Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Ni kweli ndomana sitaki kuongezewa umaskini
Kiufupi suala hili linakera sana sana, wengine tumeumbwa kwa haya tunachangia ila maumivu yanaishia ndani kwa ndani. Ila lazima tubadilike waweza fanya harusi ndogo ya chini ya 2M na maisha yakaenda. Kinachoniuma zaidi sikuchangisha mtu nilipokuwa naoa na sikutumia zaidi ya 3M ila sasa msururu wa kadi, message, simu mpaka unatamani kuzima simu.
 
Sijawahi changia harusi wala sitakuja kuchangia. Kwanza mimi nitafanya ndoa tu navaa dira langu jekundu kama bibi harusi wa kihindi , ni kutia ubani, watu wale biriani wasepe. Shuhuli inafanyika nyumbani kwetu nilikozaliwa na kulelewa. Tusichoshane hayo maswala ya shela ni ya kizungu.
 
Kiukweli juzi nimeshangaa kidogo, huyu tulisoma nae,sasa anaoa hana kazi maalum lakn anaoa na wazazi wake kidogo mambo siyo mabaya.

Mchango 100,000 double na single 70,000/

Ikabidi tu nimuulize hii harusi ni unatafuta mtaji wa biashara ama inakuwaje? Hakujibu kitu kabisa na amesema hatokuwa na card za pesa ya chini hapo. Ukitoa 60,000 kushuka chini hakuna card! Ukitoa 80,000- single!

Nikamwambia sitakuchangia kwasababu sina hela hyo niliyonayo ni single 40,000/ tu. Akanifata inbox anasema niongezee angalau ifike 50,000/- nikachukua hela yangu nikaenda kununua mafuta ya kupikia.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] Hapo kwenye viwango ndo huwa nachoka kabisa.... Utasema aliwekeza Kwako
Kiukweli juzi nimeshangaa kidogo, huyu tulisoma nae,sasa anaoa hana kazi maalum lakn anaoa na wazazi wake kidogo mambo siyo mabaya.

Mchango 100,000 double na single 70,000/

Ikabidi tu nimuulize hii harusi ni unatafuta mtaji wa biashara ama inakuwaje? Hakujibu kitu kabisa na amesema hatokuwa na card za pesa ya chini hapo. Ukitoa 60,000 kushuka chini hakuna card! Ukitoa 80,000- single!

Nikamwambia sitakuchangia kwasababu sina hela hyo niliyonayo ni single 40,000/ tu. Akanifata inbox anasema niongezee angalau ifike 50,000/- nikachukua hela yangu nikaenda kununua mafuta ya kupikia.
 
Kuna jamaa alichangiwa akasepa na michango yeye na mkewe maana alipokuwa anawaomba watu mtaji wa biashara wanagoma kumpa Ila mchango walitoa fasta!
Akaja kuwalipa baadae kidogo kidogo wachangiaji mpk akawarudishia wote michango yao
 
Back
Top Bottom