Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Umeoa usiku wewe
Mimi nimeshasema sitokuja kuchangia harusi ya mtu.
Mambo mengine ni ujinga tu,kama mmeamua kufanya jambo fanyeni kile kilichopo ndani ya uwezo,mambo ya kuomba omba pesa tena kwa nguvu nyingi ni kujitia aibu.
 
Hivi kwanini watu mkiamua kuoana msifanye kitu kilicho ndani ya uwezo wenu,? Kama ni utamu au uchungu mnaenda kupata wewe na mkeo/ mmeo why tabu mtupe wengine.mnakeraaaa..
Hii ni kero kubwa Sana hasa miaka hii.
 
Mimi mwenyewe inanikera sana yaani hapa ninakadi inahitaji mchango.

Wanafikiria wote ambao hatujahalalisha mahusiano yetu tunapenda hamna wengine hatupendi. Kama mimi natamani sana siku moja nisimame mbele yababa paroko nikiwa namwenzangu ila usawa unabana nahatutaki kuwasumbua watu kwastarehe zetu.

Yaani hapa nimepanga nikipata milioni 2 ambayo nitakuwa sina hesabu nayo basi nafunga ndoa nabejeti yangu nihiyohiyo kiingilio ukumbini nikinywaji chako endapo kama utapenda kunipa kampani.
 
Sio lazima uchangie, huo ni mchango wa hiari na sio lazima. Kama huyo mchangiwaji mna bond lazima utajisikia vibaya na kumchangia, kama ni mtu baki wala hutajigusa.
 
Kuchangia/kuchangiwa siyo Jambo la lazima..hujisikii kuchangia usitoe ahadi ili kuepuka msg za usumbufu..
 
usipo pata mwaliko unalalamika! kadi ikijaya mwaliko unalalamika pia.

tukuweke kundi gani?
 
Kama unayo wachangie tu lakini kama huna tulia tu kimya.
 
Hivi kwanini watu mkiamua kuoana msifanye kitu kilicho ndani ya uwezo wenu,? Kama ni utamu au uchungu mnaenda kupata wewe na mkeo/ mmeo why tabu mtupe wengine.mnakeraaaa..

Ushaolewa ? Ilikuwaje wakati unaolewa ?
 
Back
Top Bottom