Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

nafikiri ni wakati wa kubadilika na kuacha kuchangia mambo yasiyokuwa na tija ivi tuna watoto wangapi kwenye familia zetu wasiokuwa na karo za shule ,tuna wagonjwa wangapi wanahitaji matibabu,mitaa yetu tumeshindwa hata kufukia makorongo kuchangia mil 25 kwa ajili ya kutumbua masaa machache halafu kesho maharusi wanaamka wakipiga miayo kwangu huo ni upuuzi uliopitiliza .
 
Nimeacha kuchangia harusi na sherehe zote. Kwenye shughuli yangu ya harusi sihitaji pia mchango wala zawadi kwanza nyumba yangu ni ndogo, kupokea zawadi za mchina.

Mmmh,
Jamani mbona wachangiaji mnanitisha, inaonekana wengi bado hamjaoa/hamjaolewa kwa jinsi mnavyoandika......

Anyway, ni kweli tabia hii tunaiendekeza tu bila faida za msingi, i remember on my wedding tulialika ndugu na marafiki home, tukapika pilau na wali plus nyama kama sherehe ya krisimasi tu vile, na ilipendeza sana tu, cha msingi ni ile inayoitwa ndoa, ule muunganiko wa watu wawili unaofanyika kanisani/msikitini.

Nawashaurini wala msiogope kuoa kisa kuchanga, ila la Msingi ni lazima muoe / muolewe ili mpate kukamilika wandugu
 
Nadhani ni wakati wa kubadilika sasa, kila kukicha michango, hebu tuhesabu, 1. kitchen party, 2. Send off , 3. Wedding Day. Unajikuta wachumba wote unawafahamu na unapaswa kuwachangia.
Tatizo lingine naona na ushindani pia, yaani mtu anataka harusi yake iwe kama ya fulani!!
Tubadilike jamani hata kwa wale ambao wamemaliza, sio lazime walipe fadhila tena kwa kuchangia wengine. Kuna michango mingine ya shule, ugonjwa, kutunza familia, watoto yatima nk.
Mi nadhani anayetaka kuoa agharimie sherehe yake!!! Kuna nchi nyingine tena hapa Afrika wanafanya hivyo kwa nini sisi wabongo tushindwe?
 
Wangapi humu mnaopinga hii michango lakini mmeshawahi kuchanga na mnaendelea kuchangia hizo sherehe kubwa?

Manake watu tunapenda sana kuchonga domo dhidi ya kitu fulani huku wakati huo huo tu washiriki wakubwa wa hicho kitu au jambo tunalolipinga!
 
Dr Olomi my research supervisor nakuunga mkono, binafsi kwenye harusi yangu tuliomba kuitwa tu watu tunaowajua, such as friends and family ONLY sikuchapisha kadi ya mchango hata moja! Harambee ilifanywa moja tu na watu walitoa wanavyojisikia ambao ni ndugu na jamaa, harusi ilikuwa nzuri sana,
Sipendi kushiriki harusi za watu nisiowajua, na nitaendelea kuchangia harusi za ndugu zangu na marafiki wa karibu, ni moyo tu sii utajiri..sherehe ya harusi kwa mtu wako wa karibu ni outing nzuri inayokutanisha ndugu mnacheza na kufurahi..kuhusu kuchangia elimu, hilo pia tunalitekeleza kwa mfuko wa kijijini kwetu, pia tuna saccos ya cousins..wazee wa FOE mpooo ?
 
Siku hizi michango imezidi hadi birthday tunatakiwa kuchangia.
 
kuchangia inategemea uhusiano na mchangishaji Jambo la msingi ni nani ametengeneza hafla ya kuchangia maendeleo akakwama hapo ndipo kwa kuanzia sio useme wale tuliowachangia watutose
 
Tusipindishe maneno kwa manufaa ya ushabiki this is what i said
So to you its all about eating and drinking no matter hao maharusi wanakwenda kuanza maisha yao vipi..... for you the occassion its all about feeding tumbo lako na kuhakikisha mchango wako umetumika??????

So this means A amechanga..... A anahakikisha alichokichanga anakwenda anakila na its worth mchango wake..... Hajali B ambaye ndio anafunga ndoa anakwenda kuishi vipi (nyumba ya kupanga..... na shughuli nyingine..... mara nyingi siku hizi hata bibi Harusi anakuwa na mimba tayari) huyu A hajali hayo

kesho A atakapokuwa na function anategemea huyu B ambaye ndio kwanza kapata haya majukumu mengine ya maisha amchangie
Yaani huelewiki nini unachoongea hapa!
 
Siku hizi michango imezidi hadi birthday tunatakiwa kuchangia.

Mchango wa nini sasa kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa? Kununulia keki na mishumaa?

Watu wengine sijui wakoje tu. Mtu kama huna uwezo usilazimishe kufanya mambo usoyaweza. Kuombaomba michango ya sherehe ni kuleta usumbufu tu kwa watu na kutaka kupeana lawama.
 
Muasisi wa ujumbe huo ninamkubali sana, ni mwalimu mzuri sana wa ujasiliamali BiD Network - Donath Olomi pale UDSM. Nafikiri atakuwa ameona ni jinsi gani mitaji inavyotumiwa isivyo. Mi binafsi huwa siifagilii sana michango kwani. Kuna watu usipomchangia ujue ofisini mmeshakuwa maadui na atakununia wewe na kukusema kila aina ya neno kana kwamba alikuwa anakudai.

Umefika wakati sasa masuala ya michango yawe ni hiyari ya mtu kama ilivyo michango ya vifo. Kwenye mazishi mtu anatoa alicho nacho. Mtu akikuletea kadi inayosema ukichangia kiasi fulani basi utapata kadi ya mwaliko wa kuhudhuria sherehe mwambie kuwa wewe huhitaji kuchangia ili ule bali unamsaidia tu na toa ulicho nacho. Mimi binafsi wakati wa sherehe yangu nilipata shutuma nyingi sana eti sikuwachangisha watu, nikawaambia kuwa sherehe ni yangu mimi na nilifanya kilicho ndani ya uwezo wangu.

Tuache utamaduni wa kufuja pesa kwa usiku mmoja, tuchangie maendeleo badala ya kula na kunywa. Kuanzia leo ukiniomba mchango wowote wenye kiwango jua sitoi, ila nitakupatia at maximum Tshs 20,000 na sihitaji kadi ya mwaliko kama sharti ni kuchanga. Tuchangie elimu na maendeleo sasa badala ya kula na kunywa.

Big up Mzee wa UDEC
 
Ngumu sana kuindoa hii tabia bila ya any enforcing mechanism.

Ningekuwa mimi ndiyo govt, ningetunga ka-regulation kadogo chini ya income tax act na kufanya ungangari ufuatao:

1) vikao vyote vya maadalizi lazima viwe registered - otherwise it's illegal with a Tshs 2M fine when found. Inawezekana bana!!

2) kodi (say 25% ya michango yote) zikatwe na zielekezwe kwenye barabara, pembejeo, shule na hospitali.

Inawezekana bana!

Mkuu hili linawezekana. nchi za wenzetu huruhusiwi kuchngisha bila kuwa na kibali cha kuchangisha. na michango yote inatakiwa kuwa ni kwa manufaa ya jamii tu, mainly charities. Sasa na sisi tungeweka sheria kuwa kuchapisha kadi ya kuomba michango ni lazima upate kibali maalum. Mbona kuna watu huwa wanatembea na barua za wakuu wa mikoa zikisema mtu fulani asaidiwe kutokana na hali yake hapa Bongo?, kwa nini sheria hii hii isitumike kwenye michango ya harusi et al?
 
Sasa we unataka kwenda kula wenzako walivyochangia..Agrrrr!! Chako chako chetu chako?

Its shows your way of thinking
Harusi kwako equals kula
I REST MY CASE

na hivyo vyakula si vimepatikana kwa hela uliyochanga wewe

So to you its all about eating and drinking no matter hao maharusi wanakwenda kuanza maisha yao vipi..... for you the occassion its all about feeding tumbo lako na kuhakikisha mchango wako umetumika??????

Hahaha yaani mpaka mtu anaamua kuoa hajui anaenda kuanza maisha vp? Lol

so you are simply telling me kwamba until unaenda kuoa haujui unaenda vipi kuanza maisha??? That is absurd and ridiculous

to me a definition of poor person is the person who is living under one dollar, a person who lacks food and shelter, halafu hii issue ya kwamba if you dont have a house you are poor nani kasema?????

My friend you are either blind or you dont know what you are saying...... defn of poor Having little or no wealth and few or no possessions. Lacking in a specified resource or quality; (You see you might be wealthy in material things but poor in thinking... which am afraid am getting into that conclusion)....... Also look what I wrote They are Still Poor and they dont have a house ...... Did you see the AND......(means ni masikini na hawana hata nyumba) Hope am understood.

Tusipindishe maneno kwa manufaa ya ushabiki this is what i said
So to you its all about eating and drinking no matter hao maharusi wanakwenda kuanza maisha yao vipi..... for you the occassion its all about feeding tumbo lako na kuhakikisha mchango wako umetumika??????

So this means A amechanga..... A anahakikisha alichokichanga anakwenda anakila na its worth mchango wake..... Hajali B ambaye ndio anafunga ndoa anakwenda kuishi vipi (nyumba ya kupanga..... na shughuli nyingine..... mara nyingi siku hizi hata bibi Harusi anakuwa na mimba tayari) huyu A hajali hayo

kesho A atakapokuwa na function anategemea huyu B ambaye ndio kwanza kapata haya majukumu mengine ya maisha amchangie

Yaani huelewiki nini unachoongea hapa!

Je hapa ni nani ambaye haeleweki???????
 
Naunga mkono hoja hii, niko mbioni kupunguza kiasi then kuacha kabisa nibaki kuchangia matibabu, elimu na suala jingine la kijamii. Asante Dr. Olomi pamoja na Dr. Nguli
 
Nafikiria sana kuachana na kuchangia matukio ambayo ni ya kianasa na ambayo ynawezekana kufanywa na wahusika wenyewe na ndugu zao

Mimi nitaanza kuchangia wagonjwa, walemavu, na huduma nyingine za kijamii

Nimependa topic ya Dr. Nguli na Dr. Olomi (Jukwaa la Habari Mchanganyiko)
 
Uliza ambapo haukuelewa ueleweshwe sio kutoa comment just because you can.....
yaani nikikuuliza utarudia yaleyale ambayo nimeshindwa kukuelewa!
Mara upuuzi, mara mie nachanga ila kwa marafiki wa karibu, mara watu wanaanza maisha, mara watu watu wanabaki maskini, mara unalazimishwa kuchanga! Mi sikuelewi unajua!
 
Ngumu sana kuindoa hii tabia bila ya any enforcing mechanism.

Ningekuwa mimi ndiyo govt, ningetunga ka-regulation kadogo chini ya income tax act na kufanya ungangari ufuatao:

1) vikao vyote vya maadalizi lazima viwe registered - otherwise it's illegal with a Tshs 2M fine when found. Inawezekana bana!!

2) kodi (say 25% ya michango yote) zikatwe na zielekezwe kwenye barabara, pembejeo, shule na hospitali.

Inawezekana bana!

mze M.mbabe, umenifurahisha sana! Haha lol
 
Back
Top Bottom