Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Hivi kwanini watu mkiamua kuoana msifanye kitu kilicho ndani ya uwezo wenu,? Kama ni utamu au uchungu mnaenda kupata wewe na mkeo/ mmeo why tabu mtupe wengine.mnakeraaaa..
Namshkuru Mungu, hili jambo nililimaliza kwa kushika mshati ndugu pekee hadi watu wakawa wanashangaa kuwa sikuwaomba michango
 
Mwingine eti hoo siku ya kuzaliwa naomba mchango wako.nikawa natukana kimoyo moyo kila text ya kukumbushia ikiingia
 
Kama mnajiweza mnaomba hela za michango za nini?
mimi nilivyooa niliomba michango kwa watu niliowachangia na wale niliotarajia wao wataniomba marafiki 10 tu walinichangia 4 nilishawachangia 6 ni wapya. gharama nyingine nilibebeba mwenyewe kamati na familia, sikuwahi mpigia mtu simu kumuomba mchango meseji nilituma 4 hazifiki sherehe ilikuwa ndogo classic maisha yanaendelea. kushindwa kuchangia arusi ni umasikini sababu sio lazima utoe kiwango kilichotajwa unashindwaje mchangia rafikiyako hata 30 na unafanya kazi? Japo siwezi mchangia mtu ambaye hajanichangia.
 
hongera sana, watu mnakaa kwenye kamati wanapiga hesabu kila mtu anywe bia 10, jamani huu si ulafi uliopitiliza?
 
Dah! Michango hii inakera. Binafsi nilishaamua kuonekana mbaya kwa kuwa sichangii sherehe za watu. Mwanzoni wakawa wanasema ngoja tuone harusi yake ataifanyaje, kumbe hawakujua ninachowaza. Nilifunga ndoa Bila kumchangisha mtu hata mmoja, hili lilinipa uhuru sana,maana watu wangu wa karibu wamethibitisha kuwa sikuwa natania kwenye hili, tuungane kwa pamoja kuipinga michango hii, inatuletea UMASKINI.
 
Yaan sasa hiv mtu anataka kuoa yeye kero inakua kwa watu wngne..yaan unastukia umeingizwa kwenye group sjui la watu uliosoma nao shule ya msing.marra sekondari mara wap sjui..mara group la ndugu wa ajabu ajabu..ndugu wa family yako kweli iala sjui mtoto wa mjomba ake mama gan sjui huko etc etc

Halaf watu wazima wanachat ujinga..msg simu inajaa had inapata moto...

Mim sitak..nasema sitak..(msemo wa shemej yenu huu)

Enewei ishu ndo hyo

Michango imekua miing sana.ukigeuka huku mwenyekit wa jumuia nae anakukimbikiza na daftar la michango

Michango michango michango

Ya harus imezid sasa

Ifike mahal kila mtu abebe mzigo wake..mbona kwenye mambo ya maana hamsaidiani...ushawia skia watu wanajichanga kumchangia mtu mtaj wa biashara...

Nasemaje...juzi nilianza left magroup kama sina akil nzur...well ...niliya mute lakin bado naona kero kubwa...

Kisingizio ooh ukipata shida hutasaidiwa...well in life watu wanaoweza kukusaidia ile kwelkwel hawazid wa3...wengne ni kupotezeana muda tu

Uzi tayar...wale wapenda magroup na michango ya harus najua mtaponda...kuna watu kwa kupenda kuongoza kamati za harus hawajambo ..wanahis wanaongoza kamat za bungen .
 
Back
Top Bottom