Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Huu utamaduni si wa muhimu kabisa maana watu wanachangishana na wanahakikisha wamekula pesa zote ingekuwa afadhali katika michango yote iliyochangwa maharusi wanatengewa fungu lao hapo kama asilimia 20 hivi la kuanzia maisha.

Inabidi pia tuanze kuchangishana kutafuta ada za shule na si harusi
Hebu sema neno moja kati ya kuchanga au kutochanga achana na mambo ya asilimia!
 
kwahiyo wewe unaona kama una wajibu wa kutoa msaada, mpaka mtu akukumbushe kwa kadi?????, wewe kama unajua jamaa yako anafanya sherehe je mpaka usubili akukumbushe kwani wewe huoni???, fanya issue yako kwa uwezo wako.... kama uwezo wako mdogo usitake mambo makubwa..... michango kwa kawaida ya culture ya kitanzania (hutoa ndugu wa karibu), watu wengine hutoa shukrani zao kama zawadi kwa maharusi sio kuchangia bia na vyakula ambavyo wanakwenda kuvila wenyewe......

Sasa ndugu yangu kwani umesema kadi ya mchango ndo utamaduni wa kipuuzi au kuchangia?

kwahiyo kosa ni kukumbushwa kwa kadi sio?
 
Sasa ndugu yangu kwani umesema kadi ya mchango ndo utamaduni wa kipuuzi au kuchangia?

kwahiyo kosa ni kukumbushwa kwa kadi sio?
Ndo maana mi sipendi majournal!
 
Kwakweli ni upuuzi na upumbavu. Watu wanataka kufanya mambo makubwa. Mwanamke anataka awaoneshe mashostito zake kwamba na yeye sasa anaolewa na ndio maana wanaume wanajiminya sana katika harusi.
Mi itabidi nifunge ndoa ya mkeka. Sitaki gharama.
hao mashostito si ndo wanao mchangia ama?
 
Kuchanga ni hiyari..changa huwezi potezea..
 
Sasa ndugu yangu kwani umesema kadi ya mchango ndo utamaduni wa kipuuzi au kuchangia?

kwahiyo kosa ni kukumbushwa kwa kadi sio?

The all notion ya Harusi kama culture yetu na utamaduni wetu ulivyo (hii ilikuwa ni shughuli ya kifamilia mtu unafanya sherehe yako kulingana na uwezo wako) watu wanakuja kujumuika na wewe kusherekea...... sasa mambo yakaanza kubadilika.... (watu kuweka kamati za harusi na kupisha michango)......., kutumia michango hiyo kutengeneza kadi ili kupelekea watu wachange....... hii inafanya hata wale ambao sio wahusika wa karibu kupewa priority (hapa priority sio ukaribu wako na mwenye harusi bali ni mchango kiasi gani umetoa)...... Hapo basi watu wanachanga pesa nyingi lets watu 100 people.... ambavyo pesa hiyo ni nyingi sana kiasi kwamba ungeweza kufanya sherehe kwa kiasi kidogo.

Baada ya Harusi waliofunga ndoa..... wanakuwa wana madeni sababu wote waliokuchangia wanaexpect na wewe utarudisha fadhila (tena mtu kama ametoa 200,000/=) atakuwa anaexpect the same amount..... Kumbuka sasa huu mzigo sio wa kamati ya harusi tena ambayo ilileta ile bajeti ya ajabu.... ni ya hawa maharusi ambao ndio wanaanza maisha.... SO THE ALL NOTION IS UPUUZI LETS GET BACK THE WAY WE USED TO.... HARUSI IS A ONE DAY OCCASSION DO IT BY YOUR OWN MEANS.... KAMA MICHANGO TUTATOA ZAWADI... MTU AKIPITISHA MCHANGO WA KUWANUNULIA MAHARUSI KIWANJA WAANZE MAISHA NITAWAELEWA ILA SIO MICHANGO YA KUKODI UKUMBI WA SHS NGAPI SIJUI WAKATI HALL ZA KAWAIDA ZINGETOSHA
 
hivi nyinyi ni nani aliyewambia watu wanaanza maisha wakioana? kwahiyo mzee watu Malecela alipooana na Mama anne kilango walikuwa wanaanza maisha pale? mzee madiba na mama graca walipooana walikuwa wanaanza maisha pale..so wangechangiwa hela ya kununua kiwanja na sio bia na chakula? au wangepewa asilimia 20 ya kuanzia maisha...let the harusi industry grow, btw inasaidia kukuza ajira na kuondoa umasikini
 
Sioni tatizo liko wapi, michango sio lazima, ukitaka toa usipotaka hewala
 
hivi nyinyi ni nani aliyewambia watu wanaanza maisha wakioana? kwahiyo mzee watu Malecela alipooana na Mama anne kilango walikuwa wanaanza maisha pale? mzee madiba na mama graca walipooana walikuwa wanaanza maisha pale..so wangechangiwa hela ya kununua kiwanja na sio bia na chakula? au wangepewa asilimia 20 ya kuanzia maisha...let the harusi industry grow, btw inasaidia kukuza ajira na kuondoa umasikini
Listen ndugu yangu takujibu swali moja baada ya jingine
Ndio watu wakioana ndio wanaanza maisha...... (tunaongelea majority, %age, nipe statistics za watu wanaoa for the first time na wale wa 2nd au 3rd time... kwahiyo its still stands watu wengi wanoa ndio wanaanza maisha na wengi huwa hata nyumba hawana... wanaenda kupanga)

Wedding Industry Grows ( Grows kwa faida ya nani unajua kuna kitu kinaitwa economy cycle; mzunguko wa pesa na pesa je inakuwa injected kutoka wapi na vipi???......) hii inanikumbusha kukuza ajira kwa kuwa na mabaa mengi sababu tunapata kazi za mabar maid na wabeba soda.....
 
Jamani mtaendelea ku-beat around the bush lakini at the end of the day ukiletewa kadi ni uamuzi wako kuchanga au kutochanga which means ukichanga harusi utahudhuria na usipochanga kwenye harusi vile vile hautahudhuria wala kupewa kadi, na mnaposema kuchangia elimu na kadhalika sio lazima kutoa hela cash naweza kwenda kumnunulia mwanafunzi husika sare za shule na viatu na vitabu hapo tayari nimemuwezesha kwenda shule
 
kwakweli ni upuuzi na upumbavu. watu wanataka kufanya mambo makubwa. Mwanamke anataka awaoneshe mashostito zake kwamba na yeye sasa anaolewa na ndio maana wanaume wanajiminya sana katika harusi.
Mi itabidi nifunge ndoa ya mkeka. Sitaki gharama.

mbona kabla ya kuchangiwa kwenye harusi zenu hamsemi hivyo mkiisha changiwa na kufunga ndoa ndio mnaanza ohoooo eti ni upuuzi na upumbavu haya banaaa
 
which means ukichanga harusi utahudhuria na usipochanga kwenye harusi vile vile hautahudhuria wala kupewa kadi

Thats why ninasema the all notion ya Harusi (kulingana na mila na tamaduni zetu) imebadilika Harusi imekuwa sio tena jamaa kwenda kujumuika na mwenzao na kusherekea sherehe yake (you need to pay for the ticket like in some sort of a show)........ that's why I asked NI NANI ALILETA HUU UTAMADUNI WA KIPUUZI
 
Inaonyesha ni watu wengi sana wamechoshwa na huu uchangiaji wa harusi, ila ninashangaa ni kwa nini watu hatuchukui hatua! Mfano kuna hii email nimeipokea leo....,Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa
inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka
kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza
kukuomba mchango.

Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya
watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na
kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna
familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji
ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao
zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku
wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa
wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti
na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia
milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?

Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa
anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda.
Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi,
ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.
Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu
mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa
(na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya
msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa
tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo
uje ubadilike wenyewe!.

Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale
ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha
ufukara na kuviza maendeleo.

Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na
kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa.
Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae
nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July
2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia
elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia
nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.
Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.

Dr. D.R.Olomi
Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania
Important Notice:
 
mbona kabla ya kuchangiwa kwenye harusi zenu hamsemi hivyo mkiisha changiwa na kufunga ndoa ndio mnaanza ohoooo eti ni upuuzi na upumbavu haya banaaa

Speak with facts..... Je unamjua mr husninyo..... Amesema atafunga ndoa ya mkeka sasa ni nani alimchangia
 
Yaani jambo hili kumbe linakera kila mtu eeh! Kama umechangiwa, basi unaweza kuchangia kwa hao waliokuchangia, kwa kuwashukuru kwa kusema asante!
Unajua ndio maana ndoa nyingi za kifahari hazidumu! Maana watu wametoa kwa manug'uniko sasa baraka itoke wapi? Mie nafikiri cha maana ni kufunga ndoa, mengine ni kufuru tu. Tena utakuta watu wameleeewa ile mbaya!
Mie niko nawe mtoa hoja, nilishapunguza sana kuchangia, na kama ukiiniita kwenye kamati ndo kabisa siji. Unakuwa na kadi 10 na kila moja ina kiwango cha 50,000/= utafikiri wanajua badget yako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
thats why ninasema the all notion ya harusi (kulingana na mila na tamaduni zetu) imebadilika harusi imekuwa sio tena jamaa kwenda kujumuika na mwenzao na kusherekea sherehe yake (you need to pay for the ticket like in some sort of a show)........ That's why i asked ni nani alileta huu utamaduni wa kipuuzi

Je umegundua baada ya muda au miaka mingapi kuwa huu ni utamaduni wa kipuuzi?
Je umechanga au kuchangiwa na wangapi ndipo ulipokuja kugundua ni utamaduni wa kipuuzi?
 
Back
Top Bottom