Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Sawa kabisa. Nami naanza ku"left".
 
Bro. Hata mimi nilikuwa na mtazamo huo..Ila niliubadili yaliponikuta..nilikuwa spendi magroup ya michango michango..
Sasa mim sio wew...ifike mahala harus mtu ajigaramie..mbona wenzetu wanafanya hvyo
 
Itakua uko loaded wewe
Yan hata kikiwaka unavuta atm card yako unatoa miamala ya kutosha so hujali wala nini!
Kwa ambao kila kukicha afadhali ya jana siwashauri kabisa mfate ushauri wa mtoa mada,tulieni humo yakikufika zile elf 5 na 10k huwa za msingi sana!
 
Tunataka mzunguko wa pesa mtaani.
Hizo pesa mnazochanga zinatawanyika kwa watu waliojiajiri...wapiga picha, wapishi, wapiga tarumbeta, nk nk.

Mleta mada acha hizo bhana...usipochanga sisi wajasiriamali tule wapi?
 
"Mimi sitak nasema Sitak"

Shemeji yetu hapo anakuwa amekugomea nini mfano?
Hapo namsengenya labda hyo nguo yako kwakwel hapana..au mmmh..pilau ndo linapikwa hivyo???

Au.."katika basi"..ndo utaskia "sitaki..nasema sitaki"
 
Mimi sichangii chochote zaidi ya gharama za matibabu na msiba tu.
 
Mods..mambo ya kutuunga uzi wakongwe wa jf kama sis mnatukera...nyie achen

Mtu tokea 2012 mnaniungia uzi utafkir mtoto aliejiunga jf 2020
 
Inategemea na uwezo wa mtu lakini mimi sichangii wedding, sendoff wala kipaimara.
Bro..kwa.mtu mzima life ni kusapotiana..sio lazima utoe Kama fulani alichotoa..toa/changia kutokana na mfuko wako...hata buku itakuwa Kama mark alart kwa watu / mtu uliyemchangia..japo now days ukichanga 100 tarajia kupata 100 nawe..hata kama uliyemchangia anauwezo wa kutoa zaidi ya hio..hata jali Hali yAko..

Michango ni uwekezaji.
 
Sasa mim sio wew...ifike mahala harus mtu ajigaramie..mbona wenzetu wanafanya hvyo
Hatujafika kwa wenzetu aisee..then hao ni mabepari sisi ni wajamaa..haukatazwi..Ila jua watu wanakuchora tu..maana Kama Sio harusi Basi Kuna msiba..kuumwa nk..watakuacha ufight mwenyewe
 
Wazo langu ni serikali kuingilia kati na kupiga maraufuku michango isiyo ya maendeleo. Mfano harusi, na mifano yake. Watanzania huu utamaduni ni wa nchi za kipato cha chini. Mungu ametujalia kuingia kipato cha kati, kwa hiyo michango ya harusi inaondoka yenyewe. Naomba wabunge waokoe hili janga ni tishio kwa wananchi maskini na matajiri pia.
 
Hatujafika kwa wenzetu aisee..then hao ni mabepari sisi ni wajamaa..haukatazwi..Ila jua watu wanakuchora tu..maana Kama Sio harusi Basi Kuna msiba..kuumwa nk..watakuacha ufight mwenyewe
Wew unaelekea huwa unafanywa mwenyekit kabisa..acha hyo tabia mbaya..kama huna uwezo usifanye harus.sio kusumbua watu..misiba changia..mgonjwa changia..ada changia.ila sherehe..ni aibu
 
lakini pia mjiulize nyie hamkuchangiwa? wadogo zako wakitaka kuoa hutaomba michango? tuanzie hapo kwanza ingawa hata mimi sikubaliani kabisa na suala la michango
 
Unatoa mchango,
Unatoa zawadi,
Unatafuta nguo+viatu.

Baada ya mwezi wanaachana.
Kuna mmoja hapa juzi Kati aliniletea kadi nimchangie

Huyu ni demu niliyempenda Sana nilitamani awe mke wangu .

Wakati namtokea alijibu nyodo Sana akaenda kwa kibosile Fulani ambaye ni kitombi ile mbaya yaani kitaa tunamjua[emoji1787][emoji1787]

Basi nikavunga mchango wao wakaona.

Umepita mwaka mmoja tu nasikia wameachana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nikasema afadhali hela yangu nilinywea bia[emoji1][emoji1][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…