Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

ukitaka iwe mwisho, harusi yako usichangishe mtu. Kuwa mfano wa kuigwa.
Hahahahahaaa lazma niliowachangia wanirudishie hata kidogo...nimechanga nyingi sana aiseee
Ila wewe tutakuchangia usijali
 
dah mkuu hii mambo inachanganya aisee,kamshahara kenyewe haka ka m.kwere
Yan jamaa wa harusi wanasumbuaje....kimapato tunatofautiana ila hawaelewiii....
Yan mtu anaandaa sherehe kupitia michango....Je huu ni uungwana???
 
ni poa sana, tatizo wabongo shughuli bila mapochopocho hawaji hata iwe ni msiba. ww huoni msiba wa masikini na tajiri!
Bongo bana!
Hahahaa siku hizi misibani tunagonga na NDOVU BARIDIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
yan mkishazika mnamsahau marehemu.....ikitokea akafufuka ghafla akakuta mnakula na kunywa....atazimia na kufa tena hapohapo
 
Usichange na wewe usitaraji kuchangiwa.
Mi nshachanga sana...niliowachangia wanatosha tu kunipa campany....hata hivyo sihitaji kufanya sherehe kuuuuuubwaaaaaa wakati maisha ni kujipanga
 
Mi nshachanga sana...niliowachangia wanatosha tu kunipa campany....hata hivyo sihitaji kufanya sherehe kuuuuuubwaaaaaa wakati maisha ni kujipanga

Aah bana ricky fanya sherehe kubwa watu tule..tucheze..tunywe.. Lol.
 
Duh! Huu uzi umenigusa, ni majuzi tu tar 18/02/2012 nimefanya harusi na sasa bado nahisi nipo kihoneymoon honeymoon. Niliamua kwenda kufanyia home huko Mbeya kwa kuogopa hayo hayo ya gharama. Mimi nilijipanga na 4.8mil ili hata ningekosa support niweze kufanya. Niliwaomba watu wachache kama kamati kwa ajili ya kuratibu mambo, wakanipangia 1.5mil na kuona kama watafanikisha. Na wao wakajipangia 30elfu kwa kila mwanakamati na partner wake na wa kadi double 30elfu na single 15elfu. Sikuwaambia kuwa nina kiasi chochote ila niliwaondoa wasiwasi kuwa tutafanikisha, kwenye budget ilikuwa kama 7mil kwa watu 250. Support kubwa kama 2.5mil niliipata kutoka kwa ndugu marafiki wa karibu na kamati wakapata kama 1.5mil. Zilitengenezwa zaidi ya kadi 350 lakini nilitoa warning ya kuzifuatilia kwa wasiotaka maana najua inasumbua sana na nilitaka pia kupunguza idadi ya watu wa kuendelea kuwachangia. Kwa hiyo nadhani kuna watu walifurahi sana ambavyo sikuwafuata wala kuwatafuta kwa kukumbushia kumbe ulikuwa ni mtego pia kujua marafiki wa kweli. Waliokuwa tayari ndo waliojitahidi kunichangua bila ya kuwasumbua na kuwakumbusha. Nilicho fulahi ni kwamba ilifanikiwa kwa kiasi nilichokuwa nataka. Nilichoshangaa kuna watu kibao huko nyuma nimewachangia sana tuu lakini ilipofika yangu walinikaukia kana kwamba hatufahamiani na wakati kwenye harusi zao walikuwa wanalazimisha na kukumbushia utadhani wananidai vile.
My take kwa vijana wenzangu: please, kama hujajipanga achana na mambo ya harusi kubwa maana kuna jamaa mmoja ameahirisha zaidi ya mara2 harusi yake kisa eti michango watu wanatoa kidogo. Panga kufanya harusi ya uwezo wako na ikitokea ikawa zaidi ni jambo la kheri.
 
Hahahaa siku hizi misibani tunagonga na NDOVU BARIDIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
yan mkishazika mnamsahau marehemu.....ikitokea akafufuka ghafla akakuta mnakula na kunywa....atazimia na kufa tena hapohapo

haaaah haaah mnakula then mnashushia na castle lite dah haah haaah, kwa hali hii masikini watazikwa na nani sasa?
 
Aah bana ricky fanya sherehe kubwa watu tule..tucheze..tunywe.. Lol.
Ni sawa Amy...hata ikiwa kubwa ntakomaa mwenyewe bila kusumbua watu..si unajua ukiwachangisha watu na wao utalazimika kuwachangia...ntakuwa nashughulika na wagonjwa tu
 
Hapa nimepata kadi tatu za wafanyakazi wenzangu, nikipiga mahesabu na zile nne nilizopata wiki iliyopita inabidi niandae si chini ya laki mbili, kweli hii michango ni ya kupiga vita.
 
Hapa nimepata kadi tatu za wafanyakazi wenzangu, nikipiga mahesabu na zile nne nilizopata wiki iliyopita inabidi niandae si chini ya laki mbili, kweli hii michango ni ya kupiga vita.
Hapa laki mbili tu??? Mh we ngoja utajionea mwenyewe labda uwape 20,000/-
 
ni poa sana, tatizo wabongo shughuli bila mapochopocho hawaji hata iwe ni msiba. ww huoni msiba wa masikini na tajiri!
Bongo bana!

mapochopocho muhimu ila kama bora ualike watu wachache ambao unajua una uwezo wa kuwahudumia.
 
Hahahahahaaa lazma niliowachangia wanirudishie hata kidogo...nimechanga nyingi sana aiseee
Ila wewe tutakuchangia usijali

kama utataka wakuchangie jiandae kuendelea kuchangia watakapotaka kuozesha watoto wao, jiandae kuwachangia hadi ndugu zao. Solution ni kufanya harusi ya kichoyo. Ndugu kumi upande wa mke, kumi upande wa mme wanatosha sana kunogesha sherehe na watakula hadi wasaze bila kuwachangisha hata sh moja.
 
habari tanzania....huwa najiuliza bila majibu ya uhakika,kuna umuhimu gani wa mtu anaogopa kufunga harusi kisa sherehe ambayo hata ukichangiwa bado inatumika yote kwenye sherehe?nafikiri we have to change tuwe tunachangishana kwenye mambo ya dharura na siyo harusi ambayo unaweza enda kwa kanisa au shekhe na kumaliza hiyo shughuli bila ya kuleta usumbufu kwa watu.nawasilisha
 
dah......
Umenitonesha kidonda.....
Mfanyakazi mwenzangu kaka yake anaoa..50,000
mfanyakazi mwenzangu anaolewa 50,000
kuna harusi 2 kwenye kikundi chetu 100,000
binamu zangu 2 wanaoa na kuolewa 100,000

khaaaaa......!!!!!
 
Mna pesa za kuchezea. . . .
 
Back
Top Bottom