Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
saa hizi tuko busy na kuchangia huduma za afya na elimu kwa wasio na uwezo.nilishaacha siku nyingiiiiiiiii kuchanga, tena wasivyo na adabu wameweka na viwango!! ndio kabisaaaaaaaa, yangu yakinikuta nitajua mbeleni! ila kwa sasa hell no! imekuwa ni business, unajikuta u spend a lot kwenye hii makitu!
Sijawahi kuwa na utaratibu wa kuchangia harusi, ukiwa na shida nyingine your mostly welcome, wabongo wanapenda sana sifa za kijinga, unajua huna uwezo fanya kile chenye uwezo wako, usipomchangia ndo ujue umeshakuwa adui yake na kukununia juu.
mkuu naomba nichangie ada ya mtoto ya shule hata laki2
Hoja yako nimeependa
sana.
Kweli kuna watu wanatoa taarifa ndani ya muda mfupi. Mfano Mwezi mmoja
au miwili. Hapo usipomchangia anakuja leta lawama kibao.
Pia kuna wengine wanapanga kufunga ndoa miezi ya Dec, Jan, na february.
Kwa kweli miezi hii haijakaaa vizuri kwa michango ya harusi.
Mwezi Dec. ni maandalizi ya sikukuu ya X-mass pamoja na ada za watoto
shuleni.
Mwezi January pale bado tunachakalika na ada.
February tunalipa madeni tulikokopa ili kulipa ada za watoto.
Hivyo mimi binafsi miezi hii mtu akiniletea adi au kunialika kikao cha
harusi itakayofanyika miezi hii, najua huyu ananitafuta ubaya tu.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Ni kweli, mwenyewe nilibaki kinywa wazi maana wote niliowachangia hasa classmates ukiachilia mbali ndugu wa karibu hakuna hata mmoja aliyenichangia. Mtu anakuahidi lakini mwishowe anapotea. Bila kuwa na hela yangu mwenyewe ningetia aibu.kati ya wale niliowachangangia mimi ni asilimia 5 tu ndio waliokuja kunichangia. hivyo basi wanaochanga eti kwa sababu na wao watakuja kuwachangia itakapofika siku yao nawapa pole sana. sio wote watafanya hivyo. bora usave visent vyako kwa mambo ya msingi zaidi.
Wala mie sikuwahi kuchangisha mtu! Mimi na mke wangu tulikubaliana tusisumbue watu, tukamaliza kwa gharama zetu!vitu vingine kuingizana umaskini tu,yuko Lindi anakudai mchango halafu hata sio rafiki kihivyo,amua mwenyewe ukimpa sawa ukimnyima sawa. Halafu kashakupangia kabisa kima cha chini laki moja we ulishawahi kuomba mchango kwake?
Mee too inanikera xana nina kadi 4 za workmates wanasema najiwekea hazina ya wachangiaji kwenye harusi yangu while marriage is not on my life plan list
Wala mie sikuwahi kuchangisha mtu! Mimi na mke wangu tulikubaliana tusisumbue watu, tukamaliza kwa gharama zetu!
Halafu kuna watu ukiwauliza 'kwa nini msifanye harusi ndogo tu ambayo haihitaji mamilioni ya pesa' wanakushangaa.[/QUOTE
Ok, wanakushangaa! Wakati hata hizo ndoa zao za mamilioni zikidumu sana, mwaka! Hii laana?