Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuh, namshukuru aliye anzisha huu uzi,, nilikuwa nmejipanga wiki ijayo naenda kununua hii gari hakika nimeghairi kimoja.
Kitu kikishatiliwa mashaka wewe ukajitumbukiza baadae ya kikuta unabakia na ninge,, ninge,, nyingi sipendi, afadhali kuepuka mapema. Kiukweli muundo wake ulikuwa unanivutia sana ila gari ya kunifanya maskini hapana,, tupilia mbali huko...
kwa watanzania wengi, gari yoyote ambayo si toyota ni 'mbovu'.......
Hiyo oil inapatikana wapi mkuu?
There is a special oil for nissan xtrail....sikumbuki jina lake but mafundi wa nissan xtrail wanazijua....
Hahahaha,hii kaliKuna kaka yangu ana xtrail kafunga injini ya Rav4 mwendo mdundo ila body ni plastic anafunga na waya/nyaya.
kwa watanzania wengi, gari yoyote ambayo si toyota ni 'mbovu'.......
Mimi niliagiza hilo gari miaka ya 2010 ila lilinitesa sana akaja jamaa kutoka Iringa nikambambika nalo baada ya kukaa nalo mwaka tu na kuona kiama chake
kwa nini huwezi kuilinganisha na HARRIER, RAV 4, HONDA CRV au KLUGER?NI MBADALA MKUBWA WA TOYOTA PRADO. HUWEZI KUILINGANISHA NA HARRIER , RAV 4 , HONDA CRV ,AU KLUGER.
Ndugu nissan xtrail haina shida hata kidogo...hii gari inahitaji kufuata masharti yake elekezi....hii gari inatumia oil ya nissan extrail tu...hivyo watu wengi wanapofanya service huwa wanatumia oil ambayo not recommended kwa xtrail...but mtu ukitumia oil yake utaifurahia sana hii gari....ni gari nzuri....ni gari ya safar..tatizo letu watanzania tunapenda kufanya maamuzi kwa kutumia maneno matupu ya watu.....changamoto ninayoiona kwa extrail ni bei ghari ya vipuli....but vipuli vyake ni imara na original na hudumu muda mrefu