Mizengo Pinda: Tuanze mchakato wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi
Kwenye tume huru msiwaweke majaji wastaafu, wengi hawana hekima. Mtu akistaafu halafu mumpe nafasi ya kutumikia jamii anakuwa kama alisahau kitu. Tunaona mahakimu wastaafu kwenye mahakamani za nyumba, ona yule wa tume ya uchaguzi, ona msajili wa vyama, ona mnaowapa kusimamia bodi mbalimbali, yanayofanyika huko na wastaafu, Mungu tu ndie ajuae.
 
Nawasalimu.

Nimeshangazwa sana kusikia MZEE wetu Pinda WAZIRI MKUU Mstaafu kwa Taaluma ni Mwanasheria Akizungumziaa TUME Huru kabla ya KATIBA MPYA.

Pamoja na kuwa sio Mwanasheria lakini najua kuwa TUME HURU ili iiundwe Lazima KATIBA ITANGULIE hivyo niliamini Mzee Wetu Mzee Pinda Angeshauri TUUNDE KATIBA MPYA KISHA TUME HURU YA UCHAGUZI kwa sababu kwenye KATIBA LIYOPO SHERIA ya Uchaguzi inasema MATOKEO ya URAIS Yakiisha Kutangazwa na TUME ya Uchaguzi HAYAHOJIWI POPOTE.

Vifungu kama hivi ndivyo HAVITAKIWI kwenye KATIBA MPYA

WATANZANIA Tunataka KATIBA MPYA KWANZA.
 
Wakishakuwa nje ya madaraka akili huwa zinarudi.
Kuna mtaalamu alisema"watawala wa kiafrica huwa na akili baada ya kustaafu"
 
Kwanza sikuamini kama PINDA alisema huu ivi,yaani sikuamini kama waziir mkuu mstaafu amesena ni wakati wa kupata Tume huru ya uchaguzi,niliposikia nmeamimi usalama wa Taifa wameamua kabisa
.Samia jiongeze ulio nao wameamua tayar pinda no yake ni sinior in security system hata kikwete alimteua paspo kujua kuwa I nyoka.
 
Huwajui CCM wewe... utameza ndoano halafu muanze kuwalilia wahisani... Huyu unayemtaja ushasema ni jasusi tena from CCM...mpaka anasema hayo ujue washajipanga washaset mpango kazi wanawasuburi kwenye kona mjae..
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi" Mzee Mizengo Pinda

View attachment 2047118

Hii inatoka moyoni akimaanisha tume huru kweli kweli?! Au ni chezo CCM wanataka kutufanya mazuzu tuingie kwenye 18?

Tumeshuhudia mahakama ikijidhirisha kutokuwa huru, tumeona tume huru ya Jecha wa Jecha ilichofanya kule Zanzibar.

Tumuunge mkono Pinda kwa tahadhari kubwa sana, atazamwe kwa jicho la tatu.
Tunataka Tume huru itakayo letwa na katiba mpya sio tume huru ya michongo.
 
"Kuna mambo ambayo sisi CCM kama chama tawala lazima tubebe dhima. Tutoe uongozi. Kwa, mfano hili la Tume Huru ya Uchaguzi kizuizi ni nini? Hili ni jambo ambalo lazima tukubaliane na wenzetu wa upinzani na tuanze mchakato wa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi" Mzee Mizengo Pinda

View attachment 2047118

Hii inatoka moyoni akimaanisha tume huru kweli kweli?! Au ni chezo CCM wanataka kutufanya mazuzu tuingie kwenye 18?

Tumeshuhudia mahakama ikijidhirisha kutokuwa huru, tumeona tume huru ya Jecha wa Jecha ilichofanya kule Zanzibar.

Tumuunge mkono Pinda kwa tahadhari kubwa sana, atazamwe kwa jicho la tatu.
Tume ya Je,,,, ilikuwa ya maigizo (the comedy)
 
KWANI ILI TUME IWE HURU INABIDIIWEJE?
 
KATIBA MPYA NA TUME HURU NI MAPACHA ILI IWE TUME HURU LAZIMA UFUMUE KATIBA, kwa vile itagusa kipengele cha uteuzi, madaraka ya Rais kuhusiana na Tume hiyo, uwajibikaji, aina ya wajumbe mfumo wa uongozi na usimamizi kuanzia juu hadi chini,kutoingiliwa na vyombo vingine,matokeo ya uchaguzi kupingwa mahakamani na viwango vilivyowekwa vya uendeshaji na masuala ya fedha. Mengi ili yakae sawa lazima ku overhaul Katiba, mimi ninashauri kwa kuanzia tupigie kura kaitba ya SITA tuanzie hapo
 
Uliyoyaandika ni sahihi kabisa Izingatiwe kuwa katiba mpya haitapatkana kwa maneno matupu.

Kutambua tunachokitaka kama agenda ya kudumu dhidi ya marafiki na maadui ya kudumu hakuwezi kupuuzwa.

NInakazia:

Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu
 
Hakuna kitu kinakera kama mtu kutoa maoni lkn kwanza akauliza mtawala anapenda upande upi, akishajua hivyo basi na yeye maoni yake yataangukia hukohuko.
 
Back
Top Bottom