Acheni kulalamika tu chukueni hatua, acheni kuchangia. Mimi nilishaacha kuchangia harusi huu mwaka wa tatu sasa na watu wemeshanijua na wala hakuna anayeniletea kadi.
Sijui unaishi katika jamii ya namna gani ndugu yangu, nadhani watu wamalazimika kukuzoea kwa tabia yako hiyo.
Any way, kuna wakati michango ya harusi inazuia kufanya shughuli nyingine za maendeleo, lakini hii tabia imeshakuwa ni mazoea sasa, na inapokuja kwa mtu ambaye ni wa karibu (Mtoto, kaka, Dada, house maid n.k) kwa kweli tunalazimika kuwaambia wale marafiki zetu washiriki pamoja nasi kusheherekea siku yao ya kuanza maisha.
Tukienda katika ideal condition, bwana harusi anaafford chakula chake pamoja na mke wake na wasimamizi wao, baada ya hapo nadhani ndipo concept ya michango inakuja, kwamba watu tunapenda tushiriki nao chakula baada ya ibada, jambo ambalo haliko kwenye uwezo wa walio wengi, hivyo tunahimizana kuchangia kile chakula na gharama za maandalizi.
Ukiangalia gharama zinaongezeka kadiri idadi inavyozidi kuwa kubwa (ingekuwa wageni ni 2-10 wanaweza kukaa kwenye sitting room nyumbani kwao, sasa mmekuwa 300, inakuja gharama za ukumbi, MC nk, ingekuwa unataka kuchanga TZS20,000/= sasa inalazimika kumegwa kiasi iende kucover hizo gharama nyingine)
Nachokiona mimi ni kuwa kuna haja ya sisi waTanzania kujenga tabia ya kuprioritize mambo kwa umuhimu wake, tumeona watu wakichanga millions of shillings kwa ajili ya harusi lakini hawawezi kukutana na mahitaji yao ya muhimu, mfano elimu bora kwa watoto wao, kuwahudumia wana ndugu wagonjwa na masikini n.k. Mimi niliwahi kuhudhuria kikao kimoja na nilishangaa kuona ndugu ambaye mara nyingi hulia shida akichanga TZS 200,000/=, nikajiuliza hivi angechanga hata robo ya hicho kiasi angekuwa amefanya kosa? Anyway, ifike mahali tuwekeze nguvu kwenye mambo ya maana zaidi, tusikie kuna harambee za kupeleka watoto masomoni, kujengeana nyumba bora, kupeana mitaji ya kuanzisha biashara n.k
Good day.