Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Kwa mfano watu mnasifu ra4 ila rav4 ya 2002 mpaka 2004 zina shida ya gear box especially zikifika km 100,000. Kama unanunua gari bila tathmini ili mradi ni toyota kanunue model hiyo uone. Nina watu wamenunua model hiyo cha moto wamekiona ,baada ya kyfanya research wakagundua ni production failure na hii iligunduliwa na toyota marekani waka recall magari ya model hiyo na kuongeza extension of warranty. Ila humu watu hamsemi mnangangania nissan xtrail
 
Msichukue mkopo mkanunua x....mimba narudia tena ntarudi badaee
 
Hapana Bodi sio plastic ni fibre! Ni tofauti kubwa. Unajua kwanini wametengeneza vile? Technolojia hii ni kumlinda mtembea kwa miguu, mtu akigonwa na gari hili kama impact sio kubwa sana hawezi kuumia kwani bodi hubonya na kurudi kawaida. Pili bodi hili ukikwaruzwa au kugonwa kidogo au kuguswa bahati mbaya hubonya na kurudi akama kawaida hivyo kupunguza gharama za kunyoosha na matengenezo yasio ya lazima. Kama zilivyo bampa za magari yote yanayotoka sasa hivi ni ya Fibre na ukigonga au kugongwa nyuma au wewe ukigonga kama sio gari kubwa sana au impact sio kubwa unaweza usijue kama kuna kilichotokea.

Sijaelewa vizuri ni fibre ya namna gani iliyoko kwenye xtrail. Maana mie najua Carbon fibre, ni a very strong material but very light as well. Inatumika saana kutengenezea super cars, the like of the Ferrari, Pagan Zondas, Lambo etc. Ila production yake ni very expensive, sidhani kama ingewekwa kwenye Nissan Xtrail wabongo wa kawaida tungeweza ku afford.
 
kuna vitu kweli watu wanaongelea ushabiki kwa mfano mimi binafsi kila ni kiwa safarini nikikuta breakdown ya scannia basi inakuwa ni 124 si jui kuna shida gani na hili toleo.
 
Ushauri:
1. Gari kama limekushinda wewe usikimbilie kupotosha kuwa gari fulani ni baya au halifai

2. Unapofanya service tumia oil zenye kiwango kinachokubalika kama oil za castrol/BP

3. Usipende cheap spares

4. Gari ikipata tatizo tumia nyenzo za kufanya diagnosis/kama huna tafuta gereji ambayo wanafanya diagnosis na yenye mafundi wenye uwezo wa kutumia taarifa za hiyo diagnosis

5. Usipeleke kwa fundi anayefanya matengenezo kwa kubahatisha. Hata tatizo linalohitaji kubadili sensor au fuse linaloweza kuisha kwa dakika 5 au 10 yeye anakimbilia kufungua egine au gear box matokeo yake anaishia kuongeza tatizo na hataki kukubali kwamba gari limemshinda analiweka juu ya mawe. Tutumie vizuri mfumo uliopo (on-bord diagnostic) kuepusha gharama zisizo za lazima

6. Spea zote genuine bila kujali ni Toyota au Mitsubishi au Nissan bei zake hazina tofauti. Ukitaka kuthibitisha angalia bei za spea japani kwa spea yoyote ulinganishe bei. Unaweza kupata bei hizo kwa kuangalia kwenye catalog iliyopo online Japanese cars online catalogs ingiza chasis namba yako tafuta bei ya spea mfano shock absorber ya magari aina tatu ili ujiridhishe. Hizo ni bei za spea kutoka kwa manufacturers wa magari. Kisha tafuta bei ya spea hiyo hiyo alibaba.com kwa kutumia part number.

7. Ukinunua spea ambayo ni halisi kwa sh milioni moja ukaitumia miaka 3, na mwingine akanunua spea isiyo halisi kwa sh laki moja kisha akabadili spea kila mwezi ni spea ipi ambayo ni expensive?. Tafakari.

8. Unapotafuta spea usitafute kwa jina la gari, tafuta spea kwa kutumia parts number ambayo unaweza kuipata kwenye database ya magari (nimetoa database link hapo juu), ukiweka chasis number itakupeleka hadi kwenye gari yako na utapata part number.

Umuhimu wa kutumia parts number ni kwamba spea nyingi zinaingiliana na magari mengine na ni rahi kupata spea unayotaka, lakini ukitafuta spea kwa jina la gari utaishia kulalama tu eti spea hakuna.

Mimi gari yangu ni Mitsubishi, na engine yake ni GDI. Nimetumia tangu mwaka 2009 hadi sasa, sijaona tatizo lake. Spea ni bei kubwa lakini nikibadili sitarajii kupata tena tatizo kwenye spea hiyo hiyo.

Pia natumia engine oil na NTF za BP/Castro, weka mafuta vituo vyenye mafuta mazuri, usiweka mafuta ya gari kana kwamba unaweka mafuta kwenye pikipiki, usipende kuendesha hadi taa ya reserve tank iwake ndio uende kuweka mafuta, usitumia mafuta ya kupima mtaani

HITIMISHO: Spea zipo, Kama una uwezo wa kumiliki gari nunua kama uwezo bado subiri au nunua gari inayoendana na pato lako.
Hakuna gari mbovu.
 
Nina xtrail mwaka wa pili hainisumbui. Labda kama kuna aina nyingine ya xtrail
 
Naona watu siku hizi magari haya ya Nissani Extrail wananunua sana.

Je wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu.

Mawazo ya masikini bwana, Kama huna hela kaa chonjo! Haya toa sababu tano kuonesha
ubovu wa X-trail!
 
Tatizo watu wamekariri,kuwa gari ni toyota. Hata ukiwauliza viashiria vya kwenye dashboard vina maana gani hawajui
 
Tatizo watu wamekariri,kuwa gari ni toyota. Hata ukiwauliza viashiria vya kwenye dashboard vina maana gani hawajui

hili nalo neno, hata mie nilikua muumini wa hiyo dhana
 
Mtu asikudanganye mkuu. NISSAN NI GARI BORA. Ebu angali Nissan safari, Patrol nk. Haya magari yameonyesha kumudu hali ya hewa ya Tanzania.
 
Ndugu nissan xtrail haina shida hata kidogo...hii gari inahitaji kufuata masharti yake elekezi....hii gari inatumia oil ya nissan extrail tu...hivyo watu wengi wanapofanya service huwa wanatumia oil ambayo not recommended kwa xtrail...but mtu ukitumia oil yake utaifurahia sana hii gari....ni gari nzuri....ni gari ya safar..tatizo letu watanzania tunapenda kufanya maamuzi kwa kutumia maneno matupu ya watu.....changamoto ninayoiona kwa extrail ni bei ghari ya vipuli....but vipuli vyake ni imara na original na hudumu muda mrefu

Nina X Trail lakini oil zake zile special napata wapi mkuu! Naomba unijulishe wapi kwa kuzipata?
 
Back
Top Bottom