Sio kweli.
CHA KWANZA KABISA UMJUE FUNDI ANAEJUA KUTENGENEZA NISSAN XTRAIL NA SIO TAPELI. FUNDI MWENYE UJUZI NA MUELEWA NA SIO MWENYE TAMAA!
Mimi fundi wangu miaka yote ni fundi mmoja anaitwa Deo yuko pale Mwenge alifundishwa na Nissan Wenyewe, yuko karibu na Maryland Bar opposite ITV.
Gari la kwangu nilinunua 2013 na mpaka leo ninalo na nimetembea nalo mikoa mingi sana nchi hii. Tayari tangu nimenunua nimetembea Kilometre 134,000 (nilizotumia mimi) Hili hapa:
View attachment 260838
Nimetumia magari mengi tangu ninunue gari la kwanza 1998. Nissan X-Trail haijawahi kuni-disapoint hata siku moja! Ni gari durable na comfortable hata ukiwa off road na stable barabarani sana. Nissan X-Trail spare zake ni ghali kidogo na sio kiasi kikubwa kama watu wanavyosema, ila bush, na stabiliser links ambazo ndio unabadilisha zaidi kama ni mtu wa pori kama mimi ukifunga ni mwaka. Spare zake karibu zote ni original. Vitu vikubwa vinavyokufaga na ni mara moja kwa mwaka ni sensors ambazo magari mengi ya siku hizi yanazo, usipoibadili ukaipuuzia basi unaweza kuharibu gari, gari ikaheat au tatizo lingine. Sensor moja inaweza kuwa laki mbili, ila sensor kama ya air filter mara nyingine huhitaji kusafishwa tu na spray maalum.
Muhimu usipitilize service milage, hakikisha unaweka collant na sio maji yako ya Dawasco, engene yake ni high efficient na moderm na ukiona tatizo lolote lile, peleka kwenye computer wa diagnose full stop. Iwe ni miss au engene ina mngurumo wa ajabu. Taa yoyote isiyo ya kawaida ikiwaka kwenye dashboard ni Computer tu ndio itakwambia.
Ujinga wa sisi Waafrika wengi tunataka gari ambalo hata usipofanya servie litakwenda tu na fundi yoyote ukimpa atategeneza. Ukimsikia fundi anakwambia hizi gari mbaya sana kama wanavyosema siku hizi gari za VVTI au D4 ujue huyo mbulula hana shule na hajui kulitengeneza. na ukimwachia atakuharibia gari.
Nissan X-trail haikuwahi kukwama katika tope, sio chini ya mara moja nimeziacha Rav 4, Suzuki Escudor na Hiluz Double cabin porini mimi nikapasua katika tope, vumbi na vichaka na sikupata shida yoyote. Pia clearance yake chini ni nzuri na sio rahisi kugonga.
Zingatia service yake, na ukifunga spare ni mkataba mwaka sio kama Toyota spare bei rahisi lakini utabibadili tu mara kwa mara na hutakumbuka mwisho wa mwaka umeingia gharama kiasi gani.
Kwa ealuation zaidi soma hapa:
https://www.youtube.com/watch?v=GR7kHC6yiQI