Kwanza kabisa, wakuu hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje wakuu?
Naomba kuwasilisha.