Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Mjadala: Je, ni kweli Magari aina ya Nissan Xtrail ni mabovu?

Duuh, namshukuru aliye anzisha huu uzi,, nilikuwa nmejipanga wiki ijayo naenda kununua hii gari hakika nimeghairi kimoja.

Kitu kikishatiliwa mashaka wewe ukajitumbukiza baadae ya kikuta unabakia na ninge,, ninge,, nyingi sipendi, afadhali kuepuka mapema. Kiukweli muundo wake ulikuwa unanivutia sana ila gari ya kunifanya maskini hapana,, tupilia mbali huko...

Kama unahela nunua tu maana hela yako itasaidia pale
Spea ukiambiwa kiasi fulani ww unatoa tu ukiambiwa agiza nairobi unatoa tu ila kama una hela ya kiasi bora toyota huwezi anza kuagiza mbali kama uko mikoani mara uende dar ni shiida
 
Unaweza kutupa sababu za msingi??

Usipeleke gari service vichochoroni,,,peleka kwa dealers ambao wamekuwa authorised na Nissan kwan ndo wanayajua magari vema. Ukipeleka kichochoroni unapigwa oil fake unaendesha wiki mbili then autoparts zina kuwa useless. Tuache janja janja ya kukwepa gharama.
 
Jodeo
Kwa hiyo unashauri watu wanunue ila wawe makini kwenye service pamoja na utunzaji wa hali ya juu?
 
Last edited by a moderator:
Jodeo
Kwa hiyo unashauri watu wanunue ila wawe makini kwenye service pamoja na utunzaji wa hali ya juu?

Ndivyo inapaswa kuwa mkuu. Tukiuliza wangapi wanaweza kununua land cruisers,, sidhani kama Kuna mtu atanyoosha mkono. Ni being gari ila vifaa vyake very cheap and vipo kila mahali. Nissan being rahisi,,vipuli bei ghari,, utunzaji ni nidhamu.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nissan hawataki magumashi kabisa na kama wabongo tungekuwa niwafuatiliaji kwenye utumiaji wa magari na kuyahudumia ipasavyo hakika yangekuwa yanadum sana tuu.

na hasa hawa nissan kwa kuwa hawana fake spea kabisaa.zinadum sana gari zikihudumiwa vizuri sasa mtu unakuta anafanya servirce anaweka oil ya kupima hydrolic ya elfu 5 kwa lita 1.why magari yasiharibike??
oil filter elfu 3500 hahahahaha.

kitunze kikutunze na kidumu.

Hahahahahaha Mkuu u made my day hapo kwenye red.. Ila umenena ukweli kabisa, Watanzania kuhudumia magari yetu hatuwezi kabisa. Mtu hapeleki gari service mpaka liharibike au apate safari ndefu unategemea nini??

Kuna ndugu yangu mmoja ana miliki baadhi ya magari ya Europe na US.. Ukienda kwake anajitwalia tu na kuendesha utakavyo ila kwa sharti moja tu, likikuishia wese simama piga simu atakuja mwenyewe aende nalo kituo cha mafuta anachokiamini au hata kama hayafiki atatafuta means hicho kituo kimletee mafuta hapo hapo alipo. Basi kwa kufanya hivyo baadhi ya ndugu wacha waanze kumzushia jamaa ni mshirikina, kumbe anajua hawa wajinga ukiwaruhusu waweke mafuta kiholela tu watakuwekea vilita mbili mbili tena mafuta feki wamuulie gari zake
 
Wanaolalamika walinunua Xtrail bila kujua gharama zake haha sio kweli kuwa gari ni bovu.. binafsi siwezi kununua gari ambalo cv joints tu zikianza kupiga kelele unauma meno sitaki kabisa nilishatoka huko.
 
Mtoa mada we unatumia gari gani labda mimi nina ilo nissani nimenunua mwaka 2012 mwez wa tano mpaka apa napozungumza ni mwendo wakumwaga oil tu sijawah gusa kitu chochote na nazurula naloo kinyama mikoani ubovu wake nini na nataka .
 
hapa tunaongelea ghalama za spea
 
Nina Xtrail mwaka wa 3 Hainaut Shida hata kidogo. Cha muhimu service Kwa wakati in Gari Nzuri na very comfortable kuliko Toyota Nyingi
 
Nataka kuagiza NIssan Elgrand, 3500 cc, 4wd, Kwa ajili ya safari Za vijijini, Mwenye uzowefu nayo naomba ushauri tafadhali
 
Back
Top Bottom