Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania


Unauliza ina maana gani,maana yake vijana wamehamasika kufunga ndoa... Iwe za harusi ama zisiwe za shughuliza kujaza watu..
 
mmoja alikuja kwenye kamati eti hata hela ya gaun la bb arus hana...
alah sasa waoa nn hapo...

sasa kama huyo atataka kuchangiwa hadi hela ya suti..... Kwanini mtuusifanye sherehe ya uwezo wako?

Kuna mmoja alipanga kima cha chini 70,000, hapo bado kicheni pati, nikasema kama mtaniona nyie tumeni msg mpaka vidole viwaume. Mbona sie enzi zetu hatukusumbua watu?
 
heh elfu ngapi?! Tano? Elfu 50.. Kama ni couple Laki moja na kuendelea!! Upo hapo?

tena hizi za viwango ndo sizipendi kabisa! Siku hz mchango wa kichen party eti nao elf 50! Kama sio bange nini hii!
 
Unauliza ina maana gani,maana yake vijana wamehamasika kufunga ndoa... Iwe za harusi ama zisiwe za shughuliza kujaza watu..
Sawa vijana wamehamasika ila wasitake visivyokuwa level yao....mbona zamani walikuwa wanafunga na hapakuwa na hii michango?
 
Afu unamchangia mtu then next wk wanapeana talaka. Huku ni kuleteana hasara tu.
 

We acha tuu, umenikumbusha nikiwa kidato cha 6 msimu wa likizo nikamwomba ndugu yangu 1 nauli akasema mambo yake hayaja kaa sawa,jion nika mpigia wife wake,akasema mbona tumetoka kwenye kikao cha harusi sahiv ya RAFIKI yake na amechangia laki 2!!!!!!!!!! Nilimwaga choz kidogo alafu nikakumbuka me ni mwanaume nikatabasamu kama mtu alicheka sana!!
 
Dah pole sana mkuu...ndo ujue watu wanathamini sana anasa kuliko kusaidiana...unajua kutoa harusini labda kunakupandishia TITLE so watu wanaona kule ndo kunalipa kuliko kumsaidia either mgonjwa au km wewe.....haya maisha magumu sana
 
Teh utashangaa mmechanga nyingi halafu harusi iko hovyooo then next week unameona bwana harusi amenunua ka Vitz

akinunua usafiri atakuwa amefanya la maana kuliko kushibisha matumbo akitoka hapo kafulia.
 
kwani harusi ni lazima au uamuzi.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…