Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mimi nilishaliweka wazi hili, ugonjwa na kifo nitachanga. Habari ya harusi sijui graduation sitaki kusikia.
 
SMH. Kuna umuhimu wa ndoa ya mkeka.

Ama sivyo ndoa ya moyoni tu mtu anakuwa "significant other".

Harusi unatumia milioni ishirini halafu maisha unaanza kwenye chumba kimoja uswazi.
 
nadhani sasa m2 akitaka kuoa au kuolewa,wajipange sio kuchangisha watu cz ts becaming too much.ela yote yaishia kwenye michango mpk unashindwa kufanya maendeleo yako... au wadau mnasemaje?

Halafu kuna mijitu ni mijinga sijapata kuona.

Yaani hata ku-reason nayo haiwezekani.

Ukiiambia kwamba maisha ni magumu, people are barely making ends meet, haielewi.

Yenyewe inataka tu kuunguza mamilioni ya shilingi siku ya harusi.

Mtu kama unataka harusi ya gharama kubwa kwa nini usiigharamie mwenyewe kuliko kusumbua watu wakuchangie....
 
Hahahahaha! Kumbe mmeliona eeee! Mimi nilishaachana na hiyo biashara. Ni Upumba.. kabisa. Eti mtu anapanga chumba kimoja harafu hataki harusi inayolingana na uwezo wake? Shen.. kabisa. mimi siku hizi sikatai kadi za michango ila zote zinaishia dust-bin. Tumezoea sana watanzania kugawana umaskini. Bora ndoa zenyewe zinazoharibu budget zetu zingekuwa zinadumu basi, mwaka haujaisha watu wameachana harafu eti tuendelee kuharibu budget? Kudadade..
 
tatizo hata kama unataka harusi ndogo, wazazi wanakwambie wao wamechangia sana lazima wachangishe hata kama upendi. infact kwenye maswala ya harusi, kama una wazazi huna maamuzi. inakera sana
 
Nyie wote mnaopinga mmeshaoa au kuolewa? Kama ndiyo, harusi zenu ziliwezeshwa na akina nan? Nina kajamaa flani hapa, wadau tulijichangisha mpaka harusi ikafana japo haikuwa na gharama kubwa. Leo ni mtu wa kwanza kupinga michango harusi. Tumemwambia kama anaona ni gharama basi arudishe michango yetu tuliyomchangia ndo apinge. Siyo siku mnaoa mmechangiwa sasa mnapoanza kudaiwa fadhila na waliowachangia mnaanza kuruka kimanga. Hamna hiyo, lazima mchangie, unless kama hukuchangiwa kwenye harusi yako basi tulia wala haikuhusu hiyo michango. Ukipokea lazima utatoa ujue!
 
kha! wadau bora michango ya harusi. mi nliletewa kadi ya mchango wa birthday yan nlichoka akili mwili na damu. . . saiv naanza kuzipotezea make nahisi nafanyia kazi michango tu!

Hahaha hyo kali CL,never met one like that. mingi ni harusi, kubariki ndoa(after10-15years of coitus),kipa imara nk. Mimi nimependa kuna baadhi sasa wanaomba michango ya mambo ya maendeleo kama kwenda shule! Seen 3 guys wamepata scholarship wao wameweza ku-raise half of the amount sasa wanatafuta nguvu ya ziada. Thatz better,nachanga kwa roho safi. Kenya wenzetu Harambee kama hizi zimewafikisha mbali sana.
 
Bado sijawa kwenye system yakuchanga wala kuchangiwa,
Ila kwakiasi flani michango inaboa sana kwakweli, unakuta kwa wiki mtu unaletewa kadi 3 had 4 na zote sio chini ya shilingi 15-elfu...,
 
tatizo hata kama unataka harusi ndogo, wazazi wanakwambie wao wamechangia sana lazima wachangishe hata kama upendi. infact kwenye maswala ya harusi, kama una wazazi huna maamuzi. inakera sana

Harusi yako au ya wazazi?
 
Harusi yako au ya wazazi?

Kiranga huyo dada ana point.. kwa mila zetu za kiswahili... Utasikia watu wakisema " mama flani anaozesha mwanaye" mara nyingi wazazi ndio wanataka makuu.. wanaona fahari harusi ya bint/ kijana wao inapokuwa kubwa mno
 
nadhani sasa m2 akitaka kuoa au kuolewa,wajipange sio kuchangisha watu cz ts becaming too much.ela yote yaishia kwenye michango mpk unashindwa kufanya maendeleo yako... au wadau mnasemaje?

Mimi nimeshastaafu kuchangiachangia, naona ni unafiki tu, yaanai badala kusaidia wazazi wako nyumbani watu tumeandamwa na michango. Nimepoteza marafiki wa 4 wananichukia kisa sijawachangia harusi yao. Poltelea pote, ndoa nitafunga bila kuomba thumni ya mtu. kUNA RAFIKI YANGU MMOJA NAYE YUKO mentally liberated amefunga harusi ya sh elfu 50, hapahapa dar, na ilifana ni ya kuigwa. Njoo uombe mchango wa kununua kiwanja nitakupa si harusi
 
Halafu kuna mijitu ni mijinga sijapata kuona.

Yaani hata ku-reason nayo haiwezekani.

Ukiiambia kwamba maisha ni magumu, people are barely making ends meet, haielewi.

Yenyewe inataka tu kuunguza mamilioni ya shilingi siku ya harusi.

Mtu kama unataka harusi ya gharama kubwa kwa nini usiigharamie mwenyewe kuliko kusumbua watu wakuchangie....

Mie kwa mtazamo wangu huu kama unataka kuoa/kuolewa ita ndugu wa karibu sana na wewe then sema ya moyoni lakini habari ya kupeleka kadi ya mchango Kigoma kwa mtu ambaye mlikaa naye siti moja kwenye basi mkapeana namba sa simu no kwa kweli kama ni mimi sichangi ng'ooooo.

Kaka/dada cku ukitaka kuoa/kuolewa nakwambia utaona michango yenyewe hiyo hata bado haijatosha
 
Mimi nimeshastaafu kuchangiachangia, naona ni unafiki tu, yaanai badala kusaidia wazazi wako nyumbani watu tumeandamwa na michango. Nimepoteza marafiki wa 4 wananichukia kisa sijawachangia harusi yao. Poltelea pote, ndoa nitafunga bila kuomba thumni ya mtu. kUNA RAFIKI YANGU MMOJA NAYE YUKO mentally liberated amefunga harusi ya sh elfu 50, hapahapa dar, na ilifana ni ya kuigwa. Njoo uombe mchango wa kununua kiwanja nitakupa si harusi
aisee mdau unasema kweli? tshs 50 elfu? seriously nauliza. nimependa idea yake ila alifanyafanyaje kwa 50 elfu?
 
kuna siku nilikuwa napitia page moja hivi "I Love Being Black" nikakutana na mdada mmoja wa kiMarekani kafanya shughuli yake ya arusi kwa pungufu kidogo ya USD 4000. Nkajiuliza hivi kwanini sisi tunapenda macomplicado?

nikagundua sisi tunapenda mno matukio, yawe mazuri au mabaya...(i stand to be corrected).
hebu angalia mtu anapokuwa mgonjwa tunapojivutavuta then akifariki wanajamii tunavyojistretch mifuko yetu ili "tukio" la msiba liende kwa heshma "zooooote"...

unakuta kuna mtoto wa ndugu waliofariki (yaani ni yatima) kusoma kwake kunakuwa na msukosuko saaaaana. akifanikiwa akasema sasa anaoa au anaolewa,tunajistretch mifukoni kwaajili ya "tukio" la arusi ili liende kwa heshima "zoooote"....

tubadilike,tukianza wachache kubadilika, wengine naamini watafuata...
 
mimi nilishaliweka wazi hili, ugonjwa na kifo nitachanga. Habari ya harusi sijui graduation sitaki kusikia.

mi leo kuna mmoja kaniacha hoi. Kaniita kanaiambia oh sijui kuna mtoto sijui wa nani yangu anao namba unichangie. Nikamwambie mh nnazo nyingi ndani tayari akaniambi eti hata elfu ishirini tu najua hutakosa, nusura nimwambie naziokota eeh!!
 
Watu tuna complicate sana mambo, Haingii akilini mtu anaishi nyumba ya Kupanga hana hata Baiskeli halafu anataka harusi kubwa na anakodisha six door, Huku arusha kuna jamaa angu mmoja ni Dreva wa Tours na ana pesa laini siku ya Ndoa yake alienda yeye na Mwenzake wawili tu kwa Padri na hakutaka hata kuwa sumbua marafiki zake kwenye ishu ya Usafiri alitembea kwa mguu hadi geto kwake na baadae jioni akatoka wakaenda Pub kuchoma nyama na marafiki zake na alitumia 50,000 tu, So mpaka mwisho alitumia 50,000 tu kwenye harusi yake, na mpaka sasa hivi wanaishi kwa amani kabisa
 
Mi nina harusi ya mwana natakiwa nitoe lak 5 nimeduwaaa, but as long ni mwana from primary, kitaa, chuo na hata kwenye career tunagumiana. Daily mjini lazima nijisachi tu japokuwa roho inauma maana budget ipo deficit
 
Mi nina harusi ya mwana natakiwa nitoe lak 5 nimeduwaaa, but as long ni mwana from primary, kitaa, chuo na hata kwenye career tunagumiana. Daily mjini lazima nijisachi tu japokuwa roho inauma maana budget ipo deficit, na nataman harus ya mwana ipendeze as tumesota pamoja
 
Back
Top Bottom