Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 5,988
- 6,226
X-trail kama hulijui kaa kimya
Punguza jazba umeleta uzi tarajia maswali hii ndio JF,,JIANDAE NA WENGINE NA MASWALI YAO WW UNAULIZA NA WAO WANAKUULIZA..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
X-trail kama hulijui kaa kimya
Xtrail ni majanga linakupa umaskini ujanani
xtrail ni kujipa mawazo tu. body plastic, engine aluminium ikizingua kidogo unalisahau juu ya mawe
Likamfie huko!ama kweli sitakaa kamwe kununua gari kwa mtu, ngozi nyeusi tuna laana yani unamuuzi rafiki yako kimeo
Passo, vitz, swift na duet ni ushuzi mtupu hazifai kusafiria safari ndefu
Subaru nying ni full time 4wd,issue ya kijiji huna hofu,mafuta 10km/L city kwa highway 12km hapa nazungumzia cc2000, kwa vipuli Shock up,bush,body,pump,plugg vyote bei ya kaiwada,
Jaribu forrester 2005 xt au cross sport ukishindwa hata impreza siyo mbaya maana engine za subaru structure ni moja.Zina tofautiana vitu vidogo kama cc,turbo, drive type
Sio kweli.
CHA KWANZA KABISA UMJUE FUNDI ANAEJUA KUTENGENEZA NISSAN XTRAIL NA SIO TAPELI. FUNDI MWENYE UJUZI NA MUELEWA NA SIO MWENYE TAMAA!
Mimi fundi wangu miaka yote ni fundi mmoja anaitwa Deo yuko pale Mwenge alifundishwa na Nissan Wenyewe, yuko karibu na Maryland Bar opposite ITV.
Gari la kwangu nilinunua 2013 na mpaka leo ninalo na nimetembea nalo mikoa mingi sana nchi hii. Tayari tangu nimenunua nimetembea Kilometre 134,000 (nilizotumia mimi) Hili hapa:
View attachment 260838
Nimetumia magari mengi tangu ninunue gari la kwanza 1998. Nissan X-Trail haijawahi kuni-disapoint hata siku moja! Ni gari durable na comfortable hata ukiwa off road na stable barabarani sana. Nissan X-Trail spare zake ni ghali kidogo na sio kiasi kikubwa kama watu wanavyosema, ila bush, na stabiliser links ambazo ndio unabadilisha zaidi kama ni mtu wa pori kama mimi ukifunga ni mwaka. Spare zake karibu zote ni original. Vitu vikubwa vinavyokufaga na ni mara moja kwa mwaka ni sensors ambazo magari mengi ya siku hizi yanazo, usipoibadili ukaipuuzia basi unaweza kuharibu gari, gari ikaheat au tatizo lingine. Sensor moja inaweza kuwa laki mbili, ila sensor kama ya air filter mara nyingine huhitaji kusafishwa tu na spray maalum.
Muhimu usipitilize service milage, hakikisha unaweka collant na sio maji yako ya Dawasco, engene yake ni high efficient na moderm na ukiona tatizo lolote lile, peleka kwenye computer wa diagnose full stop. Iwe ni miss au engene ina mngurumo wa ajabu. Taa yoyote isiyo ya kawaida ikiwaka kwenye dashboard ni Computer tu ndio itakwambia.
Ujinga wa sisi Waafrika wengi tunataka gari ambalo hata usipofanya servie litakwenda tu na fundi yoyote ukimpa atategeneza. Ukimsikia fundi anakwambia hizi gari mbaya sana kama wanavyosema siku hizi gari za VVTI au D4 ujue huyo mbulula hana shule na hajui kulitengeneza. na ukimwachia atakuharibia gari.
Nissan X-trail haikuwahi kukwama katika tope, sio chini ya mara moja nimeziacha Rav 4, Suzuki Escudor na Hiluz Double cabin porini mimi nikapasua katika tope, vumbi na vichaka na sikupata shida yoyote. Pia clearance yake chini ni nzuri na sio rahisi kugonga.
Zingatia service yake, na ukifunga spare ni mkataba mwaka sio kama Toyota spare bei rahisi lakini utabibadili tu mara kwa mara na hutakumbuka mwisho wa mwaka umeingia gharama kiasi gani.
Kwa ealuation zaidi soma hapa: https://www.youtube.com/watch?v=GR7kHC6yiQI
wadau nataka kununua Pajero ios, naomba wenye uzoefu na hii gari wanipe mazuri na mapungufu yake kwani mimi kwanye tasinia hii ya magari ni mtupu kabisa
Forester X20, 2002-2004 Mimi ninayo KM 5 kwa lita, taa kubwa ya mbele 600,000 shock up si chini ya laki 550,000