Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Watu wengine jamani huwa hawana aibu,unakuta mtu hamjaonana karibu miaka mitatu siku anakutafuta mnaonana unaanza kufurahi,unashangaa anakutolea kadi ya mchango ha!! kuna watu wanajua kuchuna sura.

hata kama sijaonana nae miaka kumi asseee kama msimamo wangu ni kutochanga nitamwambia aisee mimi hapa nimesitisha hili swala tangu muda mrefu sana.... unajua inatakiwa tuishi maisha ya uhalisi wa mioyo yetu bwana.... unampa live hapo hapo yani kupunguza matatizo khaaa
 
hahahahahaaaa umenichekesha sana mkuu..!!
 
Halafu ukipatiwa kadi ya mchango tena yenye kiasi cha mchango
(Double sh .... na single sh......)
utakuta unatumiwa sms ya kukumbushwa, utadhani ni deni lazima ulipe.
hiyo sms imeandikwa maneno ya kuvutia kutoa mchango
Unajitahidi unachangia, huko arusini unaweza usipate
hata maji ya kunywa.
kweli inakera sana.
double sh 100000..single 50000
halafu sasa unajikuta una kadi 5 za dizaini hiyo......yan ni kutiana umaskini tu.
 
Niliogopa kujibu mwanzoni nilipoona hii thread maana watu wengine wanaweza kwazika maana unakuta yuko kwenye harakati ya kuchangiwa. Ila mada ni nzuri na naamini jambo hili lifikie mahala ili turudi kwenye harambe za maendeleo na siyo pesa za starehe.
 
Michango imekuwa ni kero kwa jamii,maana wengine wanaona umuhimu wako pale tu anapotaka umchangie. Niliwahi kumleta baba yangu atibiwe hapa Dar, japo alikaa miezi minne jamaa moja tunayetoka kijiji kimoja na anamfahamu baba yangu na alikuwa na taarifa za ujio wake hapa DAR hakuwahi hata siku moja kuja kumjulia hali hata kwa kupiga simu kwa kisingizio kwamba sehemu niokuwa nimehamia (Tegeta kutoka mwenge, yeye anakaa Kinondoni) ilikuwa mbali na hakuwa na mtu wa kumleta. Sasa baada ya muda akawa anaoza kijana wake,,kwanza akanipigia simu niwe kati ya wanakamati ya maandalizi, NIKAUCHUNA. Hakukata tamaa nilishitukia naletewa kadi ya mchango ofisini, mimi niliiweka kama moja ya mapambo yangu. Alipoona siku zinazidi kwisha jioni moja narudi nyumbani kama saa mbili hivi usiku namkuta jamaa kajaa tele ananisubiri nimpe mchango. Nilimweleza kwamba hela yoote nimemaliza katika kumuuguza baba yangu, alitoka analia kwa aibu. Ukweli sikuchangia harusi hiyo
 
eeh bwana acha kabisa unaweza kumaliza mshahara wote kwenye kadi siku hizi hata graduation kuanzia kindergaten,la saba,form four,six,chuo zote michango utadhani ni fashion du nakuunga mkono hii ni kero kubwa sana nchini
 
Hahahahaaaaaa!!
Sasa kama wameshazoeshana jamani........inabidi wachangiane tu!!!

Ila kadri dau linavozidi kupanda wataacha wenyewe tuuu!!!
 
Hivi hili ongezeko la michango ya harusi siku hizi linatokana na nini maana zamani hii mambo haikuwepo....yan mi naona kila nikipatacho kinaenda kwenye michango ya harusi na kila kukicha naletewa card...mi nishachoka sasa na kuwakatalia siwezi kwa kuwa mtu anakudai kama deni kabisa yan kila saa anapiga simu kukumbushia hadi inakuwa kero...
 
Na wewe si ulichangiwa? Na kama bado, na wewe si utakuja kuchangiwa someday? Au utafunga ndoa ya watu 10, simple!
 
Na wewe si ulichangiwa? Na kama bado, na wewe si utakuja kuchangiwa someday? Au utafunga ndoa ya watu 10, simple!
Mi bado sijachangiwa ila tatizo linakuja michango inatakiwa mikubwa sana na ni mingi...je ni lazma kufanya sherehe kubwa km huna uwezo????
 
Mi bado sijachangiwa ila tatizo linakuja michango inatakiwa mikubwa sana na ni mingi...je ni lazma kufanya sherehe kubwa km huna uwezo????

Ila kweli.. Mazoea tu. Ndio hivyo jamii imesha adopt kuacha ngumu. Roho inakusuta mtu. Sie wanawake ndo ununue sare kuanzia kitchen party mpaka harusi. Mh..
 
Huu ni utamaduni unaotakiwa kupigwa vita, tumeponzwa na hizo siasa za ujamaa na kujitegemea mimi nilishaacha siku nyingi kwani zinalostisha tu familia na zinapunguza pato la nchi kama vipi inabidi tuwambie TRA waanzishe makato kwenye kila harusi.
 
Ila kweli.. Mazoea tu. Ndio hivyo jamii imesha adopt kuacha ngumu. Roho inakusuta mtu. Sie wanawake ndo ununue sare kuanzia kitchen party mpaka harusi. Mh..
Yan ni mateso...inabidi serikali iingilie kati kupiga marufuku michango ya harusi aisee au unaonaje
 
Huu ni utamaduni unaotakiwa kupigwa vita, tumeponzwa na hizo siasa za ujamaa na kujitegemea mimi nilishaacha siku nyingi kwani zinalostisha tu familia na zinapunguza pato la nchi kama vipi inabidi tuwambie TRA waanzishe makato kwenye kila harusi.

Kweli inalostisha sana hasa ukizingatia wanaooa wamekuwa wengiiii na mtu ukimpa hata elfu 50 hataki anataka kuanzia laki....tutafika kweli??
 
Back
Top Bottom