Kuchangia sharehe ya harusi ni lazima kutokana na culture yetu na event yenyewe. Kwanza kufunga ndoa ni jambo zuri na jema sana hivyo kupongezwa ni lazima, sasa mnataka kupongeza bila kunywa na kula nguvu za kupongeza - vigelegele na vifijo mtazitoa wapi? Nani akulipie wakati una uwezo? Uliza wazee wako na wale wengine wa zamani for sure watakuambia zamani huko vijijini walikuwa wanaalikwa kwenye harusi bila kuombwa michango lakini ilikuwa very clear kwamba kila anayealikwa anafika kwenye harusi tena hata siku mbili kabla lakini akiwa na aidha debe la unga, kidumu cha maziwa, nusu gunia la maharage, mkungu wa ndizi. Sasa sisi huku mjini na siku hizi tunatoa pesa badala ya vitu.
Jambo ili ni la kitamaduni halitakwisha kabisa, labda nenda kaishi huko Kenya au subiri Federation labda mambo yatakuwa kama huko Kenya au huko Kenya yatakuwa kama Tanzania. Kwanza huko Kenya watu wanaalikwa na wanakwenda na vinywaji vyao yaani kunakuwa na mini bar halafu wananunua, sina uhakika na chakula. For sure tukichukua mwelekeo wa Kenya bado utalalama tu, kwani utadai kuwa hauna pesa ya kuisogelea ile mini bar!!!
Kuchangia kunahitaji busara kwani usichangie wakati nyumbani hakuna chakula, mtoto anahitaji ada, n.k. Pia changia kutokana na uwezo wako hata kama wameweka kima cha chini. Pia toa sababu za msingi za kuwa financially constrained.
Rate ya uchangiaji inaendana na ukubwa wa network yako, uwezo wa networks, na age. kama ni age ya kuoa na kuolewa tarajia kadi nyingi sana once your generation is done with marriage kadi zitapungua. Issue inakuja kwa yale majamaa ya generation yako yanapochelewa kuoa na kuolewa - hata ile harusi haipendezi kwani high table inakuwa imejaa mizee!!
Suala la elimu ni jukumu la mzazi na serikali kwani huko tunapeleka michango yetu kwa jina la KODI. Kodi zetu ziboreshe elimu ili watoto wetu wafaulu vizuri. Pia wazazi wasizae watoto kibao ambao hawataweza kuwapeleka shule. Upande wa wagonjwa, ili pia ni jukumu la serikali kwani huko tunapeleka kodi yetu ili kuboresha huduma. Hivi wazazi kulala mzungu wa nne ni uzembe wa serikali au mume wa yule mzazi? Ni serikali isiyokusanya kodi na kupunguza safari za ovyo ovyo.
Kwa kifupi kuchangia harusi sio tatizo kabisa, tunaliona ni tatizo kwa sababu ya ugumu wa maisha. Sasa tutafute kiini cha ugumu wa maisha hapa Tanzania. Kuchangia harusi ni value ya culture yetu na wazee wetu hapo awali waliweza kwa kufanya kazi kwa bidii - kilimo, kwa nini sisi tushindwe au tuache?