Watu wengine jamani huwa hawana aibu,unakuta mtu hamjaonana karibu miaka mitatu siku anakutafuta mnaonana unaanza kufurahi,unashangaa anakutolea kadi ya mchango ha!! kuna watu wanajua kuchuna sura.
hata kama sijaonana nae miaka kumi asseee kama msimamo wangu ni kutochanga nitamwambia aisee mimi hapa nimesitisha hili swala tangu muda mrefu sana.... unajua inatakiwa tuishi maisha ya uhalisi wa mioyo yetu bwana.... unampa live hapo hapo yani kupunguza matatizo khaaa
double sh 100000..single 50000Halafu ukipatiwa kadi ya mchango tena yenye kiasi cha mchango
(Double sh .... na single sh......)
utakuta unatumiwa sms ya kukumbushwa, utadhani ni deni lazima ulipe.
hiyo sms imeandikwa maneno ya kuvutia kutoa mchango
Unajitahidi unachangia, huko arusini unaweza usipate
hata maji ya kunywa.
kweli inakera sana.
eeh bwana acha kabisa unaweza kumaliza mshahara wote kwenye kadi siku hizi hata graduation kuanzia kindergaten,la saba,form four,six,chuo zote michango utadhani ni fashion du nakuunga mkono hii ni kero kubwa sana nchini
double sh 100000..single 50000
halafu sasa unajikuta una kadi 5 za dizaini hiyo......yan ni kutiana umaskini tu.
Mi bado sijachangiwa ila tatizo linakuja michango inatakiwa mikubwa sana na ni mingi...je ni lazma kufanya sherehe kubwa km huna uwezo????Na wewe si ulichangiwa? Na kama bado, na wewe si utakuja kuchangiwa someday? Au utafunga ndoa ya watu 10, simple!
Mi bado sijachangiwa ila tatizo linakuja michango inatakiwa mikubwa sana na ni mingi...je ni lazma kufanya sherehe kubwa km huna uwezo????
Yan ni mateso...inabidi serikali iingilie kati kupiga marufuku michango ya harusi aisee au unaonajeIla kweli.. Mazoea tu. Ndio hivyo jamii imesha adopt kuacha ngumu. Roho inakusuta mtu. Sie wanawake ndo ununue sare kuanzia kitchen party mpaka harusi. Mh..
Yan ni mateso...inabidi serikali iingilie kati kupiga marufuku michango ya harusi aisee au unaonaje
Huu ni utamaduni unaotakiwa kupigwa vita, tumeponzwa na hizo siasa za ujamaa na kujitegemea mimi nilishaacha siku nyingi kwani zinalostisha tu familia na zinapunguza pato la nchi kama vipi inabidi tuwambie TRA waanzishe makato kwenye kila harusi.
Subiri mnichangie mimi halafu ndo mpige ban hayo mambo..lol.
Teh utashangaa mmechanga nyingi halafu harusi iko hovyooo then next week unameona bwana harusi amenunua ka VitzWengine wanatafuta mitaji!