CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,357
- 6,424
Hivi ni sawa jamaa anataka kuoa hana hata sent mfukoni anategemea michango ya washkaji...?...Mi naona Harusi BOMBA ni ile jamaa anaandaa kila kitu anawaita washkaji kwenda kushuhudia,kumpongeza na kumpa zawadi....Au wana JF mnasemaje..?
Ni kweli wengine kuchangia harusi ushakuwa ugonjwa. Atasahau hata kulipa ada za wanafunzi anahangaikia nichango ya harusi. Watu kama hao wape kadi za mchango zisizo na kiwango ili wachange kwa kutafuta sifa.ukiwachangisha watu hawapendi wanapenda kula bure ...hata kama ni sherehe yako lakini ni vizur uchangie chochote kitu ...
wengine usipowachangisha hawaji kusherekea pamoja nawew
Nani kakwambia ni hiari. Kama unataka utengwe na jamii, basi usichangie uone..Lakini kuchanga nako ni hiari, si lazima!
Nani kakwambia ni hiari. Kama unataka utengwe na jamii, basi usichangie uone..
Watanzania HAtuna budi tubadilike, mtu alikuwa anauguliwa, hukuwahi hata siku moja kumpelekea matunda au juice kwa ajili YA mgonjwa. Mgonjwa kafariki, mchango wako ni Elfu kumi, Huku ukijua anahitaji chakula kwa ajili YA waombelezaji, gharama ZA maziko kwa mwili wa marehemu NA gharama zote zinazoambatana.
Maziko yanapita mtu kajisimamia mwenyewe kwa Msaada wa Mwenyezi Mungu. Baada ya muda unakuwa na sherehe ZA harusi, unamwendea huyo mfiwa unataka akuchangie LAKI MOJA, akikuambia hana ugomvi, hivi hii ni haki kweli?
Jamani tubadilike na kusaidiana KWENYE mambo yenye tija, sherehe ZA harusi ni MBWEMBWE TU SAY NO TO MICHANGO YA HARUSI
Mtu kama huyu unamwambia live, mie huwa nawaambia kabisaa harusi sichangii ukinipa kadi unapoteza bure.
Kwenye mambo mengine shiriki ipasavyo tena mwanzo mwisho tena ikibidi toa michango mikubwa coz utapoanza kukataa michango wataanza kukufuatilia ushiriki wako katika maswala ya kijamii ili kukubagua.
Kwa mfano amefariki mtu hapo mtaani kwenu, watu wengi hutoa mia tano au buku! Toa hela ndefu kweli kweli ili kuonyesha kwa nini huchangii harusi au sherehe. Shiriki mwanzo hadi mwisho, I mean kuanzia kuchimba kaburi mpaka uhakikishe maziko yamefanyika na penye gape jitolee ipasavyo!!
Ila ukigoma kutoa michango ya harusi na kwenye misiba usionyeshe tofauti siku yakikukuta bro umekwishaa!! Unasusiwa live mbele ya kadamnasi, mi napenda watu mtaani/kazini kwangu wanavyoanza kuniiga msimamo wangu tu. Kifupi wamenikubali kwa sana
Nilishaamua, sichangii tena harusi coz nilipofanya yangu sikuomba mchango wa mtu! Nashukuru na ndugu zangu wakaiga mfano wangu so michango ya harusi nooo....!! Tena ni Big Noooo....!!
Nachangia elimu, magonjwa, misiba na mambo mengine ya maana.
Harusi unafanya ndogo unaalika watu unaowamudu wale, wanywe, wacheze mpaka wachoke, wakitoka hapo wakathimuliane huko mtaani!! Kuoa ukaoe wewe kukuchangia tukuchangie sisi, why??
Nilishaamua, sichangii tena harusi coz nilipofanya yangu sikuomba mchango wa mtu! Nashukuru na ndugu zangu wakaiga mfano wangu so michango ya harusi nooo....!! Tena ni Big Noooo....!!
Nachangia elimu, magonjwa, misiba na mambo mengine ya maana.
Harusi unafanya ndogo unaalika watu unaowamudu wale, wanywe, wacheze mpaka wachoke, wakitoka hapo wakathimuliane huko mtaani!! Kuoa ukaoe wewe kukuchangia tukuchangie sisi, why??