Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Yaani jambo hili kumbe linakera kila mtu eeh! Kama umechangiwa, basi unaweza kuchangia kwa hao waliokuchangia, kwa kuwashukuru kwa kusema asante!
Unajua ndio maana ndoa nyingi za kifahari hazidumu! Maana watu wametoa kwa manug'uniko sasa baraka itoke wapi? Mie nafikiri cha maana ni kufunga ndoa, mengine ni kufuru tu. Tena utakuta watu wameleeewa ile mbaya!
Mie niko nawe mtoa hoja, nilishapunguza sana kuchangia, na kama ukiiniita kwenye kamati ndo kabisa siji. Unakuwa na kadi 10 na kila moja ina kiwango cha 50,000/= utafikiri wanajua badget yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ha ha ha ha kumbeeee eeh inawezekana aiseee:teeth:
 
Pia ukiona mtu hujawasiliana nae kwa muda mrefu akikupigia usipokee simu hio ni KADI ya mchango

Mtu anaanza kukupigia baada ya miaka mitano.......anajizoeza kupiga siku tatu...siku ya nne, mchango! :redfaces::redfaces:
 
Uwiano kati ya michango ya miradi ya maendeleo na michango ya mambo ya burudani pengo lake ni kubwa sana.

Laiti watu wangekuwa na hamasa ya kuchangia mashule, hospitali, ujenzi wa maktaba n.k. pengine tusingekuwa na shule ambazo ziko chini ya miti au huenda tusingekuwa na wagonjwa wanaolala kwenye sakafu za simenti!!

Lakini minuso ya harusi na upuuzi mwingine kama huo ni full kujiachia mfukoni. Ajabu sana.
 
My friend you are either blind or you dont know what you are saying...... defn of poor Having little or no wealth and few or no possessions. Lacking in a specified resource or quality; (You see you might be wealthy in material things but poor in thinking... which am afraid am getting into that conclusion)....... Also look what I wrote They are Still Poor and they dont have a house ...... Did you see the AND......(means ni masikini na hawana hata nyumba) Hope am understood.

What does this have to do with me getting married kama naoa na watu wanataka kunichangia nitakaa???????
 
Nguli na wengine,

Naanza kufarijika kuwa jumuiya inayonizunguka inaanza kuona hili. Wakati nakuja Tanzania toka huko nilikuta mambo haya yamepamba moto sana. Sikuwahi kuhisi wala kujua kuwa watu huchangishana na kuamua kuangamiza kiasi kikubwa kama hiki kwa muda mfupi sana. Wakati huo kuna jamaa yangu ndugu alitualika kwenye kikao alichokiita Kikao cha ukoo. Kufika kwenye kikao nikaambiwa kikao cha harusi.

Nilikataa kuchangisha na nikawapa darasa kuwa kwenye ukoo wetu kuna vijana wengi ambao wangeweza kuchangia harusi kam wangekuwa wamewezeshwa kwenye elimu. Nikawaambia na wakakubaliana nami kuwa kweli kwenye ukoo wako ambao walishindwa kuendelea na shule kisa kukosa ada! Mimi nilikataa wazi kuwa siishi kwa kuteketeza fedha kwa siku moja. Tangu wakati huo nimeishi kwa dunia ninayoiamini mimi. Ulifika wakati dini ikanilazimisha nifunge ndoa. Nilikubali kwa kuwa mama yangu alinisihi ili arudi kundini.

Nilifunga ndoa. Ndoa yangu haikuwa na watu zaidi ya 20. Na niliwaalika na kulipia bili kama niendavyo baa. Kidogo kidogo wadogo zangu kwenye ukoo nao wakafata nyayo zangu. Niongeapo sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa elimu wa ukoo. Tunataka mwanaukoo yeyote asishindwe kuendelea na shule kisa kakosa ada. Baada ya hapo tutaendelea na jamii inatotuzunguka hadi hapo tutakapotokomeza ujinga kijijini kwetu.

Ni wakati muafaka kwa Watanzania wote kuacha mtindo huu wa kuchangisha fedha nyingi kwa sherehe badala yake wawekeze kwenye kuchangishana kwa elimu. wakati fulani huko Kenya utasikia bandiko " FAMILIA YA SO AND SO INAKUKARIBISHA KWENYE HARAMBEE YA KUMCHISHIA MTOTO WAO ANAYEENDA KUSOMA MAHALI FULANI" na believe me wamefanikiwa sana. Why not us? Harusi ni suala ambalo ni very personal, wenzetu hagharimiakia shughuli hizi kwa mifuko yao sio kutegemea mifuko ya watu.

Kama ni kuiga TUACHE SASA!
 
Jamani msilaumu tu unajua watu wanachangisha sababu nao walikuchangia ndio hivyo inavyoenda sasa wewe unalaumu coz ushamaliza shughuli yako sio
 
What does this have to do with me getting married kama naoa na watu wanataka kunichangia nitakaa???????

Ninajibu swali lako......... la wewe ulilouliza kuhusu kuwa na nyumba na utajiri (naona unachanganya issues).....

point yako ya watu wanataka kukuchangia naona tunarudi kwenye square one.... thats how things used to be..... watu wako wa karibu walikuwa wanakuchangia na kila mwenye uwezo alikuwa anakuchangia (sio kwa pesa tu vitu mbalimbali) (those were the good old days) fast forwad to these days....... mchango equals kadi = kualikwa kwenye sherehe = madeni kwa aliyechangiwa sababu mchango ni mkopo
 
Ni tabia mbaya sana tuliyoizoea, nimeichukia sana, hivyo kweli mil20 kwa harusi? mimi pesa kama hizo naoa wake 20! na sherehe nafanya, watakula pilau na nyama!, tuache ujinga!
 
Mimi naunga, kama siungi mkono.
Kwanza nadhani ni muhimu watu kuchanga kwa harusi ya ndugu na rafiki. ni alama ya umoja, support na pia social responsibility ya wale wanao jiweza toward wale wenye ku-strugle. kwa hiyo ukipew mchango wa harusi usikatae, ni rizki yako.
Ila naona sio vizuri sherehe ya harusi kua ya kifahari kuliko uwezo wa wenye harusi. It is ridiculous kutumia milioni 10 kwa sherehe ya harusi wakati unaanza maisha ukiwa na milioni 1 benki.
Vile vile haina maana kuchanga laki 5 kwa harusi ya rafiki kama lengo ni kumuona na yeye akikuchangia kwa kiwango hicho siku ya harusi yako ao ya ndugu yako.
Ao tena, sio vizuri kutoa mapesa hayo kwa sherehe ya harusi kuliko kuwapa harusi zawadi ya kitu cha kuanza nacho maisha (kuna watu wanatoa zawadi ya fridge, furniture or anything worth that money).
 
acheni ubahili bana, changieni harusi ili tuujaze ulimwengu, kuna kila dalili kwamba utajaa karibuni.
 
Mtu anaanza kukupigia baada ya miaka mitano.......anajizoeza kupiga siku tatu...siku ya nne, mchango! :redfaces::redfaces:

hii kitu kweli kabisa, kuna jamaa nilikuwa nae facebook, karibia miaka mitatu hatujawasiliana zaidi ya kwa marafiki FB, ghafla mwezi uliopita nikashangaa kanisalimia ghafla..msg iliofata baada ya slamu akaniambia anaoa mwezi huu na kafurahi saana kuwasiliana na mimi.... nilimweleza ukweli kuwa hali si nzuri. Chat ikaishia hapo hapo lol
 
Ngumu sana kuindoa hii tabia bila ya any enforcing mechanism.

Ningekuwa mimi ndiyo govt, ningetunga ka-regulation kadogo chini ya income tax act na kufanya ungangari ufuatao:

1) vikao vyote vya maadalizi lazima viwe registered - otherwise it's illegal with a Tshs 2M fine when found. Inawezekana bana!!

2) kodi (say 25% ya michango yote) zikatwe na zielekezwe kwenye barabara, pembejeo, shule na hospitali.

Inawezekana bana!
 
Nimeacha kuchangia harusi na sherehe zote. Kwenye shughuli yangu ya harusi sihitaji pia mchango wala zawadi kwanza nyumba yangu ni ndogo, kupokea zawadi za mchina.
 
Nguli na wengine,
Naanza kufarijika kuwa jumuiya inayonizunguka inaanza kuona hili. Wakati nakuja Tanzania toka huko nilikuta mambo haya yamepamba moto sana. Sikuwahi kuhisi wala kujua kuwa watu huchangishana na kuamua kuangamiza kiasi kikubwa kama hiki kwa muda mfupi sana. Wakati huo kuna jamaa yangu ndugu alitualika kwenye kikao alichokiita Kikao cha ukoo. Kufika kwenye kikao nikaambiwa kikao cha harusi. Nilikataa kuchangisha na nikawapa darasa kuwa kwenye ukoo wetu kuna vijana wengi ambao wangeweza kuchangia harusi kam wangekuwa wamewezeshwa kwenye elimu. Nikawaambia na wakakubaliana nami kuwa kweli kwenye ukoo wako ambao walishindwa kuendelea na shule kisa kukosa ada! Mimi nilikataa wazi kuwa siishi kwa kuteketeza fedha kwa siku moja. Tangu wakati huo nimeishi kwa dunia ninayoiamini mimi. Ulifika wakati dini ikanilazimisha nifunge ndoa. Nilikubali kwa kuwa mama yangu alinisihi ili arudi kundini. Nilifunga ndoa. Ndoa yangu haikuwa na watu zaidi ya 20. Na niliwaalika na kulipia bili kama niendavyo baa. Kidogo kidogo wadogo zangu kwenye ukoo nao wakafata nyayo zangu. Niongeapo sasa hivi tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mfuko wa elimu wa ukoo. Tunataka mwanaukoo yeyote asishindwe kuendelea na shule kisa kakosa ada. Baada ya hapo tutaendelea na jamii inatotuzunguka hadi hapo tutakapotokomeza ujinga kijijini kwetu.
Ni wakati muafaka kwa Watanzania wote kuacha mtindo huu wa kuchangisha fedha nyingi kwa sherehe badala yake wawekeze kwenye kuchangishana kwa elimu. wakati fulani huko Kenya utasikia bandiko " FAMILIA YA SO AND SO INAKUKARIBISHA KWENYE HARAMBEE YA KUMCHISHIA MTOTO WAO ANAYEENDA KUSOMA MAHALI FULANI" na believe me wamefanikiwa sana. Why not us? Harusi ni suala ambalo ni very personal, wenzetu hagharimiakia shughuli hizi kwa mifuko yao sio kutegemea mifuko ya watu. Kama ni kuiga TUACHE SASA!


Nimefarijika sana na huu msimamo wako, kuna mama hapa ofisini tumemchangia elfu 20 mpaka sasa hapokei salamu yangu. Kwa vile ili upate kadi lazma utoe 50 elfu imagine. Kwa sasa tunasema inatosha niko mbioni kutunga wimbo ambao nitalipia garama za studio mimi mwenyewe kuhamasisha kutokuchangia garama za harusi na badae tufanye kama ulivyofanya wewe hakika tunaweza.
 
Nimaecha kuchangia harusi na sherehe zote. Kwenye shughuli yangu ya harusi sihitaji pia mchango wala zawadi kwanza nyumba yangu ni ndogo, kupokea zawadi za mchina.

Mpwa mm nasubili mwaliko tu na nitakuja na kijiko bila kusahau ndizi.
 
Si lazima kufanya sherehe kubwa ya ufahari, hususan kama unategemea michango.
 
Back
Top Bottom