Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna kipindi watu walichangisha mpaka humu JF. Tabia mbaya sana. Inazidi kutujenga kwenye mawazo ya uombaomba.
Habari wanajf,sijawahi kuanzisha thread yoyote ila leo nimeona hili jambo linanikera na linazidi kukua.Kuna tabia ambayo sidhani kama ni nzuri hapa Tanzania.watu wanakuwa wanataka kuoana na wanaishia kuchangisha watu.
Mtu unajikuta unacard hata 8 ndani na zote zinahitaji michango!Wengine hata huwajui na wanakudai mchango kama vile ni deni!Wenzetu wa nchi nyingine harusi ni suala la mtu binafsi na hawamchangii.
Mfano Kenya wanafanya harambee kuchangia elimu na sio harusi.Ila hapa Tz tunaishia kuchangia harusi ila mtu mgonjwa au aliyekosa ada ya shule hachangiwi.
Najua kuna nitakaowakera hapa ndani kwasababu tayari washapeleka card zao kwa watu. Ila kwanini tusianzishe kampeni ya kuacha kuchangia harusi?Sidhani kama nia ya kufunga ndoa ni kula na kunywa!Mtu kama hana hela ya kufanya sherehe afunge ndoa na kutulia nyumbani kwake.Naombeni mawazo yenu please!!
nilichangia harusi moja kubwa sana mwaka jana. Ndoa hiyo ikavunjika baada ya miezi nane, nataka wanirudishie hela yangu.
Toa data ili tujue kama michango imezidi kwa wakati huu. Je population growth inachangia kuongezeka kwake? lete data hapa.
Siku hizi kutoa mchango ni kwa lazima tu, hata usipohudhuria kikao cha harusi wanakupigia simu kisha wanaweka laudi spika kila mtu anasikia unachosema kwenye kikao,