Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mimi sku hizi nawatosa, maana kuna na watu wazima wamekaa ten years wanatusumbua na harusi zao eti
 
nadhani sasa m2 akitaka kuoa au kuolewa,wajipange sio kuchangisha watu cz ts becaming too much.ela yote yaishia kwenye michango mpk unashindwa kufanya maendeleo yako... au wadau mnasemaje?

ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa_nina kadi sita hapa kwenye droo ofisini....bado zilizoko home,.....zingine mwanakamati....yaani sijui nani katuloga...lo!
 
Za kwenu muliwachangisha watu za wenzenu its too much
jirekebisheni
 
sawa sio lazima uchange lakini unakuta ofisini kuna watu km wanne hv wanaoa na kuolewa,then mtaani huko nako km umepanga mtt wa mwenye nyumba naye anaoa umeletewa kadi bado marafiki zako nao wanakuomba uwachangie... yaani kasheshe kwakweli.maisha yanazidi kuwa magumu na hii michango... alafu siku hz ukitaka kuchangia unaambiwa kianzio 70000 tena hapo kakufanyia kishigaji tofauti n ahapo ni 100000.duh tutafika kweli?
 
changia tu kadili ya unavyo jaaliwa... sio lazima lakini. jiamini kwa unalo amua kufanya.... tatizo letu tunadhani mahusiano yataboreka zaidi kwa kuchangiana tukumbuke wachangishaji wazuri sio watoaji wazuri usitegemee watakuchangia na wewe... hivyo ukiamua kuchangia changia usifanye kama unakopesha
 
Yah,hata mimi hili jambo linaniboa,ivi kibongo bongo kwani huezi kwenda kanisani na mtarajiwa wako na watu wachache ambao unaweza kuwamudu kwa pesa yako,yani ufanye sherehe kutokana na mfuko wako rather than depending on others kufanikisha ur dream wedding
 
kha! wadau bora michango ya harusi. mi nliletewa kadi ya mchango wa birthday yan nlichoka akili mwili na damu. . . saiv naanza kuzipotezea make nahisi nafanyia kazi michango tu!
 
kha! wadau bora michango ya harusi. mi nliletewa kadi ya mchango wa birthday yan nlichoka akili mwili na damu. . . saiv naanza kuzipotezea make nahisi nafanyia kazi michango tu!

Kuna hili la birth day na kipaimara sijui wanaita ubarikio lol,hapana kwa kweli!
 
Mimi nilijaribu mwaka mmoja kuweka orodha ya michango kwenye excel ilizidi 2M. Kwanini watu hawabadiliki??hata kama mlichangia watu ndo tuendeleze utamaduni wa kuumizana??? kwani lazima ufanye sherehe kama huwezi kugharimia??? ndo mwanzo wa kuishi maisha ya kuigiza
 
Changieni tu jamani,ndiyo mabadiliko hayo.Enzi za bibi zetu kulikuwa hakuna send off lakini siku hizi kuna hadi kitchen part ambayo kihalisia binti alitakiwa kukaa na somo na shangazi chumbani lakini sasa tunachangia na ukumbi unakodishwa!
 
Kwanza wadada ndo mara nyingi wanataka harusi ya Gharama!!! Loh badilikeni, maisha ni zaidi ya harusi!!!
 
Hii inatokana na watanzania kupenda kula na kunywa kuliko pitiliza!
 
Wazimbabwe wanatuchekaga sana ktk hili, wanasema badala ya kuchangia mtu aende shule au akatibiwe sisi tumeng'ang'ana na harusi tu
 
Sisi ni WAJAMAA tulilolelewa kwenye UJAMAA unategemea nini?nyie mnaolalamika BABA na MAMA zenu tumewachangia wakafunga NDOA wakawazaa nyie na KAKA NA DADA zenu tumewachangia wakaoa na kuolewa kuweni wapole kama unacho changa kama huna sema huna mnalalamika pembeni sababu mnakikimbia KIVULI chenu kulingana na nilichokieleza hapo juu.
 
Back
Top Bottom