Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mkuu mimi huwa sitoi michango ya harusi kabisa, hakuna haja ya harusi kunigharimu ka faida kangu kadogo nakokapata kwenye vibodaboda vyangu.

 
Aisee harusi ni mtaji kuna dada alipewa kparty mil4 sendoff akapewa 15.6 sasa harusi sijajuaaaaa ni capital kwa kweli
 
utakuta mtu anatamba kufanya sherehe ya 15n alaf yeye ana 2m. hii ni kuwapa watu majukum/mzigo usio lazima. fanya sherehe kwa pesa yako.
na kingine ni kuwatajirisha wenye kumbi tu et ukumbi unakodishwa 4m.
 
Mi sitaki hata kusikia hz habari. Harusi yangu nilifunga bila kuchangisha watu. Sherehe ilikuwa family level ndugu zangu na ndugu wa upande wa mume wangu basi. Na watu walikula kunywa na kutosheka. Sikutaka shobo za kuchangishana kufuatana fuatana mara usemewe mbovu kisa michango.
 
I believe jamii inaelimika sana sherehe kubwa za harusi zitakw sio big deal tena. Kwa wale waliofanikiwa kutochangia harus hongereni. Na wale ambao bado tunachangia tunatoa lkn 95% kwa kunung'unika sana na kuumia coz ni ndugu, jamaa au rafiki huna jinsi. Kwa hii trend tutafika mahali huu utamaduni utachange completely kila mtu atafanya harusi ya uwezo wake sio kutegemea michango
 
Inakera sana me kuna jamaa nilimwambia kua nimeacha utaratibu wa kuchangia harusi izo message alizonifurumishia hatari..
 
cha kushangaza kijana anaomba msaada sh 500,000 kama mtaji afanye biashara hakuna aliye tayari kumsaidia ila akitangaza harusi hata mil 20 atachangiwa!

Watu wapo busy na michango ya harusi lakini Ukiitisha michango ya Ada ya Shule au kuuguza Mgonjwa hawaji wanagoma kuchanga ! Lakini kuchangia harusi kwa sisi watu Weusi ni Utamaduni ambao bado ni Analogia sana,Wazungu wao hawana huu uzushi ,huwezi ukamkuta Mtu anamsumbua Mtu juu ya mchango wa Harusi ,Wazungu wao Harusi hufanya pindi Bajeti ikiwaruhusu tu,hawalazimishi Harusi wala kuwasumbua watu na michango.
 
Moja ya Tamaduni mbaya iliyosalia Tanganyika ni hii ya kuthamini Harusi Kuliko Ugonjwa na Ada ya shule, watu wapo tayari kununiana kisa Mtu hajamchangia kwenye Harusi yake ! Michango ya Harusi sasa ni Majanga imekuwa Kero ,Watanzania ni wepesi wa Kuiga Tamaduni za Ulaya lakini hapa kwenye Michango bado wamesinzia ! Wachina,wahindi,wazungu huu usumbufu walikwisha achana Nao kitambo ! iweje sisi weusi wa Tz tunauendekeza?Kwanza 50% ya wanandoa ni Full michepuko ndio nyingi zimejaa lawama na migogoro,Watu wanachanga kwa kujinyima kisha Michepuko inashika Kasi hatimae ndoa kuvunjika ! Pesa za michango ni Bora sasa zielekezwe kwenye kusaidiana shida Sugu ikibidi watu wachangiwe kujenga nyumba kwa wale masikini sana,watu wachangie wagonjwa,Hii kero ya michango haina budi sasa ikemewe na Katiba mpya .
 
Inakera sana me kuna jamaa nilimwambia kua nimeacha utaratibu wa kuchangia harusi izo message alizonifurumishia hatari..

Ni kweli Michango ya Harusi imesababisha wengi hawaongei wamenuniana,Kibaya zaidi watu wanaendekeza Harusi huku Wagojwa na wanafunzi wakikosa misaada.
 

Hapo umenena mkuu, "RAHA ZAKE ZITUPE SHIDA SISI" kama hana uwezo anatangaza harusi ya nini? Mpaka anageuka ombaomba.
 

Watu hupenda Ku-copy vya Wazungu ,sasa kwa nini Watu wasiige hii Tamaduni ya Wazungu ambapo wao hawachangishi Mtu kuhusiana na Harusi ,Wazungu huamini ktk kualika watu waje kusherekea tu si kuwasumbua kuchangia Harusi Binafsi ambayo hawana Uhakika Kama Ndoa itadumu .
 
Hapo umenena mkuu, "RAHA ZAKE ZITUPE SHIDA SISI" kama hana uwezo anatangaza harusi ya nini? Mpaka anageuka ombaomba.

Ni kweli sasa Harusi Zimewafanya watu Kuwa Omba omba kibaya wakati mwingine watu hujua mapema Ndoa haitadumu kutokana na Matabia mabaya ya wenye harusi,lakini Michango hung'ang'anizwa na wakati mwingine huleta Uhasama pindi watu wakigoma kuchanga.
 

Wameiga wapi? Kumbuka Wazungu hawana Michango ya Harusi ! Huko kuiga ni kwa sisi kwa sisi tu ! Katiba Mpya ipige Marufuku michango ya Harusi lakini ihamasishe watu kuchangia Wagonjwa na wanafunzi masikini waliokosa Ada.Harusi ziwe Digtal si lazima watu wale wanywe Kama huna pesa Binafsi tulia pika Ugali kuleni siku ipite.msilazimishe mambo makubwa wakati Uwezo Hakuna !
 

Michepuko bado ni Majanga wengi huwa hawachani na wapenzi wao wa zamani matokeo yake ni Watu kuchangia Pesa nyingi lakini ndoa nyingi hazidumu,
 
Hii pia inasababisha watu kukosana maana unaweza kuwa unamatatizo kibao muda huo lakin jamaa akiona hujamchangia anakuchukia....!! Tujifunze kujiandaa wenyewe.

Michango ya Harusi ni full majanga
 
Watu wachangie Ada za shule na Wagonjwa Michepuko imezidi sasa michango ya harusi haina budi ifutwe
 
Tabia ya u-ombaomba michango ya arusi inakera sana. Watu wanapenda ufahari wkt hawana uwezo. Kaa na ndugu zako wa karibu muandae shughuli. Msitusumbue sisi watu baki (majirani)
 
Tabia ya u-ombaomba michango ya arusi inakera sana. Watu wanapenda ufahari wkt hawana uwezo. Kaa na ndugu zako wa karibu muandae shughuli. Msitusumbue sisi watu baki (majirani)

Kama vp iingizwe kwenye katiba itamkwe hv ni Mwiko kwa wana Ndoa au watarajiwa ndoa kuwasumbua watu juu ya Michango ya Raha zenu,Pia Harusi isiwe ni Jambo la lazima pindi ndoa zinapofungwa ,tujifunze toka Ulaya wazungu huwa hawachangishi Michango juu ya Harusi hujipanga wenyewe kisha ndugu,jamaa na rafiki hualikwa kubunja msosi pasipo kusumbuliwa na mtu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…