Najua kwamba kutoa ni moyo na sio utajiri ......... na Waa Tanzania kuchangiana ni jambo la kawaida katika shughuli mbalimbali za kijamii ...... sio siri upande fulani inaumiza lakini kukwepa pia inakuwa vigumu .......Jamani kumbe hii michango mbalimbali tunayotoa ukiijumlisha kumbe ni balaa hebu angalia yaliyonisibu tangu januari hadi sasa na bado
- Michango kwa ndugu zangu 300,000
- Michango kwa marafiki 200,000
- Michango kwa ninaofanyanao kazi 150,000
- Michango kwa ninaosali nao 200,000
- Michango ya ndugu wa mke wangu 200,000 ,,,,,,,,,, hapa imevuka 1m
Michango ya sikuhizi inataja kiwango na kutoa deadline.....kama michango yenyewe ni hiari hilo sijui. Ninachojua ni kwamba sherehe ni watu na watu lazima wale, wanywe n.k ambavyo ni gharama.
Changia rafiki wa karibu, ndugu au jirani ili mujumuike kufarahi pamoja. La kama unataka kuchangia kila mtu hapo tatizo ni la kwako.
Unachanga elfu 50 halafu siku ya sherehe unaenda kukutana na juisi ya Azam ya kopo
Mi kiukweli wazazi wangu washachanga sn ila nikaona sio issue.
Ctaki kumchangisha mtu!
Ht mwanaume wangu Nitamwambia na tukubaliane no kamati, ndugu wa karibu tu tunawapa plan yetu tunataka iweje basi.
Tunafanya kutokana na uwezo uliopo
Na ikitokea imechangwa pesa kwa watakaotaka kuchanga bajeti ni ile ile hyo nyingine bora tufanyie mambo ya muhimu. ...
Mambo ya kufanya sherehe kubwa baada ya sherehe mnaanza kuhangaika maisha magumu ctaki kabisa.