakapigiwa kelele mpaka bungeni hawakusikia. Ila ninajifunza kuwa huu mtandao unawafaa vijana tena wakihunikihuni, watu wazima tunatakiwa kutafuta mtandao mbadala wenye heshima zake
 
Mkuu hapa Rostam kaboronga, basi angalau angesema 'Yaspesa au mix pesa'
 
Mkuu hapa Rostam kaboronga, basi angalau angesema 'Yaspesa au mix pesa' !!!
Toba!!!
 
Hakuna mtu kaipokea vyema hili jina.

Walibadili tu.
Bado Lina maana ile ile. Kwa sasa ndio wamekinukisha zaidi.
Kama career corp inavyoitwa kariakoo, hii ya sasa mixx by Yas itasomeka “miks my As”… “changanya makalio”- bado ni uloda wa Tigo huo huo. Au labda ni ili waaendane na ile kauli “ sex sells”…ktk biashara. Ubunifu hafifu.
 
Mixx by yas hii imekaa kihuni sana kwa kweli
 
Sijawahi kuona jina baya la kampuni kama YAS, sijawahi kuona mtandao wa miamala ya kifedha hauna neno (au kiambata chochote) linalohusiana na fedha, kwa Tanzania MIXX BY YAS ndio wa kwanza.

Zaidi ya Lisaa sasa, sio menu (mssd)huduma hakuna. Huu mtandao unauswahili sana.
 
Jina baya!
 
Pale tiGo watoto wengi pia ni wajinga wajinga tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…