MADAM T
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,747
- 2,977
mbona kabla ya kuchangiwa kwenye harusi zenu hamsemi hivyo mkiisha changiwa na kufunga ndoa ndio mnaanza ohoooo eti ni upuuzi na upumbavu haya banaaa
Tell them!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mbona kabla ya kuchangiwa kwenye harusi zenu hamsemi hivyo mkiisha changiwa na kufunga ndoa ndio mnaanza ohoooo eti ni upuuzi na upumbavu haya banaaa
Yaani jambo hili kumbe linakera kila mtu eeh! Kama umechangiwa, basi unaweza kuchangia kwa hao waliokuchangia, kwa kuwashukuru kwa kusema asante!
Unajua ndio maana ndoa nyingi za kifahari hazidumu! Maana watu wametoa kwa manug'uniko sasa baraka itoke wapi? Mie nafikiri cha maana ni kufunga ndoa, mengine ni kufuru tu. Tena utakuta watu wameleeewa ile mbaya!
Mie niko nawe mtoa hoja, nilishapunguza sana kuchangia, na kama ukiiniita kwenye kamati ndo kabisa siji. Unakuwa na kadi 10 na kila moja ina kiwango cha 50,000/= utafikiri wanajua badget yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Naona umeirudia avata yako ya ukweli.
https://www.jamiiforums.com/customa...ko fit kwenye lyrics ile mbaya, na hana makuu
Pia ukiona mtu hujawasiliana nae kwa muda mrefu akikupigia usipokee simu hio ni KADI ya mchango
My friend you are either blind or you dont know what you are saying...... defn of poor Having little or no wealth and few or no possessions. Lacking in a specified resource or quality; (You see you might be wealthy in material things but poor in thinking... which am afraid am getting into that conclusion)....... Also look what I wrote They are Still Poor and they dont have a house ...... Did you see the AND......(means ni masikini na hawana hata nyumba) Hope am understood.
What does this have to do with me getting married kama naoa na watu wanataka kunichangia nitakaa???????
Has this got to do with anything we are talking????!!!
Mtu anaanza kukupigia baada ya miaka mitano.......anajizoeza kupiga siku tatu...siku ya nne, mchango! :redfaces::redfaces:
Nguli na wengine,
Naanza kufarijika kuwa jumuiya inayonizunguka inaanza kuona hili. Wakati nakuja Tanzania toka huko nilikuta mambo haya yamepamba moto sana. Sikuwahi kuhisi wala kujua kuwa watu huchangishana na kuamua kuangamiza kiasi kikubwa kama hiki kwa muda mfupi sana. Wakati huo kuna jamaa yangu ndugu alitualika kwenye kikao alichokiita Kikao cha ukoo. Kufika kwenye kikao nikaambiwa kikao cha harusi. Nilikataa kuchangisha na nikawapa darasa kuwa kwenye ukoo wetu kuna vijana wengi ambao wangeweza kuchangia harusi kam wangekuwa wamewezeshwa kwenye elimu. Nikawaambia na wakakubaliana nami kuwa kweli kwenye ukoo wako ambao walishindwa kuendelea na shule kisa kukosa ada! Mimi nilikataa wazi kuwa siishi kwa kuteketeza fedha kwa siku moja. Tangu wakati huo nimeishi kwa dunia ninayoiamini mimi. Ulifika wakati dini ikanilazimisha nifunge ndoa. Nilikubali kwa kuwa mama yangu alinisihi ili arudi kundini. Nilifunga ndoa. Ndoa yangu haikuwa na watu zaidi ya 20. Na niliwaalika na kulipia bili kama niendavyo baa. Kidogo kidogo wadogo zangu kwenye ukoo nao wakafata nyayo zangu. Niongeapo sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa elimu wa ukoo. Tunataka mwanaukoo yeyote asishindwe kuendelea na shule kisa kakosa ada. Baada ya hapo tutaendelea na jamii inatotuzunguka hadi hapo tutakapotokomeza ujinga kijijini kwetu.
Ni wakati muafaka kwa Watanzania wote kuacha mtindo huu wa kuchangisha fedha nyingi kwa sherehe badala yake wawekeze kwenye kuchangishana kwa elimu. wakati fulani huko Kenya utasikia bandiko " FAMILIA YA SO AND SO INAKUKARIBISHA KWENYE HARAMBEE YA KUMCHISHIA MTOTO WAO ANAYEENDA KUSOMA MAHALI FULANI" na believe me wamefanikiwa sana. Why not us? Harusi ni suala ambalo ni very personal, wenzetu hagharimiakia shughuli hizi kwa mifuko yao sio kutegemea mifuko ya watu. Kama ni kuiga TUACHE SASA!
Nimaecha kuchangia harusi na sherehe zote. Kwenye shughuli yangu ya harusi sihitaji pia mchango wala zawadi kwanza nyumba yangu ni ndogo, kupokea zawadi za mchina.