Kwa ujumla tuachane na mawazo mgando,magari ya sasa yanahitaji kutengenezwa kwa akili zaidi kuliko kufungua. Kwa maana hii ndio maana dash board za magari huwa yana viashiria vingi, ukiona kiashiria kimojawapo na kama hukijui kapime gari upate jibu sahihi kuliko kufungua fungua mwisho wake utalalamika kuwa magari ni mabovu. Na hili sio xtrail pekee hata toyota za sasa hivi pia zinahitaji matunzo ya namna hii. Ukifuata utaratibu huu utasahau mafundi wa kubahatisha. Mimi natumia toyota ya mwaka 2004 nilipata matatizo kwenye gari fundi mmoja akaniambie ninunue injini mwingine akasema tubadilishe accelerator ila baada ya diagnosis shida ilikwisha kwa just simple reset ya mfumo wa gari, na mpaka leo nasafiri nayo kwa zaidi km 1000 kwa siku bila usumbufu wowote.
Kwa ujumla tuache mafundi wa kubahatisha kwani ndio chanzo cha uharibifu wa magari. Wanaosema toyota spea zake ni nafuu wajaribu ku browse kwenye internet waone bei halisi za vipuri,ndio watajua kwanini kila siku huwa wanarudi kwa mafundi kufunga spea mpya