Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Kuna kipindi watu walichangisha mpaka humu JF. Tabia mbaya sana. Inazidi kutujenga kwenye mawazo ya uombaomba.
 
Kuchangia sharehe ya harusi ni lazima kutokana na culture yetu na event yenyewe. Kwanza kufunga ndoa ni jambo zuri na jema sana hivyo kupongezwa ni lazima, sasa mnataka kupongeza bila kunywa na kula nguvu za kupongeza - vigelegele na vifijo mtazitoa wapi? Nani akulipie wakati una uwezo? Uliza wazee wako na wale wengine wa zamani for sure watakuambia zamani huko vijijini walikuwa wanaalikwa kwenye harusi bila kuombwa michango lakini ilikuwa very clear kwamba kila anayealikwa anafika kwenye harusi tena hata siku mbili kabla lakini akiwa na aidha debe la unga, kidumu cha maziwa, nusu gunia la maharage, mkungu wa ndizi. Sasa sisi huku mjini na siku hizi tunatoa pesa badala ya vitu.

Jambo ili ni la kitamaduni halitakwisha kabisa, labda nenda kaishi huko Kenya au subiri Federation labda mambo yatakuwa kama huko Kenya au huko Kenya yatakuwa kama Tanzania. Kwanza huko Kenya watu wanaalikwa na wanakwenda na vinywaji vyao yaani kunakuwa na mini bar halafu wananunua, sina uhakika na chakula. For sure tukichukua mwelekeo wa Kenya bado utalalama tu, kwani utadai kuwa hauna pesa ya kuisogelea ile mini bar!!!

Kuchangia kunahitaji busara kwani usichangie wakati nyumbani hakuna chakula, mtoto anahitaji ada, n.k. Pia changia kutokana na uwezo wako hata kama wameweka kima cha chini. Pia toa sababu za msingi za kuwa financially constrained.

Rate ya uchangiaji inaendana na ukubwa wa network yako, uwezo wa networks, na age. kama ni age ya kuoa na kuolewa tarajia kadi nyingi sana once your generation is done with marriage kadi zitapungua. Issue inakuja kwa yale majamaa ya generation yako yanapochelewa kuoa na kuolewa - hata ile harusi haipendezi kwani high table inakuwa imejaa mizee!!

Suala la elimu ni jukumu la mzazi na serikali kwani huko tunapeleka michango yetu kwa jina la KODI. Kodi zetu ziboreshe elimu ili watoto wetu wafaulu vizuri. Pia wazazi wasizae watoto kibao ambao hawataweza kuwapeleka shule. Upande wa wagonjwa, ili pia ni jukumu la serikali kwani huko tunapeleka kodi yetu ili kuboresha huduma. Hivi wazazi kulala mzungu wa nne ni uzembe wa serikali au mume wa yule mzazi? Ni serikali isiyokusanya kodi na kupunguza safari za ovyo ovyo.

Kwa kifupi kuchangia harusi sio tatizo kabisa, tunaliona ni tatizo kwa sababu ya ugumu wa maisha. Sasa tutafute kiini cha ugumu wa maisha hapa Tanzania. Kuchangia harusi ni value ya culture yetu na wazee wetu hapo awali waliweza kwa kufanya kazi kwa bidii - kilimo, kwa nini sisi tushindwe au tuache?
 
Kuna kipindi watu walichangisha mpaka humu JF. Tabia mbaya sana. Inazidi kutujenga kwenye mawazo ya uombaomba.

Tunajua kuna baadhi ya dini harusi zao zikichangiwa itakuwa issue kubwa kwani mfano wanaoa mwezi wa ramadhani na ku-divorce baada ya idd pili!! Hivi serikali yetu kuwa ombaomba ni kwa sababu ya kuchangishana michango ya harusi?
 
Habari wanajf,sijawahi kuanzisha thread yoyote ila leo nimeona hili jambo linanikera na linazidi kukua.Kuna tabia ambayo sidhani kama ni nzuri hapa Tanzania.watu wanakuwa wanataka kuoana na wanaishia kuchangisha watu.

Mtu unajikuta unacard hata 8 ndani na zote zinahitaji michango!Wengine hata huwajui na wanakudai mchango kama vile ni deni!Wenzetu wa nchi nyingine harusi ni suala la mtu binafsi na hawamchangii.

Mfano Kenya wanafanya harambee kuchangia elimu na sio harusi.Ila hapa Tz tunaishia kuchangia harusi ila mtu mgonjwa au aliyekosa ada ya shule hachangiwi.

Najua kuna nitakaowakera hapa ndani kwasababu tayari washapeleka card zao kwa watu. Ila kwanini tusianzishe kampeni ya kuacha kuchangia harusi?Sidhani kama nia ya kufunga ndoa ni kula na kunywa!Mtu kama hana hela ya kufanya sherehe afunge ndoa na kutulia nyumbani kwake.Naombeni mawazo yenu please!!

Toa data ili tujue kama michango imezidi kwa wakati huu. Je population growth inachangia kuongezeka kwake? lete data hapa.
 
Kumbe watanzania matajiri hivyo 2ngekuwa na matumizi mazuri ya pesa ugumu wa maisha ungepungua tatizo tunapenda sifa za kijinga
 
mitz inapenda kutoa michango ya harusi kwa sababu inatolewa mara moja wakati ada ya mwanafunzi ni mpaka amalize kusoma ndio maana inakuwa ngumu sana.
pili tunaishi kwa kuogopa..
 
Siku hizi kutoa mchango ni kwa lazima tu, hata usipohudhuria kikao cha harusi wanakupigia simu kisha wanaweka laudi spika kila mtu anasikia unachosema kwenye kikao,
 
Toa data ili tujue kama michango imezidi kwa wakati huu. Je population growth inachangia kuongezeka kwake? lete data hapa.

we unahitaji data za aina gan ili uelewe? mambo mengine hayahitaji hata upewe data ndo yaeleweke! haijalishi kuwa kuna population growth or not! Sikatai kwamba harusi ni jambo la heri, ila watu tufanye harusi kwa kuangalia tuna uwezo gani!

Mtu anataka afanye kitchen party, sendoff na harusi kwa kuchangisha watu! Kama huna uwezo kwanini usifunge ndoa tu na kutulia nyumbani kwako? Mi kwa kweli sion logic ya kuchangia harusi!

Kuna wakati mtu unajikuta unashindwa kufanya mambo yako ya maendeleo kwa kuishia kuchangia starehe za watu! Kwa mwezi unakuwa na card sio chin ya tano!!

For sure I am tired!
 
watz tunapenda sana kitu inaitwa 'status' hivyo wengine wako radhi kupata hata 'artificial status'.
logically kama watu (ndugu, jamaa na marafiki) wanaweza kuchanga 15m ili wazitafune siku moja alafu baada ya hapo mhusika anaelekea kwenye nyumbani (chumba na sebule), hakuna kiwanja wala msing mwingine wa kuanzia ...ni kwa nini msikubaliane mkatumia 2m alafu 13m apewe akaanzie maisha kwa masharti ya kununua vitu vya msingi kama nyumba.
Lakini hapo mswahili hauelewi, anatake apande Porsche na afanyie Mlimani City ka waliomtangulia (just washirika tu)
 
Mi naona swala zima la harusi za kitanzania halijakaa vizuri. Hata mtu asipoomba michango, bado ataingia gharama lukuki mpaka aoe. Kuna vitu viiiingi vya kijinga jinga vinakula hela kuliko hata harusi yenyewe. Nimeamua kuviweka kwenye thread inayojitegemea, na hizo ni kwa harusi ya kawaida kabisa!
 
Siku hizi kutoa mchango ni kwa lazima tu, hata usipohudhuria kikao cha harusi wanakupigia simu kisha wanaweka laudi spika kila mtu anasikia unachosema kwenye kikao,

hahahahaha
,....hivi ee? umenifunza la maana leo....ahsante sana.
 
Kama wewe bado kujiwekea priorities, basi hayo mambo ya kadi yatakusumbua sana.
Mbona rahisi tu? u najieleza ukweli wako baso maisha yanaendelea,
Ila kuna wakati zinafululizana harusi za watu muhimu sana, inabidi ujitume zipite salama. Hakikisha unajenga mahusiano mazuri na wote.
Uzuri siku hizi watu wanaelewa.
mimi principle yangu ni kuwa sichangii mtu nisiyemjua, hata kama ni dada/kaka wa rafiki yangu wa karibu.
Na mie kadi zangu huwa napeleka kwa watu wa karibu sana yani watu wenye kumpenda mwenye harusi au wenye ulazima nae kama wazazi tu. Sipeleki kadi ofcn wala kwa rafiki zangu.
Pia Sipokei kadi kwenye vikao vya harusi ili kwenda kuchangisha, unless wamesha identify na kuongea na mhusika, mie nakuwa nawakilisha kadi tu.
 
watanzania wote sasa tujivue magamba katika hili hasa michango ya arusi
 
Duh! kweli inaboa, yaani mimi binafsi huwa napenda hii culture ibadilike, lichukuliwe kuwa ni jambo la kifamilia na watu wafanye kadri ya uwezo wao hii ingesaidia pia ku-motivate watu wa wafunge ndoa.
 
Watu wengine jamani huwa hawana aibu,unakuta mtu hamjaonana karibu miaka mitatu siku anakutafuta mnaonana unaanza kufurahi,unashangaa anakutolea kadi ya mchango ha!! kuna watu wanajua kuchuna sura.
 
yani hata miminimechoka wana jamii manake hata birthday watu wanaomba mchango eti wanakuja na kitambaa cha sare ya birthday eti wanataka uwachangie bado uvae sare ya birthday, zawadi, kumtunza mama wa mtoto mh aibu imezidi.
 
Back
Top Bottom