Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

kuna work mate wangu, alipata nayo ajali, hapo ndipo nilijua kuwa xtrail siyo gari ni jini la kuleta umaskini. yaani taa moja kubwa 350,000 ndogo 150,000 kwa taa 4 ni 2,000,000. yaani jumla ya cost ilikuwa milion 7 na point.

Duuuuuuu hatari kabisa spea ghali mno
 
Asante High Vampire kwa uzi mzuri.
Naomba nijue ubovu wa hz nissan x-trial.

Binafsi nazipenda coz naona ni gari yenye nafasi sana na je kwa ushauri wako kama nataka kuagiza nikiagiza Voxy au Noah ntakuwa nimecheza vema na opportunity cost (kwa ku forgone xtrial)

Asante.

Hapo kwenye Noah pako vizuri ila VOXY haipo kwenye ubora kama utapata Noah ya mwaka 1999 mpaka 2001
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli, xtrail haziko reliable kabisa kama Toyota. Inaweza kukuharibikia ghafla ukashindwa kujua cha kufanya, na spea zake ni chache sababu nyingi haziingiliani na gari nyingine. Kimeo kingine ni Nissan Murano. Kama umeshafanya utafiti kidogo wa bei zake kwenye used, zimeshuka saana, sasa hivi ni affordable kwa watu wengi. Ila haziko reliable hasa kwa barabara zetu na mafundi wetu

Duh Murano tena unaumiza wwngi
 
Jamani hizi x-trial ni janga Kwa sie wenye pesa za kuungaunga siyo rafiki kabisa hizi gari na wanao bisha haijawatokea Mimi lilitaka kunisababishia umaskini ikabid niliweke bond Kwa mtu mpaka saiz nimelisahau na sina mpango wa kulichukua akitaka aliuze tu.
 
kuna work mate wangu, alipata nayo ajali, hapo ndipo nilijua kuwa xtrail siyo gari ni jini la kuleta umaskini. yaani taa moja kubwa 350,000 ndogo 150,000 kwa taa 4 ni 2,000,000. yaani jumla ya cost ilikuwa milion 7 na point.

Kiujumla gari za kisasa ambazo sio toyota ni ishu sana. Gari moja ya aina ya Escudo 2006, taa moja ya nyuma ni 900,000 kwa seti! Kama nadanganya aje mtu abishe hapa.

Tuwe makini tu ikiwa huna haja ya fasheni km ww ni 'bora usafiri' tununue ist, starlet,rav4 (<2003) ni magari mengi mno mjini ingawa hayana hadhi kwa sababu ya kuwa km uniform
 
Hapo kwenye Noah pako vizuri ila VOXY haipo kwenye ubora kama utapata Noah ya mwaka 1999 mpaka 2001

Noah is far better than voxy, nimemiliki zote I still like noah ila iwe less than mwaka 2002
 
kuna work mate wangu, alipata nayo ajali, hapo ndipo nilijua kuwa xtrail siyo gari ni jini la kuleta umaskini. yaani taa moja kubwa 350,000 ndogo 150,000 kwa taa 4 ni 2,000,000. yaani jumla ya cost ilikuwa milion 7 na point.

Maisha haya bado we na rafiki yako mnakata third party???!!!
 
Jamani hizi x-trial ni janga Kwa sie wenye pesa za kuungaunga siyo rafiki kabisa hizi gari na wanao bisha haijawatokea Mimi lilitaka kunisababishia umaskini ikabid niliweke bond Kwa mtu mpaka saiz nimelisahau na sina mpango wa kulichukua akitaka aliuze tu.

mkuu limekusumbua nini??
 
Nimekaa nayo muda mrefu sana na sijapata tatizo lolote. Nimepiga safari za nje ya nchi kama safari sita kwenda Uganda na Mara nane Congo. Sijapata tatizo lolote. Sasa mtu anapokuja na story nyingine namshangaa.

Oil ya gearboc ni Dx4 smbayo nayo mnaibadilisha kwa makosa. Inabadilishwa baada ya km 130000. Ball joint zipo imara sana zijabadili kiasi kwamba ningekuwa na Toyota ningeisha badili kama mara saba. Ni gari zuri sana.
 
Naona watu siku hizi magari haya ya nissani extrail wananunua sana je wanajua kuwa ni mabovu na spea zake ghari au hawaambiwi na watu

pole sana mkuu kwa fikra zako hizo sijui kama utakuja kuweza kumiliki magari ya europe.
na bila shaka kama unamiliki gari utakuwa unamiliki hizi gari za promotion aisee.

mziki wa nissan hautaki fake fake na hata hizo toyota bado hujakutana na toyota za technologia ya miaka ya 2010.gari yenye engine ya d4 mtu kama ww lazima utailaani tuu.

huwezi kamwe fananisha nokia jeneza na nokia touch bei ya touch peke yake ni bei ya nokia jeneza hata 3 hapo lazima uilaum simu kuwa ni mibovu na haitengenezeki
 
Marafiki, mimi natumia Nissan QR20 (NT30) tangu May 2008.

Ni gari nzuri kwa mambo yafuatayo:
1. Fuel consumption ni ya kawaida
2. Inachanganya mwendo haraka
3. Ina nafasi ya kutosha ndani
4. Inatengenezeka (haina complications kama Pajero IO, the GDI)
5. Engine, wheel na gearbox parts zinapatinaka kwa wingi isipokuwa baadhi ya parts kama Exhaust systems ambazo mpya hazipatikani, only in used parts shops na bei yako ni nouma.
6. Mafundi wa kibongo wanapatikana kwa wingi

Mapungufu yake makubwa ni:
1. Spares very expensive kwa mmiliki mwenye kipato cha chini na kati e.g. CV joint moja inauzwa 600'000, shock absorber ya mbele moja 350,000 mpaka 400,000 (Duka la MasterCard Kariakoo ambao wanauza spare halisi za Nissan)
2. Mfumo wake wa radiation kwa nchi za joto unasumbua (ukitembea safari ndefu, e.g. Km 600 plus, mara 3 au 4 inaanza kuchemsha)

Otherwise kama unajiweza kifedha ni gari nzuri tu.

Asante.
 
Ila ukifunga spare ya Nissan Xtrail ni mkataba wa muda mrefu, zinadumu sana. Unaponunua, check hali ya gari hasa Engine.
 
oil inaitwa Nissan unapatikana master card msimbazi kariakoo. Ziko varieties kadhaa.

mkuu nissan hawataki magumashi kabisa na kama wabongo tungekuwa niwafuatiliaji kwenye utumiaji wa magari na kuyahudumia ipasavyo hakika yangekuwa yanadum sana tuu.

na hasa hawa nissan kwa kuwa hawana fake spea kabisaa.zinadum sana gari zikihudumiwa vizuri sasa mtu unakuta anafanya servirce anaweka oil ya kupima hydrolic ya elfu 5 kwa lita 1.why magari yasiharibike??
oil filter elfu 3500 hahahahaha.

kitunze kikutunze na kidumu.
 
Noah is far better than voxy, nimemiliki zote I still like noah ila iwe less than mwaka 2002

noah na voxy kwani kunatofauti gani mkuu.

ukiachana na ile model ya noah box hizi zingine ni sawa karibia kwa kila kitu isipo kuwa kwa taa ya mbele na nafasi ndani tuu ila vipuli ndio vile vile
 
Back
Top Bottom